simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Treni … Bongo …

with 3 comments

Mandhari ya Railway Station Dar es Salaam …

Ndani … behewani … katika Daraja la Tatu …

Biashara? Ya nani? Au siku hizi Shirika la Reli wanagawa soda kwa wasafiri?

Warembo (wa Kinyamwezi? Kiha? Kisukuma? Kigogo? Kikaguru? Kinyaturu? Kibende? kireli ya kati?

Mandhari ya nje pale Railway …

Ni miaka mingi sijapanda treni. Mara yangu ya kwanza ilikuwa zaidi ya miaka thelathini iliyopita, kabla ya Vita vya Kagera. Treni lilikuwa safi zaidi na msongamano kidogo. Nilipokuwa nikisoma kule Moshi, miaka ya mwisho ya themanini na mwanzoni mwa miaka ya tisini … hali ilikuwa tofauti … Uchakavu, uchafu na msongamano. Hivi sasa, hali nafikiri ni mbovu zaidi. Mara ya mwisho niliposafiri na treni (2010) kwa Second Class (Sleeping) … hali ilikuwa mbaya zaidi. Najiuliza … tunapoadhimisha miaka 50 ya Uhuru … tunarudi nyuma au tunasonga mbele? Kwa nini hakuna mwendelezo mzuri wa yale yaliyoanzishwa zamani hizo? Taswira ya Shirika letu la Reli (baada ya kuwatimua Wahindi wale waliomilikishwa miaka ya hapa kati) inaakisi vema sana hali ya nchi yetu katika nyanja mbalimbali. Kwa ujumla kumekuwa na kuporomoka mno kwa viwango vya ubora. Je, sisi tumekuwa na mchango gani katika kuporomoka huku … hebu kila mmoja wetu ajichunguze ili TUJIREKEBISHE na kurekebisha hali ya mambo. Hebu fikiria, kama leo hii Ulaya wanalia na hali tata ya uchumi … sisi ni kina nani kuendelea kuchapa usingizi huku miguu ikiwa juu ya meza? Tuna mengi ya kufanya kuanzia ngazi ya juu kabisa hadi mie wa chini kabisa. Nawakilisha.

Advertisements

Written by simbadeo

November 4, 2011 at 7:12 pm

Posted in Siasa na jamii

3 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Mimi mara ya mwisho kusafiri na THIRD CLAASS katika treni hiyo ni mwaka 1995 natokea High School Mazengo DODOMA. Bado kidogo nipoteze mzigo wangu wakati nauona kwa kuwa ilikuwa hata kupiga hatua moja ni kwa shida siku hiyo na nikaapa sisafiri tena kihivyo!

  Kwa hiyo nikicheki picha na nikikumbuka yaliyonikuta , nahisi kuna unafuu.

  Ingawa ki halihalisi nashindwa kuelewa kwanini hiii huduma yenye wateja inashindikanaje kuiboresha zaidi!:-(

  Like

  Simon Kitururu

  November 4, 2011 at 7:18 pm

 2. Wow, Kitururu … Hiyo ni bonge ya experience. Miaka hiyo unayoitaja … usafiri wa treni ulikuwa ni balaa, hasa ukizingatia kwamba usafiri wa barabara nao ulikuwa na matatizo mengi mno. Unafuuu unaouona kwenye behewa hilo pengine ni kwa hapo Dar. Ila kadiri treni linavyosonga mikoani, ndivyo linavyozidi kupakia na kutoacha nafasi. Ila maswali ni mengi … ikiwa ni pamoja na hilo. Kwa nini shirika lenye ukiritimba wa biashara – linalokabiliana na ushindani mdogo sana – lishindwe kujiendesha kibiashara na kutoa huduma zinazoridhisha? Ni swali kubwa … kubwa sana. Na swali hilo waweza pia kulielekeza kwenye mashirika mengine kibao … TANESCO … TTCL … Posta n.k.

  Like

  Deo Simba

  November 5, 2011 at 12:04 am

 3. Mie mara ya mwisho ilikuwa 1993 nilikuwa natoka dar na kwenda Makambako…briiii briii briiii

  Like

  yasinta

  November 7, 2011 at 4:21 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: