simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Sheria … Pesa …. Tafakari

with 6 comments

Msemo mzito. Unaakisi hali halisi katika jamii yetu na nyinginezo nyingi duniani. Unanikumbusha msemo ule mwingine ‘sheria duniani, haki mbinguni’. Tunaona jinsi fedha inavyozidi kutukuzwa … si makanisani … si misikitini … si katika uhusiano kati ya ndugu, jamaa, marafiki na hata wafanyakazi wenza. Ukiwa na fedha, mambo mengi yatakunyookea, utamudu pia kupindisha sheria kadiri unavyotaka. Ama kweli ‘pesa sabani ya roho’. Tafakari.

Advertisements

Written by simbadeo

December 1, 2011 at 9:02 am

Posted in Siasa na jamii

6 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. 9 Hata hivyo, wale ambao wameazimia kuwa matajiri huanguka katika jaribu na mtego na tamaa nyingi za kijinga na zenye kudhuru, ambazo hutumbukiza watu katika maangamizi na uharibifu. 10 Kwa maana kupenda pesa ni chanzo cha mambo mabaya ya namna zote, na kwa kujitahidi kufikia upendo huo wengine wamepotoshwa kutoka kwenye imani nao wamejichoma wenyewe kila mahali kwa maumivu mengi. _Timotheo 6:9,10.

  Like

  Ray E.Njau

  December 1, 2011 at 1:05 pm

 2. Ray, asante kwa Neno.

  Like

  Deo Simba

  December 1, 2011 at 1:24 pm

 3. duh! kazi kwelikweli hata la kusema zaidi nimeishiwa maana nimewahi kusikia kuwa eti pesa zilimwuua hata Yesu..je ni kweli?

  Like

  Yasinta

  December 1, 2011 at 2:04 pm

 4. ndio ni swali ambalo nimeuliza kwa sauti…

  Like

  Yasinta

  December 1, 2011 at 6:18 pm

 5. Mmh, kuhusu ‘pesa kumwua Yesu’. Kadiri ya maandiko, moja ya kichocheo kilimchomfanya Yusa Iskarioti, mmoja wa wanafunzi wa Yesu, kumsaliti Bwana wake ilikuwa pesa. Alipokea vipande kadhaa vya pesa (thelathini) ili awaelekeze wale waliokuwa wakimsaka Yesu mahali ambapo angekuwepo. Kwa hiyo, Yuda alijipatia pesa hizo na kisha kuwaambia wale Wakuu wa Makuhani na wengineo wapi wangempata Yesu. Na kweli, Yesu alikamatwa na kisha kufikishwa mbele ya Pilato na taratibu nyingine kama tunavyozifahamu. Kwa hiyo, kutokana na kichocheo cha pesa, usaliti uliingia … kwa maana nyingine tamaa na uchoyo … na matokeo yake ndiyo kama tunavyofahamu.

  Hapa namwalika Mtaalamu Ray atupatie mtazamo wa kiimani kuhusu kitendo hicho.

  Mtakumbuka pia kwamba katika Agano la Kale, kuna kijana Yusuf, mtoto wa Jacob aliyeuzwa na ndugu zake kwa vipande thelathini vya fedha. Baadaye lakini kwa kutumia njia hiyo, pasipo vijana wa Yakobo kujua, nchi yao ilikuja kuondokana na janga la njaa. Na mengine mengi yalifuatia.

  Naona fedha haitajwi kwa wema sana katika Maandiko Matakatifu. Tuendelee kuwepo.

  Ciao.

  Like

  Deo Simba

  December 1, 2011 at 7:35 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: