simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Gongo la Mboto bomb blasts … Kumbukumbu

leave a comment »

Ilikuwa usiku kama wa leo, kutoka tarehe 16 Februari kuelekea 17 Februari 2011. Muda kama huu ninapoandika, around saa 5 usiku, ilikuwa hekaheka jiji zima la Dar es Salaam kama si nchi nzima. Leo hii ni mwaka mmoja umepita. Tukio lile limeacha makovu ya kudumu katika maisha ya watu wengi. Hii si kwa waliopoteza ndugu na mali zao tu, bali kwa jamii nzima. Kila mmoja ana namna anavyoikumbuka siku ile. Kila mmoja ana namna ilivyomgusa.

Je, wewe ulikuwa wapi mabomu yalipokuwa yakifumuka kule Gongo la Mboto? Ulipataje habari? Uliguswa vipi? Unaweza kutushirikisha jinsi ulivyoguswa.

Kwa upande wangu. Siku hiyo ilikuwa Sikukuu ya Maulid ya Mtume Muhammad (S.A.W.). Familia yangu na mimi tulikuwa tumealikwa kwenye sikukuu hiyo na familia rafiki yetu. Wao wanaishi kule Kimara Baruti. Ilipotimu majira ya saa 1.30 usiku, tulianza safari ya kurudi nyumbani. Uelekeo wa Gongo la Mboto. Tunaishi ndani ya radius ya kilomita 10 kutoka kilipokuwa kitovu cha milipuko.

Tulipofika maeneo ya Tabata reli, rafiki yangu mmoja aliyekuwa Arusha alinipigia simu. Familia yake inaishi Moshi Bar, eneo la Mombasa. Aliniuliza kama nilikuwa nimesikia juu ya mabomu yanayolipuka kule Gongo la Mboto. Nilimwambia hapana. Muda mfupi, tulifungulia redio kwenye gari. Clouds FM walikuwa hewani. Ndipo walipoanza kutupa yaliyokuwa yakijiri. Tulipofika Tazara. Tulishindwa kuchukua uelekeo wa Gongo la Mboto. Maana hakuna magari yaliyokuwa yakiruhusiwa kwenda kule. Njia zote nne zilitumika kuelekeza magari yanayotoka Gongo la Mboto kuja katikati ya mji.

Nasi tukawa hatuna budi ila kuelekea mjini. Hekaheka zilikuwa zimekwisha pamba moto. Ilinipasa kuirudisha familia Kimara kwa familia rafiki zetu ili kupata hifadhi.

Hata hivyo, baadhi ya wanafamilia wangu walikuwa wamebaki nyumbani. Mawasiliano ya simu yalikuwa hola. Simu ya mezani iliita tu pasipo kupokelewa. Waliobaki nyumbani walikuwa watatu. Majira ya saa sita za usiku, nilianza safari ya kuelekea nyumbani, peke yangu ili kutafuta wanafamilia wangu wengine. Kwenye saa sita na nusu usiku nilifaulu kupata mawasiliano ya wawili kati ya watatu. Hawa walikuwa wamekimbia nyumbani na kutembea kwa miguu hadi Tabata Shule. Nilifanya utaratibu wa kuwafuata pale na kuwapeleka Kimara.

Kasheshe lilikuwa kwa yule mmoja. Kwa njia ya bodaboda nilifaulu kufika hadi nyumbani kwangu. Milango na kila kitu kilikuwa wazi. Lakini nyumbani palikuwa salama salimini. Njiani nilikutana na makundi ya mamia kwa maelfu ya watu. Watoto. Wazee. Akina mama. Vijana. Wanaume. Yaani wote. Walikuwepo waliojibanza kwenye vibaraza vya nyumba. Walikuwepo waliokuwa wamelala barabarani. Walikuwepo waliokuwa peku. Waliokuwa na kanga moja. Ili mradi kila mmoja alijaribu kuiokoa nafsi yake kwa namna alivyoweza. Ulikuwa usiku wa patashika nguo kuchanika.

Kwa kuwa nilikuwa nimepotelewa na mwanafamilia yangu mmoja. Nilichukua pikipiki nyumbani na kuanza kuzunguka huku na kule nikimtafuta. Nilipita katika makundi mengi na katika maeneo mengi. Hadi saa 11 alfajiri nilikuwa sijafaulu. Nilirejea nyumbani.

Baada ya kuona hali imetulia. Niliwasiliana na waliokuwa Kimara ili warudi nyumbani. Wakati nikijipanga kuendelea kumtafuta mwanafamilia aliyepotea, majira ya saa nne asubuhi, mara tulimwona amerudi. Kumbe katika kimbiakimbia, alijikuta ameishia Kituo cha Polisi Sitakishari. Pale ndipo alipopata hifadhi yeye pamoja na mamia ya watu wengine. Katika tafuta yangu wala sikupata wazo la kwenda kituoni pale kumtafuta.

Baadaye, niliitumia siku hiyo kwenda kwenye maeneo yaliyoathirika ili kujionea nini hasa kiliendelea.

Hivyo ndivyo ninavyokumbuka milipuko ya mabomu ya Gongo la Mboto. Leo ni mwaka mmoja tangu jambo hilo litokee. Tuwaombee wale waliopoteza maisha yao. Tuombe Mungu kwamba atuepushe na mabalaa kama yale katika nchi yetu. Tuihimize Serikali yetu tukufu kufanya juhudi kuzuia majanga kama yale. Tuiombe Serikali yetu kufanya jitihada zaidi ili wale waliopoteza maisha yao waweze kufidiwa kwa namna za kuwasahaulisha machungu ya masaibu ya siku hiyo.

Nawasilisha. Je, wewe una cha kutuambia kuhusu tukio hilo. Karibu.

Advertisements

Written by simbadeo

February 16, 2012 at 11:44 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: