simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Trafiki … mpooo?

leave a comment »

Nilipata mshtuko baada ya kuingia kwenye daladala (basi linalotoa huduma ya usafiri kwa umma) – Kinyerezi kwenda/kurudi Majumbasita – nilipokuta ‘tanki’ la mafuta yanayotumiwa na basi hilo likiwa ndani ya basi. Kidogo nishuke, ila baada ya kuona kwamba ni dizeli na si petroli basi ndiyo nikavumilia mwendo mfupi niliokuwa naenda.

Lakini, kwa ujumla hii sasa ni kuvuka mipaka. Pamoja na uchakavu wa gari, lakini kuweka mafuta ndani ya basi ni kukiuka kanuni za msingi za afya. Nilipomwuliza dereva, vipi kulikoni, alinijibu tu, ‘hii mbona kawaida tu!’ Aliongea kusema kuwa basi lake halipo peke yake hapa mjini. Yapo mengi yaliyo barabarani kwa njia hiyo.

Nikajikuta nawaza kwa sauti: Polisi trafiki mpooooo? Ukaguzi wenu vipi, unapofushwa na ‘mlungula’ nini? Kwa nini tuwe na hali kama hizi? Kisha janga likitokea, tunasemaje: ‘Mapenzi ya Mungu? Kazi ya Mungu? Bahati Mbaya?’ Tuache vurugu hizi!

Advertisements

Written by simbadeo

January 31, 2012 at 8:09 am

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: