simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Bukoba Airport …

leave a comment »

SERIKALI IJENGE VIWANJA, WAFANYABIASHARA WASAFIRISHE ABIRIA

Mwonekano wa Uwanja wa Ndege wa Bukoba kutoka juu. Ni mandhari ya kupendeza. Naelewa kwamba tuna matatizo makubwa katika uendeshaji wa shirika letu la ndege la kitaifa. Hata hivyo, kadiri wadau kutoka katika sekta binafsi wanavyoingia kwenye biashara ya usafirishaji wa anga, pengine serikali ielekeze nguvu zake katika kujenga viwanja vya ndege vingi zaidi. Serikali inaweza kumiliki viwanja na kuachia sekta binafsi ifanye biashara ya usafirishaji wa anga. Kwa hiyo, kama kutakuwa na kiwanja cha ndege cha kuaminika katika kila makao makuu ya wilaya hapa nchini, na kukawa na makampuni mengi zaidi yanayosafirisha abiria kwa njia ya anga, naamini kasi ya kusaka maendeleao itaongezeka. Hakuna ubishi kuhusu mchango wa usafiri wa anga katika maendeleo ya nchi. Usafiri huo husaidia sana kuokoa muda unaotumika kusafiri kutoka kona moja hadi nyingine. Fikiria, mtu anayesafiri kwenda Mwanza kwa ndege anatumia muda usiozidi saa mbili, lakini anaposafiri kwa barabara au reli anatumia zaidi ya saa 12.

Kumbe basi serikali ikazane katika ujenzi wa viwanja vingi zaidi. Wafanyabiashara wajikite kwenye usafirishaji. Na kukiwa na makampuni mengi zaidi, ushindani utafanya usafiri wa anga uwe wa gharama nafuu na ambao watu wengi watamudu.

Chanzo cha picha: Da Chemi Che Mponda wa Swahilitimes.blogspot.com

Advertisements

Written by simbadeo

July 20, 2011 at 10:03 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: