simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Mafuriko Dar … hatari nyemelezi na mengineyo

leave a comment »

Waheshimiwa wa Tanesco, tafadhali muiwahi nguzo hiyo katika Barabara ya Mongo la Ndege karibu na daraja la Kinyerezi … madhara yake huenda yasisemeke …

Baada ya kina cha maji kupungua … unaweza kuona jinsi daraja la Kinyerezi lilivyo hatarini. Nguzo hiyo kushoto inamong’onyolewa …

Wakubwa wa TTCL … muiwahi nguzo yenu na nyaya zenu kabla haijaondoka kabisa …

Barabara ya Kinyerezi katika eneo la Bonde la Mto Msimbazi …

Moja ya madaraja katika Bonde la Mto Msimbazi kwenye barabara ya Kinyerezi …

Ziba ufa … la sivyo … utajenga ukuta. Huo ndiyo msemo wa wahenga wetu. Una hekima kubwa nyuma yake. Barabara hii haina miaka mitatu tangu ‘ikamilike’ …

Baada ya magari kuzuiwa kupita juu ya Daraja la Kinyerezi, hivi sasa tunavuka kwa miguu … kama linavyoonekana … daraja ni jembamba. Kumbukumbu zinasema kwamba lilikuwa daraja la muda kufuatia kusombwa kwa lingine lililokuwepo enzi za Mvua za El-Nino 1997/98. Limeendelea kubaki ‘daraja la muda’ kwa miaka 14 hivi!

Naam, ndiyo hali ya Daraja la Kinyerezi ilivyo kwa sasa!

Mipango madhubuti kudhibiti matukio haya hata kabla hayajatokea ni mambo yanayowezekana …

Advertisements

Written by simbadeo

December 23, 2011 at 12:10 am

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: