simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Rukwa na Katavi … maonyesho ya utamaduni yaja

with 2 comments

Tangazo lililowekwa pale TAZARA Dar es Salaam. Maonyesho hayo ya utamaduni yanaanza kesho tarehe 25 Novemba hadi 27 Novemba. Kiingilio ni bure kama tangazo linavyosema. Ni jambo jema kujaribu kuelewa na kuvumbua utamaduni wetu. Utamaduni wa jirani yako unaweza kukueleza mengi kuhusu utamaduni wako mwenyewe. Hapa chini nawaletea picha mbalimbali kutoka kwenye mikoa hiyo miwili. Nilizipiga siku nyingi kidogo, kwa hiyo huenda mandhari yamebadilika kadiri siku zilivyopita. Karibuni:

Uwanja wa soka mjini Sumbawanga (Uwanja wa Mandela?)

Barabara inayounganisha Sumbawanga na Mpanda. Hivi sasa iko kwenye ujenzi. Lengo ni kuiwekea lami. Mradi utakamilika lini? Tusubiri na kuona.

Sumbawanga kwenda Mpanda … unapoingia Katavi

Kituo cha basi cha mjini Namanyere, Wilaya ya Nkasi

Lyazumbi – almaaruf kama ‘Kilimanjaro Hotel’ – hapo utapumzika unaposafiri kati ya Sumbawanga na Mpanda. Utapata makulaji ya kila aina.

Posta – Mpanda mjini

Double road – Mpanda

Moja ya maeneo ya mapumziko na kusubiri huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda

Tarafa ya Mwese, Mpanda

Watu wa Mpanda na uchumi wa kilimo cha mahindi …

Kilimo cha tumbaku … uchumi wa Mpanda

Utengenezaji pombe nao ni sehemu muhimu ya uchumi wa maeneo ya vijijini …

Kanisa Katoliki, Parokia ya Mwese, Mpanda, Katavi

Usafiri wa treni ni kiungo muhimu kati ya mji wa Mpanda na mikoa mingine ya Tanzania, hasa Tabora. Swali kubwa ni kwa nini hakuna juhudi za makusudi za kuimarisha na kuongeza ubora wa njia hii muhimu. Miundo mbinu tayari ipo. Kinachohitajika ni kuongeza ubora ili hata ikibidi kuwe na safari za kila siku za treni. Mji unakua kwa kasi sana. Usafiri wa uhakika ni jambo muhimu mno.

Kasi ya kupanuka kwa mji wa Mpanda … ni kubwa

Moja ya Stesheni muhimu katika reli inayounganisha Mpanda na Tabora

Shime Watanzania tujitokeze kwenda kuona asili ya Watanzania wenzetu: Wafipa, Wabende, Wakonongo, Wapimbwe na wengineo ambao pengine hujawahi kuwasikia. Ni pale Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama, Dar es Salaam kuanzia tarehe 25 Novemba hadi 27 Novemba, 2011.

Advertisements

Written by simbadeo

November 24, 2011 at 8:56 am

Posted in Siasa na jamii

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Inapendesza kwa kweli Ahsante kaka S—Picha hiyo ya “Hotel ya Kilimanjaro” nimeipenda kweli

  Like

  yasinta/kapulya

  November 24, 2011 at 1:00 pm

 2. Asante Da Yasinta. Nikipata fursa nami nitafika kwenye maonyesho ili kujifunza na kuwaletea picha zaidi kupitia jukwaa hili. Nyumbani ni nyumbani, au siyo?

  Like

  Deo Simba

  November 24, 2011 at 8:36 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: