simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Kiguu na njia … Jijini Dar

leave a comment »

Panapostahili pongezi, basi tuzitoe. Kwa wiki za karibuni, nimeona kwamba baadhi ya vipande vya Barabara ya Nelson Mandela jijini Dar taa zake zinafanya kazi usiku unapoingia. Hongera kwa yeyote au taasisi yoyote inayoshughulika na hili. Hata hivyo, tunataka mitaa yote iwe na taa, ikibidi hata vichochoroni. Naamini hatua hii itasaidia sana kupunguza vitendo vya kihuni, uhalifu, na hata ajali za barabarani.

Kwa harakati zinazoendelea huko baharini na kwingineko nchini Tanzania … huenda matenki kama haya yatajazwa mafuta yanayochimbwa hapahapa nchini badala ya yale yanayotoka masafa marefu … mathalani kule Uarabuni.

Matangazo ya maonyesho ya soccer la Ulaya katika vitongoji mbalimbali vya jiji la Dar … biashara imeshamiri … Kumbe siyo kina Drogba na wengineo tu wanaonufaika na soccer hilo … bali hata baadhi yetu hapa mjini … Mjini Shule.

Kuna uwezekano mkubwa tu kwamba ule ulabu uliolamba jana … ulitengenezwa hapa … hapa ni TBL Dar es Salaam …

Siku hizi umeme umekuwa ukikatikakatika mara kwa mara … mara nyingine kwa saa nyingi tu … JEEEE mgawo umeanza? Tuambizane jamani ili tutafute vibatari na vijenereta …

Na huu ulikuwa uvumbuzi. Makao makuu ya Democratic Party. Naamini safari ya kuisaka Ikulu bado inaendelea. Lakini, kwa ushauri, ni muhimu wenye chama hiki watafute wanachama zaidi ili kukipa nguvu na mwelekeo mpya. Vyama vyetu vya siasa nchini Tanzania kwa sasa vimepoteza uthabiti katika kuwatetea wanyonge. Kazeni buti. Mmechagua kuingia kwenye siasa, basi mfanye hiyo siasa, iwe siasa ya kujenga, si kubomoa au kuhomola.

Kwa leo hizi zatosha. Tukutane siku nyingine tena. Wiki nzima njema.

Advertisements

Written by simbadeo

February 19, 2012 at 11:40 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: