simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Biashara ndogo … maisha yanakwenda

with 3 comments

Biashara ya kuchongesha mihuri imeshamiri jijini Dar es Salaam. Wakati ambapo huenda ni biashara inayozua maswali mengi kuhusu nia za watu wanaotaka kuchongewa mihuri (jambo ambalo ni la makala nyingine), hakuna ubishi kwamba kuna kundi kubwa la vijana na wengine sasa ni watu wazima wanajipatia riziki kutokana na biashara hii. Muhuri mmoja unagharimu kati ya shilingi 4,000 hadi elfu 7,000. Inategemea uko maeneo gani ya jiji, haraka uliyo nayo, idadi ya maneno na ubora wa vifaa pamoja na kazi itakayofanyika. Ama kwa hakika, hii ni sanaa ya aina yake. Pengine ipo haja ya kuanzisha darasa maalumu kwenye vyuo vya ufundi stadi ili vijana wengi zaidi wapate kujifunza na kutumia maarifa hayo kujipatia riziki.

Mwuza karanga (kushoto) na mteja wake. Hii ni biashara nyingine ndogo inayoendesha maisha ya watu wengi hapa jijini. Dada huyu, jina kapuni, ana mwaka mmoja sasa tangu aianze. Ana mtoto mmoja. Anaishi kwenye nyumba ya kupanga. Alianza biashara hiyo kwa mtaji wa Shilingi 23,000. Hivi sasa biashara yake imefika mahali ananunua kilo kumi (10) ambazo yeye huziuza kwa siku mbili. Alianza biashara hiyo baada ya kuachika kwa mumewe. Kwa vile hakuwa na jinsi nyingine ya kujikimu yeye na mtoto wake, basi alianza biashara hii. Alijifunza kutoka kwa mama yake ambaye ameifanya kwa muda mrefu.

Kuna biashara ndogondogo za kila aina katika jiji la Dar es Salaam. Hii inatokana na ukweli kwamba idadi ya watu jijini inakua kwa kasi kubwa kuliko uwezo wake wa kutoa ajira rasmi kwa wingi. Kwa kuwa lazima maisha yaendelee basi watu hujishughulisha kwa namna mbalimbali. Na pengine hali hii ndiyo inayokuwa kivutio kwa vijana kutoka mikoani kumiminika Dar es Salaam. Ni wakati sasa Serikali ifikirie kwa makini nini cha kufanya, ikiwa ni pamoja na kufanya mazingira ya kufanya biashara ndogo yawe bora zaidi, kwa maana ya kuwa na vibanda vingi, vilivyo na standard moja, ili kulinda mazingira na kuwafanya wafanyabiashara wawe na anwani. Zaidi sana, Serikali itaweza nayo kujipatia kodi kwa kiasi kikubwa sana. Pengine kwa ongezeko la kodi kutoka sekta isiyo rasmi, kutaifanya nchi iachane na utegemezi wa wahisani.

Ni hayo tu kwa leo. Tukutane wakati mwingine.

Advertisements

Written by simbadeo

January 21, 2012 at 11:51 pm

Posted in Siasa na jamii

3 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Safi sana Simba! Nimesoma makala yako kwa furaha sana! Imekuwa hivi kwani tayari ninaona kuwa maisha hayaendi kwa mshahara huu mdogo ambao siweziupata mahali pengine. Ninatamani kubuni biashara ndogo ambayo nawezatumia laki moja au mbili kuanzisha! Pengine unishauri, ingawa mifano uliyonipa imenitia shime sana! Keep it up, wakati mwingine najiuliza unapata wapi muda kwa ajili ya kazi hii? Pengine nikuulize, inalipa? Vipi bonus unapata kwenye blog yako?

  Tuzidi kuishauri jamii
  Ni hili kwa leo

  Like

  Reginld Komino

  January 23, 2012 at 10:48 am

 2. “Tuzidi kuishauri jamii.” Nakubaliana nawe Reginald. Muda … muda ni mfupi sana hapa duniani. Inatupasa kutumia vema kila sekunde, kila dakika tunayopata. Unapokuwa njiani … unakwenda kazini, au uko njia moja kwenda kwenye miadi, au hata unapotembea ili kuwazua hili na lile, muda huo ndiyo pia yakupasa kufanya mambo mengine mengi. Simama. Zungumza na watu. Dadisi. Hoji. Uliza. Ndivyo ninavyofanya.

  Bonus? Bonus yangu ni pale wasomaji mnaponifahamisha … au kwa kunikosoa ama kunipongeza kupitia maoni yenu. Hiyo ndiyo bonus. Ninaithamini zaidi sana bonus hiyo kuliko bonus katika muundo wa ‘fedha’. Nami ni furaha yangu kuwaletea haya ninayowaletea kwa njia hii. Hiyo ni bila kujali mimi ninaingia gharama kubwa kiasi gani katika kuwakusanyia na kuwatumia makala haya na picha.

  Tupo pamoja, tuendlee …

  Like

  Deogratias Simba

  January 23, 2012 at 11:52 pm

 3. Ni imani yangu kuwa mwimbaji bora wa nyimbo za injili ni yule kwanza awe ameokoka kweli na mwenye lengo kweli la kuwafikia watu wa Mungu au wa mataifa katika kuwapa neno la Mungu na kuwaasa waache anasa na si kwa lengo lingine lolote hapo liwe la kufanya biashara au kujulikana kwa watu. Mwimbaji wa muziki wa injili Kabula John George ni mtumishi wa Mungu anayefanya kazi hiyo kupitia kipawa chake alichopewa na Mungu. Tayari amefafanikiwa kutoa albam ya nyimbo za injili inayojulikana kwa Ushindi. Watu wengi wamezipenda nyimbo zake kutokana na ujumbe mzuri uliomo na radio mbali mbali za kidini zinacheza nyimbo hizo. Radio ambazo kwa sasa zinapinga nyimbo za dada Kabula ni Wapo Radio, Prise Power zote za Dar es Salaam, Radio Safina ya Arusha na Radio Sauti ya Injili Moshi.

  Like

  Sugel

  January 25, 2012 at 1:47 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: