simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Sam Nujoma Road … waanza kutia huruma

leave a comment »

Hivi majuzi nilipita Barabara ya Sam Nujoma inayounganisha Ubungo na Mwenge. Nilipatwa na mshtuko. Eneo la katikati ya barabara lililokusudiwa kupandwa maua halipati matunzo. Kuna maua humo yalipandwa lakini hivi sasa mengine yameanza kujifia. Mfano ni hiyo miti ya maua yenye umbo la mnazi (sijui kitaalamu inaitwaje) … kuna mingi tu iliyojifia. Hivi, hawa watu wanaohusika na utunzaji wa bustani hiyo ya barabarani wanajisikia vipi kwamba bustani inadorora mikononi mwao? Je, wanaendelea ‘kukinga mkono’ kila mwisho wa mwezi? Hapana budi hatua za haraka zichukuliwe kuokoa hali ya mambo. Ni vema tuwe na mazingira yanayong’aa na kupendeza macho. Hivi miaka 50 baada ya uhuru tunataka Wazungu ndiyo waje watugawie fedha za kutunza mazingira yetu? Kweli hii inaingia akilini? Acheni utani bwana, fanyeni kazi!

Advertisements

Written by simbadeo

December 1, 2011 at 8:45 am

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: