simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Uruguay … winners Copa America 2011

leave a comment »

Mpaka kipenga cha mwisho (ndani ya dakika 90), Uruguay 3, Paraguay 0.

Ilikuwa furaha uwanjani kwa upande wa Uruguay … kurukaruka … kukumbatiana … ili mradi uwanja ulijaa nderemo na vifijo vya washindi hawa wapya wa Kombe la Copa America 2011.

Mashabiki walijipamba vilivyo kwa rangi za Taifa lao …

Taarifa zilitumwa nyumbani kwa njia ya simu na nyinginezo …

Njia moja ya kupima umoja wa kitaifa ni kupitia soka. Tuliwahi kushuhudia jambo hili kule Liberia miaka ile ambapo nchi ilikuwa katikati ya vita vya wenyewe kwa wenyewe lakini vita hivi vilisitishwa kwa muda kwa ajili ya soka.

Watanzania tunajifunza nini kutokana na mashindano haya? Tunaona wachezaji wanavyojituma, wanavyopigana kwa kila inavyowezekana ili kupeleka ushindi nyumbani. Tumeliona hili kwa Wajapani (Timu ya wanawake walionyakua ubingwa wa dunia hivi karibuni) na kwa Uruguay. Katika yale tunayofanya, iwe kwenye soka, iwe kwenye kazi, iwe kwenye kilimo, iwe kwenye chochote kile … tumimine nguvu zetu zote, ubunifu wetu wote, uadilifu wetu wote … kwa kufanya hivyo, tutaona matokeo yanaanza kubadilika katika sekta mbalimbali. Ulimwengu ni darasa, hatuna budi kusoma na kujifunza kwa bidii. Hayo ndiyo maoni yangu kwa leo. Kila la kheri.

Advertisements

Written by simbadeo

July 25, 2011 at 12:36 am

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: