simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Kiduchu … kutoka Nairobi

with 2 comments

Msikiti katika moja ya mitaa ya Nairobi. Kumwabudu Mwenyezi Mungu ni muhimu sana, au siyo? Hapa ndiyo penyewe kwa dua. Tuombe amani Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla.

Unazikumbuka hizi? Zinaitwa ‘Bedford’. Sina uhakika kama kuna inayotembea katika mitaa ya Dar. Kama ipo/zipo, hebu turushieni picha. Enzi za Vita vya Uganda … ndiyo yalikuwa yanatawala sana katika mitaa ya Bongo. Hii hapa ni katika moja ya mitaa ya Nairobi. Kitunze kidumu. Ya kale ni dhahabu!

Hapa lazima nisimame. Nimekutana na ‘ulevi’. Bei poa Sh300 tu ya kwa Mzee Kibaki. Bongo ni kama Sh6,000 hivi. Bei poa sana.

Mheshimiwa huyu … ninachomhusudu … hachoki kusoma … haweki kitabu chini miaka nenda miaka rudi. Yupo katika bustani za Jumba la Makumbusho la Taifa la Nairobi. Ukifika huko usiache kwenda kumwona na kumsalimu.

Na tufunge basi na hii ya mitaani. Waweza kufurahia walau matangazo hayo … na uhai tele katika mitaa ya Nairobi.

Tupo pamoja. Afrika Mashariki inakua kwa kasi. Inaunganika kwa kasi. Pengine ni muhimu kuona namna gani mtu wa kawaida anahakikishiwa usalama zaidi wa maisha yake na watoto wake. Asaidiwe kumudu elimu, afya, chakula, malazi, hewa, maji bora, safi na salama. Haitakuwa vema kuruhusu ukanda huu wa kiuchumi kuwa wa watu milioni 120 lakini wenye maisha bora 120! Tupo pamoja. Tunaweza kuleta mabadiliko. Tunaweza kutia uhai zaidi katika maisha ya jamii zetu. Pamoja sana.

Advertisements

Written by simbadeo

March 28, 2012 at 11:49 pm

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Miji inakua ila Tanzania suala la uchafu nalo naona linazidi kukua, sasa sijui maendeleo haya yatatufikisha kule tunakotaka kwenda au vipi, hawa wenzetu wanoruka na ndege na kuona miji mingine, mbona hawaigi hayo mazuri basi?

  Like

  Jennifer

  March 29, 2012 at 9:13 am

  • Ni kweli miji inakua – kutokana na mmiminiko wa watu mijini, kuzaliana na kwamba lazima watu waishi. Changamoto kubwa ni katika kufanya ongezeko hilo na kukua huko kuwe na ubora unaostahili. Ubora huo ni pamoja na suala zima la utunzaji mazingira, ikiwemo usafi. Wahenga walisema – mtoto umleavyo, ndivyo akuavyo. Pengine chanzo cha uchafu katika miji na mazingira yetu kipo katika familia zetu – maana ni kwenye familia hizo ndimo tunapata wakaazi wa miji yetu. Inafaa tuanze kujichunguza tangu kwenye familia zetu na vipa umbele tunavyopanga. Asante Jennifer kwa mchango wako na changamoto uliyotupa.

   Like

   simbadeo

   March 30, 2012 at 10:09 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: