simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Mombasa … Dar es Salaam

with 2 comments

Si Mombasa ya Kenya, ni kile kitongoji katika jiji la Dar es Salaam katika kata ya Ukonga. Kuna harakati zinaendelea hapa. Je, zitasaidia kupunguza kero ya vurugu za Daladala ambazo kawaida hutawala eneo hili? Kitu kama hiki tayari kimefanyika katika maeneo ya Banana na Gongolamboto. Je, hatua hizi zimesaidia kupunguza vurugu? Kwa asilimia ngapi? Je, madereva wanazingatia kutumia suhula hizi? Kama wanakwepa kuzitumia na badala yake wanaendelea kupakia na kupakua abiria barabarani … nini kimekwenda kombo? Je, kuna jambo bora zaidi ambalo lingeweza kufanywa badala ya hatua hii … ambayo wengine wanaona kama ni ya ‘zima moto’? Tuendelee kuwepo.

Advertisements

Written by simbadeo

January 29, 2012 at 11:06 pm

Posted in Siasa na jamii

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Kaka umenena na wenye macho wataona na wenye mamlaka watatenda kwa ujasiri.Serikali inastahili pongezi zake kwa kile kinachoendelea kufanyika hapa Ukonga Mombasa na katika miundo mbinu yote ya barabara mkoani Dar es salaam.Watumiaji wote wa miundo mbinu ya barabara wanapaswa kuonyesha kuwa wanajali.Kaka sogea pale kwenye daraja baada ya shule ya Sekondari Kitunda kuelekea Nyangasa-Mwanagati na Kibeberu uone jinsi hali ilivyo tete na kilima hiki sasa huenda kikaitwa kilima cha moto kwa majanga yanasubiriwa hapa.Huku ndiyo kwa mbunge wa ukonga ambaye nasikia anamiliki shule ya akademia na diwani ndiyo mkandarasi wa barabara hii ambayo hakuna matarajio ya kukamilisha ujenzi wake.Ama kweli hiki ni kilio cha samaki katikati ya bahari na machozi yake yanafunikwa na maji.

  Like

  ray njau

  January 30, 2012 at 10:31 am

 2. Hi Ray. Changamoto ni nyingi. Lakini kama wananchi, tunayo haki na wajibu wa kufuatilia. Maana barabara na madaraja yanajengwa kwa fedha zetu, kodi. vinginevyo, huwa zinatolewa kwa ajili yetu. Kumbe basi kila mmoja wetu atimize wajibu wake vizuri. Nitatafuta wasaa wa kutembele daraja la Nyangasa-Mwanagati. Asante.

  Like

  Deo Simba

  January 30, 2012 at 7:33 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: