simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Kwa David Cameron … hii ni Afrika

with 2 comments

Ni ‘taboo’. Nimeona ni vema nimfikishie ujumbe huu niliokutana nao jijini Nairoibi siku za karibuni Mheshimiwa David Cameron. Ni vema aheshimu taboo zetu katika Afrika. Ni jambo lenye mjadala na ulimwengu wa Magharibi wamelivalia njuga, lakini ni sababu zipi hasa zitakazoufanya umma wetu huku ukubali mwenendo huo uliosababisha Sodoma na Gomora kuangamizwa? Wengine wanasema eti ni ‘orientation’! Kweli hii ni ‘sexual orientation’ au ni kujiendekeza tu? Nadhani sote tumewahi kusikia watu wanaojisingizia tabia ya wizi … kwamba huwajia si kwa kupenda kwao bali ndivyo walivyozaliwa … Aaah wapi bwana … wizi ni wizi tu na ukikamatwa unaiba pale Kariakoo au kwingineko ujue wewe ni wa kutiwa kibiriti tu. Hivi walimwengu, mbona tunajihalalishia mambo ya ajabu namna hii?? Ama kweli dunia yetu imefika ukingoni.

Advertisements

Written by simbadeo

November 30, 2011 at 3:46 pm

Posted in Siasa na jamii

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Asante Bwana Simba, natamani hata kuwe na TV maalumu kwa ajili ya kuzungumzia mambo ya maadili na kila siku kuwe na saa maalumu kwa ajili ya kupinga upuuzi kama huu. Si tu ujinga wa kujisingizia kuwa hawa washenzi wamezaliwa hivyo, ila majitu mengine hufanya ujinga hata wa kuua na kujisingizia saikolojia ya ‘tumezaliwa hivyo’ na mwisho kosa lao linakuwa ‘kuua bila kukusudia’. Huu ni ufirauni mkubwa ambao dunia ya kishetani inatuletea. Ulimwengu wa imani kwa shetani unataka kuingilia ulimwengu wa kimungu. Ni ujinga wa hali ya juu kuona wasomi wanasimama jukwaani kujadiliana uhalali wa ndoa ya jinsia moja. Ni upuuzi mkubwa kwani hata wanyama wasio na utashi wanajua hilo. Kuku, mbuzi, ng’ombe, nk hufanya hivyo kwa ajili ya uzao/ kupata watoto ‘reproductive act’ – pro-creation’, inakuwaji ‘binadamu’ ambaye ndiye sura na mfano wa Mungu kuwa mpuuzi kuliko wanyama wasio na akili? Hakika hatuhitaji kufikiri sana kuhusu jambo hili, huu ni ushetani kwa 100%.

  Juzi nilikuwa pale mitaa ya karume karibu na mitumba, kulikuwa na kikundi kinachezesha bahati nasibu. Jamaa mmoja aliingia kucheza kwani aliona watu wanapata pesa bila kazi zaidi. Nilipofuatilia niliambiwa ni kikundi halali kilichosajiliwa na watu wanacheza kwa hiari yao wenyewe. Karibu nicheze, niliona watu wanalipia kuponi zenye namba, namba ile ilichagua bidhaa fulani katika bidhaa zilizopo, kisha mhusika alitangazwa kuwa ameshinda bidhaa ile ( tv, jenereta, redio, begi nk). Ila hakuna aliyeruhusiwa kuichukuwa bidhaa ingawa kiasi cha fedha kilizidi thamani ya bidhaa ile. Hii ilimlazimu mhusika achukue fedha na bidhaa ibaki. Mhusika alipewa masharti ya kutoa kiasi fulani cha fedha na baadaye alipewa fedha aliyoshinda. Kwa uchunguzi niliona kuwa kiasi mtu alichotoa kinakaribiana na kiasi alichoshinda na kama kiasi kile ni kikubwa basi kamwe mtu huyu hakupata pesa alizoshinda. Wahusika waliendelea kumuuliza maswali hadi apate swali aliloshindwa na hivyo fedha zake zilichukuliwa. Wengi walitoka pale wanalia kwa kishindo kwani masharti waliopewa mwanzoni yalibadilika na hivi kupoteza pesa zao.

  Mtu mmoja alifika pale, alionekana kama ana pesa. Mara alipoona watu wanashinda alifikiri kama mimi kuwa hiki ni kikundi halali; kumbe wale wanaoshinda ni wenzao na baadaye watarudisha pesa hizo. Alichukua kuponi kwa ofa, baada ya kushinda pesa nyingi aliambiwa kumbe hakulipia ile kuponi kwa hiyo ni batili, ila kwa kuwa alikuwa tayari kucheza alipewa ofa ya kuponi nne, ndani ya hizo ilikuwepo ile ile aliyopata mwanzoni. Nifuatilie vizuri upate uozo wa jamii yetu!

  Masharti ya kupata zawadi aliyoshinda: Nakumbuka namba aliyopata ilikuwa #800 ambayo ilikuwa juu ya redio ambayo kama ni nzima ingekuwa kati ya 100,000 na 200,000. Hakuruhusiwa kuichukua redio ila aliambiwa ameshinda Tshs 970,000/=, sasa fuatilia masharti:

  Aliambiwa kutoa sh 29,000/= mara tano, akatoa 30,000 mara tano kwani alikuwa na nyekundu tupu, then akaambiwa kutoa sh 15,000/= akatoa 20,000 kwani chenchi angepewa baadaye, then akaambiwa kutoa sh 250,000/= gharama ya kuponi ile, akakosa; bado alikuwa na hamu ya 970,000/= alizoshinda. Aliondoka haraka kwenda benki ya karibu na alitoa pesa ile 250,000/=. Kisha aliambiwa kulipa 100,000/= gharama ya mhasibu katika kutoa pesa zake hizo. Alilalamika sasa kuwa kwanini hawakumwambia kabla ili aje nazo zote toka benki; alilalamika kuwa bado ana 50,000/= tu hivyo hata hivyo angekuwa tayari kuitoa ili inayobaki ipunguzwe katika hilo donge nono. Walikubali, ila wakamwambia bado kukomboa zile kuponi nyingine tatu zilizobaki ili apate pesa nyingine pia. Hapo alichanganyikiwa kidogo kwani likuwa tayari ametumia takriban 500,000/= na bado masharti yaliendelea.Walimjaribu kama angekuwa tayari kupunguza kuponi zile ili abaki na moja ambayo itamhalalisha kupata hiyo 970,000/= alipokubali alipunguza, kumbe walikuwa na copi ya ile aliyoshinda, wakamwambia iliyobaki hapo ni ya thamani ya 1,000/= wakampa. Hapa alipata mwanga kuwa kashaibiwa au kutapeliwa mbele ya umati wa watu. Aliwakwa na hasira akataka arudishiwe pesa zake, akaambiwa hii ni bahati na sibu na hazirudi. Pale pale alikwenda kituo cha polisi cha karibu, polisi walikubali wakika pale na kusema hiki ni kikundi halali na kinalipa kodi; jamaa alijitetea akieleza yote waliyofanya na jinsi walivyobadilikabadilika ili kumwibia pesa zake; hata hivyo polisi walisema hali hii imeshazoeleka, hawana la kufanya.

  Simba nimeingiza hapa topic mpya ingawa wewe ulileta ya cameroon. Nataka kusema kuwa hiki kizazi cha nyoka, kinajua ukweli ila hakitaki kuutekeleza. Kila binadamu anajua sodomization ni ushetani lakini wanaongezeka na kuutetea. Kila mtu aliona watu walivyodhulumiwa pesa zao lakini hawakujitoa mhanga kuwasaidia; mbaya zaidi polisi ambayo ni chombo cha usalama wa raia hawakusaidia, ikimaanisha kuwa walishapokea hongo katika vikundi hivi ambavyo vinatengeneza fedha nyingi kwa kuwatapeli watu.

  Kwa kuokoa muda wako kidogo, niseme tu kuwa tusikate tamaa kuukemea uovu na Mungu atatubariki. Utatumia gharama nyingi kuutetea ukweli lakini jamii haina nafasi ya kuutii. Tujaribu kutafuta nafasi kwenye tv fulani ili kama watatudhamini, tuweze kutoa mambo mwengine ‘live’, mimi nilimaliza ‘theology’, sijui wewe mwenzangu. Tayari ninaona una mengi ya kuisaidia jamii; usikate tamaa. Tupo pamoja!

  Like

  Reginald Komino

  December 1, 2011 at 8:34 am

 2. 24 Kwa hiyo, kwa kupatana na tamaa za mioyo yao, Mungu aliwaacha katika uchafu, ili miili yao ivunjiwe heshima kati yao, 25 yaani, wale walioibadili kweli ya Mungu kwa ajili ya uwongo nao wakauheshimu mno uumbaji na kuutolea utumishi mtakatifu badala ya kumtolea Yeye aliyeumba, anayebarikiwa milele. Amina. 26 Ndiyo sababu Mungu aliwaacha katika hamu za ngono yenye kufedhehesha, kwa maana wanawake wao walibadili matumizi yao wenyewe ya asili kuwa yale yaliyo kinyume cha asili; 27 na vivyo hivyo pia hata wanaume waliacha matumizi ya asili ya mwanamke na kuwakiana tamaa kali katika uchu wao kuelekeana wao wenyewe, wanaume kwa wanaume, wakitenda mambo machafu na kupokea ndani yao wenyewe malipo kamili, yaliyostahili kosa lao._Waroma 1:24-27

  Like

  Ray E.Njau

  December 1, 2011 at 1:13 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: