simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Uhaba wa bidhaa za mafuta Tanzania …

leave a comment »

Mchoro wa Msanii mahiri Nathan Mpangala … (kutoka kwenye ukurasa wake wa Facebook)

Kizaazaa kule Ruaha, mkoani Iringa …

Kulekule Iringa … (Picha Na. 2 na 3 na Francis Godwin kupitia Fullshangwe.blogspot.com)

Kwa watani wetu wa jadi, Kenya, wastani wa bei ya bidhaa za mafuta. Petroli kwa Ksh. 115 (sawa na Tsh. 1,900) na Diseli kwa Ksh. 106 (sawa na Tsh. 1,800).

Haya, Vuta n’Kuvute imekuwa ikiendelea nchini Tanzania kati ya Serikali (kupitia Ewura) na wafanyabiashara wakubwa wa mafuta. Serikali imetoa maelekezo kwamba bei ya mafuta ipunguze. Inasadikiwa kwamba wafanyabiashara wamegomea bei hizo mpya. Kwa hiyo, kuna mvutano. Wakati hali ikiendelea kuwa hivyo kwa siku kadhaa sasa, ni Watanzania wa kawaida ndiyo wanaoteseka. Usafiri unakuwa wa tabu na aghali. Bidhaa za vyakula na huduma nyingine muhimu zinapanda sana. Wenye biashara ya usafirishaji abiria na mizigo wanapandisha bei. Wanafunzi wanateseka. Wafanyakazi wanateseka. Wafanyabiashara wanateseka. Wakulima wanateseka. Uchumi wa Taifa unaangamia.

Kadhia hii inatokea wakati ambapo nchi iko kwenye msukosuko wa umeme. Hakuna umeme wa uhakika. Mgao umetawala. Biashara ndogo kwa kubwa zinahangaika. Hakuna kinachoenda. Hakuna juhudi za makusudi zinazoonekana kuchukuliwa ili kurekebisha hali ya mambo. Jamani, nini tufanye? Nchi yetu inaangamia machoni mwetu wenyewe. Sad. Very sad indeed. Je, kwa nini tusiamini kwamba matatizo yaliyopo nchini kwetu NI ‘man-made’?

Advertisements

Written by simbadeo

August 11, 2011 at 11:59 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: