simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Buguruni kwa Mnyamani … ndio penyewe

with 8 comments

Ndiyo. Ni sehemu iliyojaa watu. Kuna uhai mwingi unaendelea kutafuta, kutafutwa, kutafutiana, kutafutiwa etc.

Advertisements

Written by simbadeo

November 11, 2011 at 11:36 pm

Posted in Siasa na jamii

8 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Kwa wakazi wa manispaa ya Ilala Jijini Dar es salaam hapa ni kiunganishi cha wakazi wa Vingunguti Kiembe Mbuzi na barabara ya Mandela kuelekea Kariakoo-Posta hadi Kivukoni kupitia barabara Uhuru.
  Hapa ni maisha mchanganyiko kwa jamii ya kada zote na bei za bidhaa ni kushuka na kupanda na hukosi ukitakacho na kwa pesa yako.
  Hapa ndiyo Buguruni kwa Mwinyi Amani.

  Like

  Ray E.Njau

  November 12, 2011 at 10:37 am

  • Asante Njau kwa ufafanuzi muruwa. Shukrani sana.

   Like

   Deo Simba

   November 12, 2011 at 10:45 am

   • Asante na kamilisha wikiendi yako na majina ya kwetu.
    ——————————————————————————————————– Wazungu walipofika kwetu na kuona kilele cha kibo walisema ‘that is kibo alone’ na waliosikia wakatamka ‘KIBORILONI’.

    Wakaweka kibao kinachosomeka’ check train’ na wenyeji wakasoma ‘CHEKERENI’.

    Walipofika kwenye sherehe wakaona mbuzi ameokwa vizuri wakasema ‘this is wonderfull’ wenyeji wakasema ‘NDAFU’.

    Walipoona njia inayotoka mnadani kwenda kiwanda cha nyama wakasema ‘cow way’ waliosikia wakasema ‘KAWE”

    Walipouliza hapa ni wapi wakajibiwa ni ‘kwa Musa Hasan’ wakasema ‘MSASANI’

    Waliposikia wenyeji wakisema ‘mambo sasa’ wakasema ‘MAMBASA’ na wenzao waksema ‘MOMBASA’

    Haya ndiyo baadhi ya majina ya kwetu na walausishangae.
    Iwapo katika maktaba yako umehifadhi baadhi ya majina ya kwenu tafadhali yaweke hadharani ili wadau wacheke kabla ya kutabasamu.

    Hadi wakati ufaao siku zijazo,kwa sasa naelekea kwetu Kiboriloni.

    Like

    Ray E.Njau

    November 12, 2011 at 1:00 pm

 2. Nimezipenda hizo picha watu walivyo na rangi yaani hapo kweli ni kujichanganya tu…Ila mie hapa ningepotea…lol

  Like

  yasinta

  November 12, 2011 at 6:01 pm

  • Rangi poa kweli kweli … karibu.

   Like

   simbadeo

   November 13, 2011 at 5:00 pm

   • Buguruni kwa Mwinyi Amani kwa sasa mambo ni tambarare baada ya barabara kuwekwa na sasa mabasi ya Vingunguti Kiembe mbuzi yanaanzia Buguruni Sokoni kupitia Mnyamani hadi Kiembe Mbuzi.Upanuzi na uwekaji umeongeza umaarufu wa mtaa huu ambao zamani ulikuwa makazi duni lakini sasa kuna Kituo cha Afya ambacho hutumika sana wakati milipuko ya kipindupindu.Maghorofa yanaota kama uyoga na maduka ya bidhaa zenye thamani kubwa yamehamishiwa kwenye ukanda huu usiokauka watu kwa saa 24 kuanzia Jumatatu hadi Jumatatu na Januari hada Januari.Enzi hizo msimu wa mvua kama sasa ilikuwa ni shughuli pevu kukatiza Mnyamani hadi Vingunguti kwa raha zako.

    Like

    Ray E.Njau

    November 14, 2011 at 12:46 pm

 3. “BAADA YA BARABARA KUWEKWA LAMI”.

  Like

  Ray E.Njau

  November 14, 2011 at 12:47 pm

 4. Siku hizi panapendeza toka ijengwe hiyo barabara.

  Like

  Fadhy Mtanga

  November 18, 2011 at 3:46 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: