simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Mnada … Maswali

leave a comment »

Nimekutana na mkusanyiko huo mahali hapa jijini Dar. Kutokana na matangazo yaliyokuwa yakiendelea hapo kwenye vipaza sauti ni kwamba kulikuwa na mnada. Mnada huo ulihusisha bidhaa anuwai: majokofu, redio kubwa na ndogo, simu za mkononi, pasi za umeme, feni, computer (laptop), seti za luninga, blender na vingine vingi.

Kwa kawaida bidhaa hizo huuzwa kwa bei ya maana madukani. Lakini hapa hakuna chochote kati ya hivyo kilichouzwa kwa zaidi ya shilingi elfu 80, hata hiyo computer aina ya Dell.

Nimebaki na maswali mengi. Mnada ni moja ya njia za kuuza bidhaa ulizo nazo. Lengo la kufanya biashara ni kutengeneza faida. Sasa, ikiwa mtu unauza kifaa ambacho kwa kawaida ungetoza laki nane (800,000/-), iweje leo ukiuze kwa elfu sitini (60,000/-)? Simu ya elfu 50, uiuze kwa elfu 10. Blender ya elfu 30, uize kwa elfu nane? Kweli?

Ninafikiri kuna mushkheri mahali. Au kuna utapeli unaendelea na bidhaa hizo hazina ubora unaostahili, ama bidhaa hizo zilipatikana kwa njia isiyo halali na kwa hiyo hata muuzaji akimwachia mtu mwingine kwa elfu 5 au kumi, hana cha kupoteza.

Lakini … vipi kuhusu kodi? Serikali inastahili kodi yake, au sivyo? Je, kodi hiyo inakwenda vipi serikalini?

Nafikiri, vyombo vinavyohusika vifuatilie kikundi hiki. Isije ikawa watu wamepata njia ya kuwapiga chenga FCC … wanaingiza bidhaa feki na kuziuza chapchap kwa njia ya minada, huku wakikwepa kulipa kodi. Hatimaye tutajikuta kama nchi tumebaki kuwa jalala la matakataka ambayo hata kuyaondoa kwake itakuwa kazi … au itatugharimu sana.

Na labda swali la mwisho, kwa nini kikundi hicho hakikai mahali pamoja kwa siku kadhaa mfululizo?

Haya, leo ilikuwa ni siku ya maswali tu … tuonane wakati mwingine.

Advertisements

Written by simbadeo

April 3, 2012 at 11:41 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: