simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Mwese … Secondary School

with 15 comments

Ni kuelekea Mwese Secondary School. Hatua kubwa hii. Hongera wana-Mwese. Vijana, tumieni vema rasilimali hiyo. Ni kupitia taasisi hiyo ndipo mtajipatia maisha bora zaidi. Kitunze ili kidumu. Picha zote ni kwa hisani ya Mwalimu Mkuu, Bw. Reuben Swilla. Asante mwalimu kwa kutushirikisha picha hizi. Tuna hamu ya kuona zaidi.

Advertisements

Written by simbadeo

March 30, 2012 at 10:49 am

Posted in Siasa na jamii

15 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Wawooo! kweli hayo ni maendeleo, hongereni sana wana mwese kwa kupata secondary.

  Like

  Rugwiza Hassan. ( Hassan Ismail)

  April 1, 2012 at 10:56 pm

 2. Congrass mwese, you’r potential,make it, it will be.

  Like

  Eudes Munyandamutsa.

  September 8, 2012 at 6:35 pm

 3. Ninawapongeza sana kwa hutua kubwa kama hiyo yakujipatia shule ya Secondary vijana hakuna kulala kwani tuko kwenye nyakati za Technology hivyo sina budi kusema kwama elimu ni msing wa maendeleo.

  Like

  Godfrey SEKIMONYO

  September 27, 2012 at 4:40 pm

 4. Since the establishment of mwese residents there was no good times as it is in these very recent days, youths were very good at schools but since there was no school to go after primary education completion only the few who had relatives out of mwese could be taken by their relatives and proceed with studies out of mwese so it is the right time for those who are there to work hard and hard to show that the plan to build a school there was not a wrong one.

  Like

  Sixto Sanoyingoma

  October 6, 2012 at 12:40 pm

 5. Hongera sana wana mwese kupata secondar! zamani uione wapi hapo mwese?

  Like

  Cherishi Mlambo

  April 23, 2013 at 2:10 pm

  • Naam, Ndugu Cherishi, ni kweli, hii ni hatua muhimu. Hata hivyo, sote tuna wajibu wa kuwasaidia vijana wanaosoma katika shule ile kuelewa kwamba hiyo ni haki ya kipekee waliyopata na wasiichezee kwani maisha hayaji mara mbili.

   Like

   simbadeo

   April 27, 2013 at 10:42 am

   • Hapo nimekusoma ndg, ni kweli tunahaki ya kuwasaidia na tusisahau tulipo toka.

    Like

    Cherishi Mlambo

    September 6, 2013 at 12:14 pm

 6. Hapo nimekusoma ndg, tujifunze kutosahau tulipo toka.

  Like

  Cherishi Mlambo

  September 6, 2013 at 12:17 pm

 7. Hongereni sna mwese kutoka enzi za paskazia makale kuzitafuta shule na hatimae leo yamekuwa.

  Like

  Cherish Mlambo

  May 19, 2014 at 8:13 pm

 8. Namshukuru sana Mwenyenzi Mungu.
  Nimeshtuka! sasa hivi ndo nimeelewa kwamba utandawazi unafika hadi Mwese, sehemu ambayo ina upekee wa aina yake kwangu. Sikufikiria kwamba kuna taasisi huko Mwese ambayo inatumia utandawazi, ingawa nina muda mrefu ninapata habari za Mwese kwa kuzitumia anuani za watafiti (Reseachers) walio nje ya Mwese.
  HONGERA SANA MKUU WA SHULE YA SEKONDARI YA MWESE.
  Mimi nilifika Mwese nikiwa na Miaka mitano, na kutoka huko nikiwa na miaka thelathini na tano. Ndiyo sehemu ambayo naichukulia kama mzizi wa maisha yangu na kwa kweli, maisha yangu nahisi kwamba yameambatana sana na Mwese ingawa nina miaka ishirini tangu nitoke huko kuelekea RWANDA. Nimeshindwa kabisaaa kuachana na Mwese katika mawazo yangu, naiwaza, kuikumbuka hata kuiota Mwese mara nyingi kiasi ambacho wakati mwingine nahisi kuwa na NOSTALIGIA.
  Hivyo kila nipatapo habari njema kwa Mwese, kama vile tukio la kimaendeleo, moyo wangu husuuzika.
  Nina furaha sana kwamba leo kuna Sekondari, natamani sana siku siku moja kuchangia maendeleo ya taaluma kwa namna moja au nyingine ktk kipindi cha uhai wangu na MUNGU atanisaidia.

  Je naweza kuanza kutoa mchango kwa kuwapatia hasa hasa wanafunzi wa shule hiyo ushuhuda wa namna nilivyokwea ngazi za taaluma kiajabu mpaka kufikia kiwango nilicho nacho sasa hivi?

  NB: Ushuhuda huu si kwa minajili ya kujitapa, la hasha, kwa sababu si kwa uwezo wangu bali ni kwa uwezo
  wake Mola, nimeweza kukwea ngazi za taaluma, kwamba leo Nina USHUHUDA unaoweza kumsaidia
  kijana au mwanafunzi ambaye anaelewa umuhimu wa Elimu na ana vision ya kufika chuo kikuu. Nia
  yangu ni kwahamasisha vijana walioko huko Mwese Kuitafuta elimu.

  Pamoja na maoni yenu, ningependa kupata maoni ya pekee ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya
  Sekondari ya Mwese.

  Like

  Rwaka rwa Kagarama.

  November 16, 2015 at 4:05 pm

 9. Nawasalimu sana wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwese, nikiwatakia kuukamilisha Mwaka huu (2015) salama na kwa ufanisi katika harakati zenu za kukwea ngazi za elimu.
  Kama Mwana wa Mwese ambaye sasa hivi niko nchini Rwanda, ninafurahi sana kwamba sasa hivi kuna wanafunzi wa Sekondari hapo Mwese, Jambo ambalo hapo kale tulipokuwa watoto/vijana ilikuwa ndoto kupata sekondari Mwese. Nakumbuka tulipokuwa tunamaliza shule ya msingi, ni wachache sana walikuwa wanapata bahati ya kuendelea Sekondari maeneo mengine ya mbali (kwa sababu hata Mpanda sekondari zilifika baadaye sana), waliporudi likizoni kutoka sekondari, tuliobaki Mwese tulikuwa tunawaona kama vile ni malaika kutoka peponi (mbinguni) na wamerudi kuivinjari dunia.
  Wanafunzi hao walikuwa wanarudi na mbwembwe za mitindo mipya ya mavazi kutoka mijini, miondoko ya vijana, mnafahamu wenyewe kuwa mitindo ya mavazi kwa vijana huenda sambamba na miondoko ya kiainaaina, aina mpya za dansi, naikumbuka sana bumping ambayo wawili wawili (mara nyingi mvulana na msichana) walikuwa wanasukumana kwa matako, dansi ikishawakolea kama msichana ameshagubikwa na jazba ya dansi na ana nguvu nyingi usipokuwa na tahadhari wewe mvulana anakuangusha chini puuuu !!! umati ndani ya ukumbi unacheka sana. Mambo mengine ambayo yalikuwa ni chanya kwa vijana na yalikuwa yanawavutia vijana walobaki kijijini ni usafi wa watoto kutoka Sekondari. Jambo moja tu ambalo lilikuwa linawaudhi wengi kati ya waliobaki kijijini, ingawa mimi binafsi ilikuwa ni changamoto ya kuisaka elimu kwa uvumba na ubani, ni kuchanganya lugha zetu tulizozoea kama vile kinyarwanda, kibende, kifipa, kichaga, kiswahili na maneno ya kiingereza kama vile IN FACT, OF COURSE, OOH YES, I UNDERSTAND.PLEASE, NO PROBLEM n.k. Hayo yalikuwa yanatuudhi sana lakini useme nini mbele ya mwanafunzi wa Sekondari? ila misamiati mipya ya kiswahili cha mitaani kama vile NDATA (police), NOMA (si nzuri), NIGEE (nipatie) n.k. ilikuwa inatufurahisha sana na tulikuwa wakiondoka tu kurudi masomoni basi, inakuwa ya ule msemo wa kiswahili kwamba PAKA AKITOKA PANYA HUTAWALA, tunaanza kuyatumia maneno hayo mapya ya kiswahili na kuiiga miondoko ya vijana kwa uhuru sana. Nasema kwa uhuru sana kwa sababu, wanafunzi wa sekondari walipokuwa wanakuwepo kipindi cha likizo, waliobaki vijijini tulikuwa tunajisikia duni sana. Unajua kama mnaongea halafu unasikia anasema OF COURSE au IN FACT ulikuwa unapotea kabisaaa, unapata msinyao bayana na kuanza kujiuliza moyoni HUYU SI TULIKUWA TUNAKAA DESKI MOJA JUZI JUZI, JAMANI, KESHANIACHA KABISAAA, MAANA LEO HII HATA LUGHA ZETU HAZIELEWANI, mwenzako akishangamua kwamba una INFERIORITY COMPLEX anakuacha bila hata kukuaga, tena anaondoka kwa mbwembwe na miondoko hiyooo, ukiinua kichwa , unamuona ameshakuacha tena anaondoka kwa mikogo, anapoondoka unasikia ahueni na badala yake unamkodolea macho huku unaitunza aina hiyo ya miondoko ndani ya fikra zako, ili utapoanza kuondoka na wewe kwa mikogo (lakini haooo watakaporudi shuleni) usikosee step.
  Vijana nawaasa kwamba mwanzo wa mada maarufu sana iitwayo UKOMBOZI HALISI, huanzia kwa mtu binafsi kujikomboa. kujikomboa kutokana na umaskini, ujinga na maradhi. Na silaha pekee ya kujikomboa wewe binafsi ni ELIMU. Ukombozi wa Jamii ya binadamu (familia, ukoo, kabila hata taifa, huwezekana pale wanajamii wote au idadi kubwa ya wanajamii wana ukombozi binafsi ELIMU.
  Vijana nawaasa kwamba hiyo ni rasilimali ambayo bado ni adimu Katika nchi za kiafrika. Hesabu ya vijana wanaoendelea na masomo ya juu baada yashule ya Msingi bado ni ndogo sana, Afrika ina asilimia ndoooogo sana ya wanafunzi wa sekondari ukilinganisha na idadi ya watoto wa Afrika, Bado wengi wapo maporini ambako hata elimu ya msingi hawaipati. wengine wanashindwa kuendelea na masomo kwa sababu ya ufukara na vita, ukosefu wa amani na usalama kwa sababu ya udhaifu wa mfumo wa uongozi, pia uongozi usiojali maslahi ya wananchi kwa baadhi ya nchi.
  Ninaamini moja ya nchi za Afrika zilizo na misingi imara inayolenga maendeleo ya wananchi ni Tanzania, yenye mfumo bora kwa manufaa ya wote . Nchi ambayo imekuwa na amani ambayo, vijana mnapaswa kuzitumia kama nyenzo za kila mmoja aliyepo shuleni kuwa na bidii ajiendeleze kwa manufaaa yake na ya nchi nzima, Afrika na dunia. Kumbukeni marais wa nchi na viongozi maarufu kama KOFI ANNAN walitoka vijijini. Naifahamu sana shule ya Wazazi ya Sekondari huko Irambo, Mbeya aliyosomea Rais wa sasa wa Kongo. sijui sasa hivi ikoje lakini kipindi hicho isingeweza kulinganishwa na shule hiyo ya Mwese, hiyo ni zaidi sana.

  VIJANA KWA SASA NIISHIE HAPA TU NIKIWAASA KILA MMOJA KUJISIKIA KUWA NI MMOJA WA WATOTO AU VIJANA CHIPUKIZI WA AFRIKA WENYE BAHATI SANA, KUSOMA SEKONDARI AMBAYO NI NGAZI ITAKOYOWAFIKISHA KWENYE NJOZI ZENU ZA MAENDELEO. NANI ASIYEPENDA MAENDELEO? LABDA MWENYE WALAKINI.
  BAHATI HIYO ITUMIYENI VILIVYO. WAKATI NI HUU,

  Ninapokaribia tamati ya ujumbe huu wimbo uliokuwa maarufu kipindi hichoooo nilipokuwa Shule ya Msingi ya Mwese, na ambao kila asubuhi tulipokuwa tumejipanga mistarini baada ya mchakamchaka kabla ya kuingia darasani, ulikuwa unaimbwa na bendi ya shule ama kwa maneno au kwa ala tu, ulikuwa unaimbwa kwa maneno haya;

  MAISHA YA SHULE NI SAFARI NDEFU,
  MAISHA YA SHULE NI SAFARI NDEFU,
  VUMI, VUMILIAAAAANI SAFARI NDEFU.

  Ninafikia tamati nikimuomba kila mmoja kuupatia uzito na kuzingatia Misemo hii ambayo inaonyesha bayana uzito, nguvu na manufaa ya elimu, misemo ambayo yaweza kuwa moja ya changamoto za yule ambaye anauelewa fika ujumbe huu na kwa kuuzingatia siku moja katika maisha ataukumbuka kama moja ya nyenzo zilizomuinua kufikia BACHELOR, MASTER and PHD Degrees. au elimu aloipata imeweza kumpatia ukombozi binafsi ambao unaweza kutoa mchango wa kutosha hata ktk ukombozi wa taifa.

  * ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA
  * ELIMU NI MSINGI WA MAENDELEO
  *.EDUCATION IS THE POWERFUL WEAPON WHICH YOU CA USE TO CHANGE THE WORLD
  (Nelson MANDELA)
  * ELIMU HAINA MWISHO.

  Wakatabahu.

  Like

  Rwaka rwa Kagarama.

  December 8, 2015 at 12:35 pm

  • Ndugu Rwaka

   Asante sana kwa nasaha hiyo adhimu. Kwa hakika vijana na sisi sote tukizingatia haya, tutajenga kujitambua na kubadili miendendo yetu ili tuwe na mchango bora zaidi kwa jamii nzima ya wanadamu. Nitamtumia Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwese ujumbe huu ili ikiwezekana siku moja ausome kwa wanafunzi. Naamini kipindi hiki wapo likizo, lakini daima wakati utapatikana.

   Kila la kheri katika yote.

   Like

   simbadeo

   December 9, 2015 at 12:02 pm

 10. KUKOSOWA MSTARI WA 21 KUTOKA CHINI KTK UJUMBE HAPO JUU.

  ” Ninapokaribia tamati ya ujumbe huu, kichwani mwangu inakuja kumbukumbu ya wimbo uliokuwa maarufu………..”

  Like

  Rwaka rwa Kagarama.

  December 8, 2015 at 12:48 pm

 11. PAMOJA SANAAAAAAA !!!

  Like

  Rwaka rwa Kagarama.

  December 8, 2015 at 1:14 pm

 12. UMEKUWA MKIMYA NDUGU DEO. VIPI?

  Like

  rwaka rwa kagarama

  February 17, 2017 at 7:06 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: