simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Geography: Land formations … erosion

with 2 comments

Ni katika bonde la Mto Msimbazi, Dar es Salaam. Section of the Msimbazi River Valley in Dar es Salaam. Unaweza kuona kazi ya maji katika kusababisha mmomonyoko. Hata hivyo, tunashuhudia pia athari za mabadiliko ya tabia ya nchi. Miaka 15 kurudi nyuma, bonde hili, na hasa njia ya mto daima ilikuwa na maji. Kina cha maji hayo kiliongezeka nyakati za masika na vuli. Lakini sasa hivi kama unavyoona, katika njia ya mto yenyewe hakuna hata tone la maji. Lakini papo hapo, miezi miwili iliyopita, mto huu ulifurika kiasi cha kusababisha mafuriko yaliyoharibu nyumba za watu pamoja na kuua. Ama kwa hakika tuna wajibu kuona nini kila mmoja wetu anafanya ili kurekebisha hali ya mambo. Hivi, hatuwezi kuimarisha kingo za mto huu ili usije kuhama njia? Tutembee. Tutembelee maeneo mbalimbali kadiri tunavyopata muda.

Advertisements

Written by simbadeo

March 14, 2012 at 12:26 am

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Huo ndiyo umissionari wenyewe! Kuona na kutenda kwa kuwafungua macho wengine. Changamoto ni moja Bwana Simba. Nchi yetu haijaweka vipaumbele katika mambo hayo ila katika wakubwa kugawana pato tulilonalo kwa njia yoyote ile. Wanajilimbikizia mali binafsi, wakijijengea wao na watoto wao maisha ya baadaye kama vile nchi itafungua macho siku moja na kujikuta wakijitegemea. Waliojaribu kufungua pazia walau kidogo tu, walijikuta wakiitwa majina kama hayati, marehemu, nk au pengine wale ambao Mungu aliwapendelea walijikuta India nk!

  Simba, natamani makala zako ziwe zinasomwa Ikulu au hata watu wa Usalama ili waweze kumshauri Rais na waandamizi wake. Keep it up Bwana Simba!

  Like

  Reginld Komino

  March 14, 2012 at 5:08 pm

  • Hi, Bw Komino

   Umenipa cheo kikubwa sana ndugu. Mie ni ‘Ndugu Mdogo’ tu … LOL! Thanks.

   Like

   Deo Simba

   March 14, 2012 at 5:32 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: