simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Nafanya ukulima …

with 3 comments

Ndiyo… unapokuwa benchi, huna budi kutafuta mahali pa kupeleka nguvu zako, huko ni wapi kama si shamba? Na, wahenga walisema, jembe halimtupi mkulima. Sitakosa mawili matatu ya kuwachomea watoto ili kupunguza njaa yao. Mjenga nchi ni mwananchi.

Moja ya maoni kuhusu makala hii:

Nimeona ubunifu wako Simba. Sasa mi nifanyeje? Mbona nakaa ktk chumba kimoja tena ghorofani na bado sina shamba wala kiwanja? … SOMA ZAIDI kwenye sehemu ya Maoni.

Advertisements

Written by simbadeo

May 22, 2011 at 4:16 pm

Posted in Siasa na jamii

3 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. NI KWELI KABISA KAKA DEO NAKUBALIANA NA UJUMBE WAKO ASILIMIA ZOTE MIA .WAAMBIE WATANZANIA WANAOHITAJI ARDHI YENYE RUTUBA NA ENEO LENYE MVUA YA KUTOSHA WAJE MWESE ,MPANDA KWANI HIKU KWETU ARDHI YENYE RUTUBA INATAFUTA WATU

  Like

  MWL SWILLA

  May 22, 2011 at 5:11 pm

 2. Nimeona ubunifu wako Simba. Sasa mi nifanyeje? Mbona nakaa ktk chumba kimoja tena ghorofani na bado sina shamba wala kiwanja? Nikiwa nimeboeka, niende kariakoo kusafisha ile mitaro iliyojaa nanihiii za matajiri? city wameshindwa kusafisha ingawa kodi wanachukuwa kila kukicha; wafanyabiashara ndogondogo na kubwa kubwa wanalia kila siku; pesa wanatoa lakini zinaliwa, unaonaje Simba? nikikosa kazi niende kufanya burebure ingawa wameshakula pesa ya watu? Natamani ningekuwa MP fulani wa pale niwatokee hata kwa mabomu ya machozi waache kula hela za wananchi. Je, ni nchi hii hii inayoitwa huru watu wanateseka katikati ya jiji kama hili? Nachoka kuitwa mtanzania Simba, naona aibu kwani kila kitu kimebinafsishwa, si ajabu hata ikulu iwe imeshabinafsishwa na mtu fulani kwani kila leo tunaambiwa hakuna hela; TRA wanaendelea kukusanya na wanaonekana wakiwa na afya nzuri tena wakijijengea majumbamajumba na kuendesha magari ya kifahari. Inauma, naona aibu kuitwa mtanzania kwani zaidi ya robo tatu ni wakimbizi katika nchi yao wenyewe. Hatuna wa kumwambia haya kwani wote wanaohusika wameshakubaliana kutunyonya hadi tone la mwisho. Angalia wanafunzi wanavyoteseka kwenda na kutoka shuleni, tena angalia wanavyokaa chini, tena walimu hawatoshi kwani hakuna hela ya kuwalipa. Ila angalia polisi na jeshi wanavyobadilisha magari na mabasi yanayotunzwa kwa kodi ya wananchi. Ikulu imeshindwa kuona hata kuwa wanatoa walau mabasi mawili ya jeshi yawe yanatoka Mbagala hadi Ubungo, Mawili Gongo la Mboto hadi Ubungo walau asubuhi na jioni tu ili kuwaonesha watu wa dar kuwa wanaona? Mabasi mengi kabisa yamekaa tu hali watoto wa wakatwa kodi wanateseka. Wanasubiri uchaguzi mkuu 2015 ndiyo waseme watatoa mabasi kwa ajili ya wanafunzi? Ukulima nifanyie wapi? Hata kama ningekuwa na shamba, si ningejikata miguu nikilima na mawazo yote haya? Simba, huoni hii ni sababu kubwa ya watu kuamua kunywa pombe ili wasahau shida zao kama ilivyoandikwa katika bibilia? Haya endelea kulima, mimi nitakuja kununua mahindi yako kwa bei rahisi, kila mwindi mmoja 200, nikawachomee wanangu wanaochezea computer huko ikulu

  Like

  Reginald

  May 24, 2011 at 9:10 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: