simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Haya tena … ‘liloandikwa limeandikwa’

with 6 comments

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BUNGE LA TANZANIA

Simu Na. 026 2322761-5
Fax Na. (255) 026 2324218
E-Mail: poctz@parliment.go.tz

(Barua zote za kiofisi ziandikwe kwa (Kiongozi wa Upinzani)
Unapojibu tafadhali taja:

OFISI YA BUNGE
S.L.P. 941
DODOMA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

9 Juni, 2011

“Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/2012 ina upotoshaji mkubwa”

Kutokana na Hotuba ya bajeti ya Waziri wa Fedha, Mhe. Mustafa Mkullo (Mb), aliyoitoa jana bungeni Dodoma tarehe 08/06/2011, kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya serikali kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2011/2012. Kambi ya Upinzani tumeshtushwa na upotoshaji mkubwa wa kitakwimu na kimaudhui uliofanywa na serikali kwa lengo la kuwajengea matumaini hewa wananchi kuwa watapata nafuu ya maisha kupitia bajeti hiyo wakati hali halisi haipo hivyo.

Yafuatayo ni baadhi tu ya maeneo ya waziwazi ambayo serikali ya CCM kupitia kwa Waziri wake Mhe. Mkulo iliamua kuupotosha umma wa Watanzania kwa makusudi kama ifuatavyo;

1. Wakati Waziri akitaja kuwa kipaumbele cha kwanza cha bajeti hiyo ni kumaliza tatizo la Umeme na hivyo kutamka kwamba ametenga shilingi 537 Bilioni, , upembuzi uliofanywa na Kambi yetu ya Upinzani kwenye vitabu vya bajeti (Kitabu Namba II na IV) vilivyotolewa na serikali yenyewe, umebaini kuwa Wizara ya Nishati na Madini imetengewa jumla ya kiasi cha shilingi 402,402,071,000 kwa mujibu wa fungu la 58. Fedha hizo zimegawanywa katika mafungu ya Matumizi kawaida shilingi 76,953,934,000 na kwa upande wa bajeti ya Maendeleo zimetengwa shilingi 325,448,137,000. Shilingi Bilioni 325 zilizotengwa katika Bajeti ya Maendeleo ya Wizara ya Nishati na Madini zinatosha kwa mradi mmoja tu wa umeme wa 160MW, 100 Dar es Salaam na 60 Mwanza. Hakuna mradi wowote mpya wa umeme unaonekana katika Bajeti. Ni dhahiri kuwa kauli ya Mkulo ililenga zaidi kuwajengea wananchi matumaini hewa kuliko kuchukua hatua za kweli za kumaliza tatizo la umeme.

2. Wakati Waziri na Serikali wanataka kuwaaminisha Watanzania kuwa bajeti ya mwaka huu imeongezeka kuliko ilivyokuwa mwaka 2010/2011, ukweli ni kuwa hakuna ongezeko halisia (real term increase) lililofanyika. Bajeti iliyopita ilikuwa kiasi cha shilingi 11.6 trilioni wakati mwaka huu wa 2011/2012 serikali ina bajeti ya jumla ya shilingi 13.525 trilioni. Kati ya ya fedha hizo za mwaka 2011/2012, kiasi cha shilingi 1.901 trilioni ambazo ni sawa na asilimia 14.06% ya bajeti yote, kitatumika kulipia deni la Taifa. Kwa mantiki hiyo, mtaona kuwa fedha kwa ajili ya kuendesha serikali pamoja na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo zitabaki kuwa ni kiasi cha shilingi trilioni 11.624 ambazo ni sawa na fedha za bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010/2011 (Japo thamani ya shilingi imeanguka ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwaka 2010/2011). Tunasisitiza kuwa hii si bajeti ya maendeleo, hii ni bajeti ya madeni.

3. Wakati Waziri akisema Bungeni kuwa Bajeti ya mwaka 2011/2012 itapunguza posho kama sehemu ya mkakati wa serikali wa kuthibiti matumizi, nanukuu “kupunguza malipo ya posho mbalimbali yasiyokuwa na tija (uk.53)”, ukweli ni kuwa Bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012 imetenga jumla ya shilingi 0.987 trilioni ambazo ni sawa na asilimia 13 % ya bajeti yote ya serikali kwa ajili ya kulipa posho chini ya vifungu vinavyojulikana kama “Personnel allowances (non discretionary na In-kind”). Kwa hiyo, kauli ya Waziri Mkulo kuwa serikali itapunguza posho sio kweli. Tunautaka umma wa Watanzania usikubali kurubuniwa.

4. Wakati Waziri akisema kuwa ili kuthibiti matumizi watapunguza posho mbalimbali, kwenye hotuba yake uk.66, waziri amependekeza kufanywa kwa marekebisho ya sheria ya kodi ya mapato SURA 332 na anasema kwenye (i) “kusamehe kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa wafanyakazi wa serikali na wanaofanya kazi kwenye taasisi zinazopata ruzuku kutoka kwenye bajeti ya serikali” . Hii inaonyesha dhahiri kuwa kauli ya Kufuta au kupunguza posho ilitolewa na Serikali ili kupumbaza wananchi lakini haina udhati.

5. Bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012 imewaongezea mzigo mkubwa sana wananchi na haswa wajasiriamali wadogo na vijana ambao wamejiajiri ama kuajiriwa kwenye biashara ya usafiri na usafirishaji. Tunasema hivyo, kwa sababu serikali katika bajeti vyake rasmi vya bajeti imeamua kufanya marekebisho ya sheria ya usalama barabarani sura 168 ili kuongeza ukomo wa kiwango cha faini inayotozwa kwa kufanya makosa wakati mtu akiwa anaendesha gari yaani (Traffic Notification Fee), kutoka shilingi 20,000 hadi shilingi 300,000. Lakini Waziri Mkulo katika Hotuba yake aliyoitoa jana ukurasa 74, alitamka kuwa wataongeza kiwango cha faini hadi kufikia shilingi 50,000. Ni dhahiri kuwa kauli ya waziri ya kusema faini itafikia 50,000 wakati kwenye vitabu rasmi vya bajeti faini hiyo inaonekana itafikia 300,000, hivyo alilenga kuuhadaa umma na kuupotosha.

6. Kambi ya Upinzani Bungeni imeshtushwa na kushangazwa na hatua ya Serikali kutenga zaidi ya robo ya Bajeti kulipa Madeni na Kulipana Posho (Asilimia 27 – 14% kulipa madeni na 13% kulipa Posho mbalimbali).

7. Kambi ya Upinzani itawasilisha Bungeni Bajeti Mbadala siku ya Jumatano tarehe 15.6.2011, saa tano asubuhi ambayo itakuwa inajali masilahi ya Watanzania yenye lengo la kukuza Uchumi wa Vijijini (rural growth) na itajikita katika kupata vyanzo vipya vya mapato na kubana matumizi ikiwemo kufuta Posho mbalimbali.

Imetolewa leo, Mjini Dodoma, na

Zitto Zuberi Kabwe
Waziri Kivuli wa Fedha
Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni

Chanzo: mtwarakumekucha.blogspot.com

Advertisements

Written by simbadeo

June 10, 2011 at 7:48 pm

Posted in Siasa na jamii

6 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Ahsante kwa Taafika kaka S!

  Like

  yasinta

  June 14, 2011 at 10:43 am

 2. KAMBI ya Upinzania ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano jana imewasilisha bajeti mbadala ya makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011 12 huku suala la kufutwa posho za vikao likisisitizwa..Akisoma hotuba hiyo jana kwenye kikao cha Bunge la Bajeti kinachoendelea mjini Dodoma Waziri Kivuli wa Fedha Kabwe Zitto Mbunge wa Kigoma Kaskazini alisema malipo ya posho za vikao kwa wabunge na baadhi ya watumishi wa Serikali hayana tija yoyote kwa Taifa..Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema alisema posho za vikao ambazo wabunge wanapewa kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya Bunge na vile vya kamati za Bunge zinapaswa kufutwa mara moja.. Kambi ya upinzani inapendekeza mfumo mzima wa kulipana posho za vikao sitting allowances uondoke katika utumishi wa umma. Wakati kiongozi wa umma anapolipwa posho kwa kikao cha kufanya maamuzi yanayohusiana na majukumu yake ya kazi ambayo kwayo analipwa mshahara polisi halipwi posho kwa kulinda mwalimu halipwi posho kwa kuingia darasani na wala nesi halipwi posho kwa kusafisha vidonda vya wagonjwa anasema Zitto katika hotuba hiyo..Alisema wakati Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo alisema ili kudhibiti matumizi ya Serikali watapunguza posho mbalimbali katika hotuba yake ya Bajeti ukurasa wa 66 waziri huyo alipendekeza kufanywa kwa marekebisho ya sheria ya kodi ya mapato Sura ya 332 1 ili kusamehe kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa wafanyakazi wa Serikali na wanaofanya kazi kwenye taasisi zinazopata ruzuku kutoka kwenye bajeti ya serikali..Katika hotuba hiyo alisema kutokana na pendekezo hilo tayari wameanza kusikia vilio kutoka Sekta Binafsi kwamba na wao wanataka wapate unafuu huo wa kodi.. Kambi ya upinzani inapendekeza mfumo mzima wa kulipana posho za vikao sitting allowances uondoke katika utumishi wa umma. Suala hili ni lazima tulianze sasa na katika Bajeti hii tunayoijadili.

  Like

  Panama corporation

  July 1, 2011 at 8:31 pm

 3. hi

  Like

  crimit

  July 3, 2011 at 4:25 am

 4. …..KAMBI ya Upinzani Bungeni imesema kumekuwa upotoshaji wa kitakwimu na kimaudhui katika hotuba ya Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo aliyoitoa bungeni June 8 kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya serikali kwa kipindi cha mwaka fedha wa 2011 2012.Taarifa iliyotolewa na Naibu Kiongozi wa Kambi ya upinzani bungeni Kabwe Zitto ilisema wakati Waziri Mkulo ametamka bungeni kuwa Serikali imetenga shilingi bilioni 537 kwa ajili ya Wizara ya Nishati na Madini upembuzi wa kambi ya upinzani kwenye vitabu vya bajeti Namba II NA IV umebaini kuwa Wizara hiyo imetengewa shilingi Milioni 402 402 071 000 kwa mujibu wa fungu la 58.Fedha hizo zimegawanywa katika mafungu ya matumizi kawaida shilingi Milioni 76 953 934 000 na kwa upande wa bajeti ya maendeleo zimetengwa shilingi Milioni 325 448 137 000.Shilingi Bilioni 325 zimetengwa katika bajeti ya maendeleo ya Wizara ya Nishati na Madini zinatosha kwa mradi mmoja tu wa umeme wa megawati 160 100 Dar es Salaam na 60 Mwanzaalisema Zitto. Kwa mujibu wa Zitto hakuna ongezeko halisia lililofanyika.Alisema bajeti iliyopita ilikuwa shilingi Trilioni 11.6 wakati mwaka huu wa 2011 12 Serikali ina bajeti ya jumla ya shilingi Trilioni 13.525.Kati ya fedha hizo za mwaka 2011 2012 kiasi cha shilingi Trilioni 1.901 ambazo ni sawa na 14.06 ya bajeti yote kitatumika kulipia deni deni ka taifa.Kwa mantiki hiyo mtaona kuwa fedha kwa ajili ya kuendesha serikali pamoja na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo zitabaki kuwa ni kiasi cha shilingi Trilioni 11.624 ambazo ni sawa na fedha za bajeti ya mwaka uliomalizika wa 2010 2011 japo thamani ya shilingi imenguka ikilinganishwa na hali ilivyokuwa mwaka 2010 2011 alisema Zitto.Alisema wakati Mkulo akisema bungeni kuwa bajeti ya mwaka 2011 2012 itapunguza posho kama sehemu ya mkakati wa Serikali wa kudhibiti matumizi bajeti ya Serikali imetenga shilingi Trilioni 0.987 ambazo ni sawa na asilimia 13 ya bajeti yote ya Serikali kwa ajili ya kulipa posho chini ya vifungu vinavyojulikana kama personnel allowances non-discretionary na In-kind .Zitto alisema wakati waziri akisema ili kudhitibi matumizi serikali itapunguza posho mbalimbali Waziri Mkulo amependekeza kufanywa kwa marekebisho ya sheria ya kodi ya mapato sura ya 332 na anasema kusamehe kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa wafanyakazi wa Serikali na wanaofanya kazi kwenye taasisi zinazopata ruzuku kutoka kwenye bajeti ya serikali.Kwa mujibu wa Zitto Serikali katika bajeti yake rasmi imeamua kufanya marekebisho ya sheria ya usalama barabarani sura ya 168 ili kuongeza ukomo wa kiwango cha faini inayotozwa kwa kufanya makosa wakati wa kuendesha gari yaani Traffic Notification Fee kutoka shilingi 20 000 hadi shilingi 300 000.Lakini waziri Mkulo katika hotuba ukurasa wa 74 alitamka kuwa serikali itaongeza kiwango cha faini hadi shilingi 50 000.Ni dhadhiri kuwa kauli ya Waziri ya kusema faini itafikia 50 000 wakati kwenye vitabu rasmi vya bajeti faini hiyo inaonekana itafikia 300 000 alisema Zitto.Zitto alidai kuwa Kambi ya Upinzani Bungeni imeshtushwa na kushangazwa na hatua ya Serikali kutenga zaidi ya robo ya ya bajeti kulipa madeni na kulipana posho asilimia 27-14 kulipa madeni na 13 kulipa posho mbalimbali ……Posted by.GDSS…at.

  Like

  Panama foundation

  July 4, 2011 at 12:47 pm

 5. KAMBI ya Upinzania ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano jana imewasilisha bajeti mbadala ya makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011 12 huku suala la kufutwa posho za vikao likisisitizwa..Akisoma hotuba hiyo jana kwenye kikao cha Bunge la Bajeti kinachoendelea mjini Dodoma Waziri Kivuli wa Fedha Kabwe Zitto Mbunge wa Kigoma Kaskazini alisema malipo ya posho za vikao kwa wabunge na baadhi ya watumishi wa Serikali hayana tija yoyote kwa Taifa..Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema alisema posho za vikao ambazo wabunge wanapewa kwa ajili ya kuhudhuria vikao vya Bunge na vile vya kamati za Bunge zinapaswa kufutwa mara moja.. Kambi ya upinzani inapendekeza mfumo mzima wa kulipana posho za vikao sitting allowances uondoke katika utumishi wa umma. Wakati kiongozi wa umma anapolipwa posho kwa kikao cha kufanya maamuzi yanayohusiana na majukumu yake ya kazi ambayo kwayo analipwa mshahara polisi halipwi posho kwa kulinda mwalimu halipwi posho kwa kuingia darasani na wala nesi halipwi posho kwa kusafisha vidonda vya wagonjwa anasema Zitto katika hotuba hiyo..Alisema wakati Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo alisema ili kudhibiti matumizi ya Serikali watapunguza posho mbalimbali katika hotuba yake ya Bajeti ukurasa wa 66 waziri huyo alipendekeza kufanywa kwa marekebisho ya sheria ya kodi ya mapato Sura ya 332 1 ili kusamehe kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa wafanyakazi wa Serikali na wanaofanya kazi kwenye taasisi zinazopata ruzuku kutoka kwenye bajeti ya serikali..Katika hotuba hiyo alisema kutokana na pendekezo hilo tayari wameanza kusikia vilio kutoka Sekta Binafsi kwamba na wao wanataka wapate unafuu huo wa kodi.. Kambi ya upinzani inapendekeza mfumo mzima wa kulipana posho za vikao sitting allowances uondoke katika utumishi wa umma.

  Like

  Panama foundation

  July 4, 2011 at 11:56 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: