simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

End of the end … News Of The World closure

leave a comment »

Leo nakala ya mwisho ya gazeti lililokuwa na wasomaji zaidi ya milioni 7 la News Of The World (NOTW) limefungwa. Sababu kubwa ni skandali inayoligubika kwamba katika utendaji kazi wake, walikuwa wakitumia ‘njia’ haramu ya kusikiliza simu za watu na hatimaye kuibua kashfa mbalimbali.

Jambo hili linazua fikra nyingi sana… hasa katika ulimwengu wetu ambapo kuna wale ‘wanaojiona kwamba wako juu ya sheria’ na wengine hawana haki ya kujiletea mabadiliko chanya kwa juhudi zao wenyewe. Sheria zetu, teknolojia yetu bado viko nyuma. Kwa hiyo, bila shaka kuna watu wengi sana wasio na hatia ambao kwa namna moja au nyingine maongezi na mawasiliano yao kwa njia ya simu yamekuwa yakinaswa na ‘hao wanaojiona kuwa juu ya sheria’ kwa matumizi yao … hasa matumizi ya kuhakikisha wanawaangamiza ‘wanyonge’ wahanga wao.

Kila kitu huja na pande mbili: nzuri na mbaya. Kuja kwa teknolojia ya simu na Internet kumekuja na pande mbili. Wapo wanaotumia vema, na wapo wanaotumia vibaya. Lakini ukweli unabaki kwamba wale watakaokamatwa wakitumia vibaya teknolojia hii … hasa kwa malengo ya kuangamiza, kukandamiza, kuonea n.k. … sheria haina budi kuchukua mkondo wake … hata kama ‘wanajidai’ kuwa ‘wateule’ …’walio juu ya sheria’ … kwamba wao tu ndiyo wenye kila haki ya ‘kuendelea’ na kwamba wengine hawana haki ya ‘kujiendeleza’. Nawakilisha.

Advertisements

Written by simbadeo

July 10, 2011 at 2:06 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: