simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Happy Fathers’ Day …

with 3 comments

Maisha ya ‘baba’ ni ya kujitoa sadaka ili wale aliowaleta duniani wapate maisha yaliyo bora zaidi. Hivyo, furaha ya baba ni kuona kwamba yeye ‘anatumika kimshumaashumaa’ ili wanawe na wale wanaomtegemea wapate furaha na mafanikio. Heri ya sikukuu ya Akina Baba kwa wote wale wanaotimiza wajibu wao kama ‘baba’. Na dhana ya ubaba ni pana. Ukiitafakari sana, inavuka sana suala la ‘jinsi’. Ili Taifa letu liendelee linahitaji kujitoa sadaka kwingi na kutazama baadaye ya miaka 100 … kupanda mti leo hata kama utakapokua wewe hutakuwepo na kula matunda yake. Kuna mtu mmoja alisema, kama mimi nakula matunda ya miti ambayo sikuipanda, kwa nini wasiwepo wengine watakaokula matunda kutoka katika miti nitakayopanda mimi? Ndiyo. Ni lazima tutazame mbali zaidi ya nafsi zetu. Siku hii itukumbushe wajibu mkubwa tulio nao kwa Taifa hili, vizazi vya sasa na vile vijavyo. Uhuru wa watoto wetu na vizazi vyetu vijavyo unapaswa kushughulikiwa SASA … na ni SISI ndiyo wenye jukumu hilo.

Advertisements

Written by simbadeo

June 19, 2011 at 5:11 pm

Posted in Siasa na jamii

3 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Simba, umenigusa mahali pake. Kwani daima natamani kama baba wote wangekuwa wanajua wajibu wao. Mimi, bado sijaanza ila ubaba wa kiroho nimeuishi sana. Nakumbuka kila nilipohamia kikazi nilifanya maendeleo fulani yaliyopingwa na wengi kwa kusema ‘wewe utakaa hapa milele?, mti uupandao hautachanua maua kabla hujahama kama wengine’, kweli mara nyingi imekuwa hivyo lakini daima niliuliza, haya matunda tunayokula walipanda akina nani? Mbona pia walipanda wakaondoka? Nakumbuka nyumbani kwetu, nilipokuwa shule ya msingi, nilichukia kuwa mara zote tunaenda kwa watu kuokota maembe kwani kwetu hayapo. Nilifanya uamuzi wa kupanda miembe mingi ingawa niliweza kufikiri kuwa itakufa hata bila kuota. Cha kufurahisha ni kwamba nilipomaliza kidato cha nne Fr Kidegu, na hata Egifrid waliweza kufika kwa wakati tofauti kuchukuwa magunia ya maembe ya kutosha shule nzima. Wazazi na hata ndugu walioniona punguani ndiyo wanaofaidi sasa. Si tu kuwa walinikatisha tamaa kuwa hadi maembe yakomae sitayafaidi, ila hata wao walidai kuwa watakuwa wamekufa tayari. Cha ajabu ni kuwa hata leo wanayafurahia maembe, tena wanagombania kuwa kila mtu ayale kwa uhuru kwani yalipandwa na Rechi.

  Natamani wengi zaidi wangeisoma blog yako na kuweza kutoa maoni yao. Happ Father’s Day

  Like

  Reginald

  June 22, 2011 at 9:25 am

 2. I love the photo of u and ur family. U look great and also a very happy dad….. It good to be a dad.

  Like

  wacuka44

  September 17, 2011 at 4:53 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: