simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Phone hacking … Murdochs on hot chair

with one comment

Rupert Murdoch: Tulilifunga gazeti la News of the World kwa sababu tuliona aibu kwa vitendo vya ‘kusikiliza’ simu za watu.

Mmoja wa Wabunge waliokuwa kwenye kamati iliyowahoji Rupert Murdoch na James Murdoch

Rupert Murdoch: Hakuna ushahidi kwamba watendaji walifahamu kuhusu ‘usikilizaji’ simu za watu.

James Murdoch: Lengo letu kubwa ni kupata kuaminiwa tena na umma.

Mpaka mahojiano yanafika mwisho, Rupert Murdoch alieleza kuwa siku hii ndiyo iliyomnyenyekeza zaidi katika maisha yake kuliko siku nyingine yoyote. Aliomba msamaha kwa wale wote ambao maisha yao yali’umizwa’ na vitendo vilivyowahi kufanywa na baadhi ya waandishi wa habari wa gazeti lake la News of the World, hasa familia ya Milly Bowler.

Tunaweza kujiuliza, sakata hili lina maana gani kwetu siye tunaoishi katika nchi zilizo mbali kabisa na Uingereza. Ukweli ni kwamba msingi mzima wa sakata hili umejijenga katika ‘kuheshimu haki ya faragha ya kila mtu’. Unapoingilia faragha ya mtu yeyote kwa njia yoyote unamvunjia mtu huyo haki yake ya kuwa binadamu. Kitendo hiki ni sawa kabisa na kuvunja haki za binadamu.

Kwa mantiki hiyo, tunaweza kujiuliza, vyombo vyetu vya habari hapa nyumbani vina mtindo huo kama uliofanywa na News of the World? Hili ni swali kubwa. Pengine ni wakati kwa vyombo vya habari kujichunguza na kujifanyia tathmini. Pengine wakati umefika pia ili kuona kwamba maadili yanayoongoza vyombo vya habari yanasimamiwa kwa uwazi na ukweli. Je, suala la umiliki wa vyombo hivyo vya habari ukoje? Je, kuna ‘ndoa’ zisizoelezeka vizuri kati ya waandishi wa habari na viongozi wa serikali, viongozi wa kisiasa, wanafanya biashara na wengine wanaotafuta kuwa na ushawishi mkubwa zaidi katika jamii? Je, uhusiano huo uko vipi? Je, maadili yanazingatiwa? Vilevile, kuna tabia za watu kufuatilia mambo ya wengine – je, wanafanya hivyo kwa misingi ya haki, misingi ya kisheria, misingi ya kuheshimu haki za binadamu?

Ama kwa hakika, sakata hili linatufundisha mengi. Ni juu yetu kufungua macho, masikio, akili na utambuzi wetu kikamilifu ili kuhakikisha kwamba tunaheshimu faragha zetu wenyewe na zile za wenzetu. Nawakilisha.

Advertisements

Written by simbadeo

July 19, 2011 at 7:45 pm

Posted in Siasa na jamii

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. .The Sun owned by media globalist Rupert Murdoch recently published an article declaring that 7 7 was a plot by the Government.

    Like

    hemp

    August 1, 2011 at 4:54 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: