simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Usafiri … kasi ya maisha

with 2 comments

Usafiri wa pikipiki umekuwa maarufu sana hapa nchini na hasa katika miji mikubwa. Naamini tulio wengi tumeutumia usafiri huu wakati mmoja au mwingine. Kila mmoja ana sababu zake kwa nini aliutumia. Kwa miaka mingi tumekuwa na hofu kwamba ukipanda pikipiki basi ndiyo mwisho wako, maana ajali ni nje nje. Swali kubwa ni kwamba, pamoja na wingi wa ajali zinazotokana na matumizi ya usafiri huu, kwa nini bado tunaendelea kuutumia? Nimetafakari. Hivi ndivyo ninavyofikiri. Maisha ya sasa yanaenda kwa kasi kubwa. Kwa sababu ya kasi hiyo, kumekuwa na mahitaji ya kwenda haraka kutoka eneo moja hadi jingine. Usafiri wa gari ni wa kasi. Lakini kasi hiyo hukwazwa na tatizo la msongamano barabarani. Msongamano unaosababishwa na wingi wa magari na ufinyu wa miundo mbinu ya barabara. Pikipiki huwa hazikwazwi na tatizo la usafiri. Ndiyo sababu mtu anayeondoka Temeke mwisho kwa gari kwenda Mwenge, akilinganishwa na yule anayetumia pikipiki, yule wa pikipiki atafika mapema kuliko yule wa gari.

Usipoendana na kasi ya maisha ya sasa, maisha yako yatasimama. Hili nafikiri ndiyo linalotufanya tuzidi kutumia usafiri wa pikipiki pamoja na ukweli kwamba una hatari nyingi. Kikubwa nafikiri ni kwa vyombo vinavyosimamia usafiri kusimamia utoaji mafunzo juu ya maadili ya uendeshaji vyombo vya moto. Mafunzo haya yakikazaniwa sana, yatasaidia kupunguza ajali zinazotokana na matumizi ya pikipiki.

Nawakilisha.

Advertisements

Written by simbadeo

December 11, 2011 at 7:15 am

Posted in Siasa na jamii

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Hakika Kaka S! maisha haya sijui kama kweli tunasonga mbele au tunarudi nyuma…Kama nilivyosema siku moja hapa ni kwamba watu wengi wanaendesha kama vile mashindano hawajali na wengine hawajapata mafunzo kabisa.
  Ningekuwa nipo ndani ya bunge au tu ndani ya chombo chochote sheye sauti ningefanya utaratibu kwamba daladala zote zitolewe na yawe mabasi makubwa ya kutosha. Mimi nafikiri nchi yetu ingesonga mbele zaidi kuliko sasa magari mengi usafiri haba..Nawza tu kwa sauti.

  Like

  Yasinta

  December 11, 2011 at 10:07 am

 2. Kuwaza muhimu Da Yasinta. Mabadiliko … kila mmoja anaweza kujaribu kuleta tofauti … hata kama ni kwa njia ndogo. Naona wale tunaowatuma Bungeni wao wanachokiwaza saaana ni posho nene nene! Kazi kwelikweli. Aliye juu … mpandie hukohuko. Nasi tunakuja huko mjengoni 2015!

  Like

  Deo Simba

  December 11, 2011 at 2:30 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: