simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Bomb blast in Oslo …

leave a comment »

Kumetokea mlipuko wa bomu katika jiji la Oslo nchini Norway. Mlipuko huo unasemekana kuua watu wawili na kujeruhi wengine zaidi ya 15. Watu walio umbali wa kilometa kumi kutoka eneo la tukio waliliambia Shirika la Habari la BBC kwamba hata wao walisikia mlipuko huo. Mpaka sasa haijulikani ni kina nani au kundi gani hasa linalohusika na mlipuko huo. Hata hivyo, polisi nchini Norway wanaamini kwamba tukio hilo limefanywa na mgeni/wageni.

Norway ni nchi yenye utulivu huku ikiwa na idadi ya watu wasiozidi milioni sita. Kwa hiyo, tukio hili limeushtua ulimwengu kwani halikutarajiwa. Swali kubwa ni kuwa je nani hasa alilengwa kwenye mlipuko huo? Je, ni Waziri Mkuu? Maana ofisi yake ipo jirani na eneo la tukio na pia imeharibiwa upande mmoja.

Hali bado ni tete kwa kuwa hakuna anayejua kama kutatokea mlipuko mwingine kuhusiana na huu. Baadhi ya wachunguzi wa mambo wanaanza kujiuliza kama Muammar Gaddafi ana mkono katika tukio hilo. Hii inatokana na ukweli kwamba alitishia kuzishambulia nchi za Ulaya kutokana na mashambulizi yanayofanywa nchini kwake kwa lengo la kumng’oa madarakani na vikosi vya NATO. Bila shaka ukweli utaanikwa hadharani kadiri siku zitakavyopita.

Tunawapa pole waliojeruhiwa katika tukio hili na vilevile ndugu wa jamaa waliopoteza maisha yao. Kama dunia … kila mmoja wetu ajitahidi kufanya dunia yetu iwe mahali pa amani na palipo bora kuishi.

Advertisements

Written by simbadeo

July 22, 2011 at 7:48 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: