simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Kama jirani zetu wanaweza … sisi je?

with 2 comments

Kama jirani zetu wameanza kujenga barabara za juu … na wanatumia wahandisi wenyeji kufanya kazi hiyo, sisi tunashindwa nini? Mbona wataalamu tunao wengi tu kutoka pale Mlimani na vyuo vikuu vingine nchini … achilia mbali wale tuliowalipia ili kusoma nje ya nchi? Kwani, tatizo ni nini? Pesa? Nia? Kama ni pesa … nani alisema kwamba Roma ilijengwa kwa siku moja? Si tunaweza kuanza kidogokidogo? Je, ni lazima tuanze leo na kukamilisha kesho? Je, kweli nia ipo? Kila jambo linawezekana … nia thabiti ni muhimu … ndiyo tunachohitaji. Nawasilisha.

Advertisements

Written by simbadeo

July 12, 2011 at 5:46 pm

Posted in Siasa na jamii

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. We Simba, tatizo ni kwamba waliozoea kula hela zetu wanafikiri hatujui kama inawezekana kuwa na maendeleo ya haraka. Wakiruhusu tu maendeleo, watakosa kuendelea kula. Yapo mengi Simba: angalia migodi inavyochukuliwa kirahisi, ni kwa kuwa wanafikiri hatujui thamani yake na kama tunastahili kupata pato lote; Simba, ebu angalia wanafunzi wanavyoteseka, utafikiri nchi hii ni maskini, angalia fedha zetu za kodi zinavyokwenda kwa polisi na askari kwa kuwa serikali inawaogopa-wao wakiingia porini, waturudishia hadhi yetu. Hawa wanapata mabasi kila mara makubwa kwa madogo. Hawajui kama tunajua fedha inayonunua magari hayo inatolewa na wazazi wa hawa watoto wanaoteseka barabarani wakitukanwa na konda nk. Leo wanafunzi na wazazi wangeinuka kusema baadhi ya mabasi ya jeshi na polisi yapige ruti za asubuhi na jioni kwa wanafunzi au wataacha kulipa kodi utaona mambo yanakuwa rahisi. Hiyo Kigamboni inayotaka kuwekewa daraja na NSSF katika mwongo huu, ilikuwa wapi tangu miaka yote? Si kwa kuwa walishafikiri kuwa wananchi hawajui kama inawezekana? Haka ka-nchi kameshagawanywa kati ya wakubwa; na sasa wapo mbio kujishikia mashamba makubwa makubwa ili watakapostaafu wahamie huko. Unafikiri Wazimbabwe walikosea sana walipoanza kuvamia mashamba? Unafikiri yote yalikuwa ya wazungu? Mengine yalikuwa ya wenyeji waliounga mkono ugandamizi wa kizungu kwa kuwa hao hawakugandamizika. Tukifungua macho sasa, ingawa tumechelewa tungeiamsha jamii yetu; leo hii wenyeji wa mtaa fulani wakijikusanya na kuona kodi inayoondoka ni kiasi gani na huduma za jamii zinazotolewa ni asilimia ngapi ya hizo itatokea tafrani kwani watanzania kote nchini wangeandamana kuhitaji maelezo…. nimechoka, endelea mwenyewe kwani najua majibu ya haya hakuna hadi itakapoingia serikali ya kidikteta ili kuwabana wanyonyaji wa ndani na nje.

  Like

  Reginald Mbuya

  July 12, 2011 at 11:11 pm

 2. Ndugu Reginald, asante kwa maoni yako. Yanatafakarisha. Ninawaomba wasomaji wengine pia wayatafakari. Wale walio katika nafasi ya kushawishi mabadiliko wayafikishe kule kunakohusika ili kila mwananchi katika nchi hii ajivunie utaifa wake, ajisikie kuwa na yeye ni binadamu mwenye hadhi ya utu.

  Hiloa la wachache kujigawia milki kubwakubwa za nchi limenigusa. Niliwahi kwenda kwenye nchi fulani (jina kapuni) ambapo wenyeji walinidokeza kwamba karibu robo ya ardhi yote ya nchi hiyo inamilikiwa na familia moja (jina kapuni)… fikiria … familia moja inamiliki robo ya nchi nzima???!!! Je, wakiamua kwamba wanataka kujitenga ili eneo hilo liwe nchi yao pekee nani atakayewazuia?

  Ama kwa hakika bado tuna safari ndefu ya kuifikia Tanzania ya ndoto za Julius Nyerere. Tuendelee kuwepo.

  Like

  Deo Simba

  July 12, 2011 at 11:59 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: