simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Breaking the monotony …

with one comment

Katika maisha kuna nyakati hatuna budi kuacha shughuli tufanyazo kila siku na kwenda mahali tofauti. Kila mmoja ana hekaheka zake katika maisha. Na ninaamini kwamba hakuna hekaheka iliyo nyepesi. Na katika kukabili hekaheka hizo za maisha mara nyingine hutokea ambapo tunawakwaza wengine. Na hutokea hata pale ambapo sisi hatukukusudia. Lakini tafsiri inayoweza kutolewa na wengine tunaoingiliana nao kwa namna moja ama nyingine, basi inaweza kukuza mambo kiasi cha mtu kujikuta unageuzwa kuwa adui. Katika hali ya namna hiyo, upande mwingine hutafakari hata namna gani unaweza kukumaliza/kukuangamiza. Hapo usishangae kuona email yako inaandamwa, simu yako inaandamwa, watu unaofahamiana nao wanaandamwa, watu unaoshughulika nao wanaandamwa, hata taarifa zako binafsi za kibenki n.k. nazo zinaandamwa. Email na phone hacking hufanywa ili kutafuta ‘ushahidi’ wa kukuangamiza. Pale inapotokea kwamba ushahidi kama huo haupo maana haukuwahi kuwepo, basi ‘ushahidi’ utapikwa, utakaangangizwa, utatengenezwa, marafiki na wale unaoshughulika nao katika uzalishaji watatishwa, n.k. Nawe utajengewa mazingira hata ya kukutupa jela. Ama kwa hakika, hapa ndio tunabaki kumshangaa binadamu. Hivi, yote haya anayafanya ili iweje? Na hili, huwa ni swali kubwa. Upande huo unatumia fedha nyingi, muda mwingi … lengo likiwa ni kumwangamiza ‘daudi’ … ni kichekesho? Ni huzuni? Na dunia yetu imejaa mifano ya aina hiyo.

Kwa hiyo, katika nyakati kama hizo. Nenda nje ya mji. Kijijini. Tulia. Vuta pumzi safi. Vuta hewa isiyojaa kemikali za viwandani na moshi wa magari. Kula vyakula vya asili ambavyo havikuungwa mafuta ya viwandani. Kunywa maji unayochota moja kwa moja kutoka kwenye chemichemi. Tazama taa nyekundu. Ota moto unaotoka kwenye gogo. Keti kwenye kigoda. Zungumza maisha na wale wanaokuzunguka. Sahau TV na redio, na email, na Internet na Facebook, Twitter na blogs n.k. Sikiliza sauti ya nyani na fisi wanaolia mwituni. Vuta harufu ya nyasi. Sikiliza nyenje wanaochikicha nyasi katika nyuma. Vuta harufu ya moshi. Ninakwambia utakapotoka katika ‘retreat’ hiyo, utarudi ukiwa mpya na mwenye nguvu mpya. Hapo utapata fursa ya kuendelea na maisha yako kwa wepesi na ubunifu wa aina yake. Acha wanaopoteza fedha zao kukuchunguza na kukutengenezea mitego waendelee kupoteza, acha wapambe wao na vikaragosi vyao viendelee kufanya hivyo. Mwisho wa siku … hakuna anayeweza kuifunga nafsi yako minyororo. Watakufunga minyororo katika mwili … lakini upeo wako … akili zako … roho yako … na moyo wako vitabaki huru. Ama kwa hakika, iliwapasa kujiuliza ‘Tunafanya haya ili iweje? Kumfunga … ili? Kumwangamiza … ili? Kufurahisha nafsi zetu … ili? na at that cost?’

Ninatunuku makala hii kwa urafiki, utashi mwema na maendeleo …

Advertisements

Written by simbadeo

July 14, 2011 at 4:55 pm

Posted in Siasa na jamii

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. Ndivyo wanavyotaka! Je, wanajua kuwa tunajua kuwa wanataka iwe hivyo ili kuwaacha wale kiulaini? Wao si tayari wana majenereta waliyonunua kwa hela zetu na wanayatunza kwa hela zetu? Wanazo hata solar powers walizonunua kwa hela zetu, hata magari yao si tunayatunza kwa kodi zetu? Mimi namshukuru Mungu kuwa walau leo kuna umeme ofisini, na nyumbani wamenunua jenereta ya kisasa. Jioni ninawasha walau hadi saa tano usiku.

    Simba, haka ka-nchi kana wenyewe!

    Like

    Reginald Mbuya

    July 15, 2011 at 8:24 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: