simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Pasaka Njema … Happy Easter

with one comment

Fumbo la mwili wa Kristu. Imani kubwa inahitajika kulielewa. Wayahudi hawakuelewa … ‘tutakulaje mwili wa mtu?’ Yesu alisema: ‘Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu …’ TAFAKARI kuhusu imani yako na endapo inakufanya ‘Uwe sura na mfano wake’ katika jamii unamoishi.

Sanamu ya Mt. Fransisko wa Asizi. Alijipa jina la ‘Ndugu Mdogo’. Aliacha utajiri mkubwa aliokuwa nao baba yake ili apate kumtumikia Kristo. Ana mengi ya kutufundisha. Baadhi ya maneno kwenye sala yake ni pamoja na:

‘BWANA unifanye chombo chako cha amani’

‘BWANA unijalie kupenda, kuliko kupendwa’
‘Unijalie kutumikia, kuliko kutumikiwa’

Unaweza pia kuongeza:

‘BWANA unijalie kutenda haki, kuliko kutendewa haki’

Niwatakie nyote PASAKA njema. Ujumbe mkubwa tangu siku ya Alhamisi Kuu ni: UPENDO. Ile amri iliyo kubwa kushinda zote. Upendo. Mapendo. Wakati huo huo ni muhimu kuheshimu namna ambavyo kila binadamu hapa duniani amejaliwa kumjua Mungu. Bila shaka kupitia njia hiyo kila mmoja anajitahidi KUWA sura na mfano wa Mungu. Maana Mwenyezi Mungu anasema katika Kitabu cha Mwanzo … Alitazama kila kitu alichoumba, aliona kwamba kila kimoja kilikuwa chema, tena chema sana. Daima tuanze kutazamana katika wema (ulio ndani mwetu) kuliko kuhukumiana. HAKI.

Siku kuu njema. Uwe chombo cha kueneza amani, utulivu, haki … na utaweza hayo tu ikiwa utakuwa mtu wa IMANI na MAPENDO. Tupo pamoja.

Advertisements

Written by simbadeo

April 8, 2012 at 12:08 pm

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. Pasaka njema nawe pia…

    Like

    yasinta/kapulya

    April 8, 2012 at 2:28 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: