simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Kinyerezi … mradi wa viwanja … mgogoro mkubwa

with 3 comments

Mmoja wa viongozi wa kamati ya ardhi ya wananchi wa Kifugu-Kinyerezi akiwasomea wananchi maendeleo ya mgogoro wa ardhi unaozidi kurindima katika eneo hilo ambapo katika maelezo yake alidai kwamba wananchi walifungua kesi dhidi ya Manispaa ya Ilala katika Mahakama ya Ardhi kwa kesi Na. 280/2009 ambayo bado inaendelea kusikilizwa … na tarehe nyingine iliyopangwa ni tarehe 31 Mei 2011.

Moja ya mabango waliyobeba wananchi …

Mmoja wa wananchi, Mzee Oswald Fabian Sokoni ambaye alidai kwamba aliwahi hata kuwekwa ndani kwa ajili ya mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na Manispaa ya Ilala katika kitongoji cha Kifuru, Kata ya Kinyerezi. Msimamo wake: Tusiutambue Mradi huu. Maeneo ya watu Yarudi kama yalivyokuwa hapo awali.

Elizabeth: Nalikemea zoezi hili na LISHINDWE!

Mbonea Silvano: Thamani ya vyura wa Kihansi iwe chini kuliko ya kwetu sisi binadamu! Yaliyotokea Madale (Manispaa ya Kinondoni) hivi karibuni yasijirudie hapa!

Mohamed Ali Ahmed: Kwa kuendesha utaratibu wa upimaji na uhakiki, Serikali imevunja sheria … imechelewa kulipa fidia stahiki katika muda stahiki … Tuweke Court Injunction!

Sarah Agaya: Silitaki zoezi hili, NI BATILI!

Hasira … tunadhulumiwa …

Mama Uji wa Mwana … hata MIMI silitaki zoezi hili … linatunyonya haki zetu!

Wananchi wakiendelea kudai kwamba Mradi huo ni batili na kwamba lengo lake kubwa ni kuleta mgogoro miongoni mwa wananchi … waliapa kwamba hawatakubali.

Sehemu ya umati wa wananchi walioshiriki kwenye mkutano huo …

Umati …

Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Kifuru … Bi Lucrecia Shayo …

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kifuru … Michael Msome. Yeye alitoa taarifa kwamba katika mkutano huo, walikuwa wamemwalika Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Mkuu wa Mradi wa Viwanja na kwamba wote hao hawakuwepo kwenye mkutano huo kwa sababu mbalimbali, kwamba RC hakujibu barua ya mwaliko, DC yupo safarini, DED na Mayor wamepatwa na dharura na wengine haijulikani kwa nini hawakufika na hakuna hata mmoja aliyetuma mwakilishi.
Alizidi kudai kwamba sababu ya kuitisha mkutano huo ni kufuatia barua ambayo ofisi yake ilipokea tarehe 3/5/2011 kumwarifu kuhusu zoezi la viwanja; na tangazo la Manispaa ya Ilala lililotolewa kupitia gazeti la Mtanzania la tarehe 16/05/2011, ambapo kwa maoni yake, hakukuwa na ushirikishwaji wa wananchi hata chembe.

Diwani wa Kata ya Kinyerezi, Leah B. Ng’itu. Yeye alidai kwamba ndiye aliyeshawishi kusitishwa kwa zoezi la utoaji fomu za kuchukua viwanja vilivyopimwa, alidai kwamba aliishinikiza Manispaa kuwashirikisha wananchi hatua kwa hatua. Aliongeza kwamba lengo la kuwakaribisha viongozi wakuu wa Mkoa wa Dar es Salaam lilikuwa kuwakutanisha na wananchi ili kueleza kwa nini wananchi hawakushirikishwa katika zoezi zima tokea awali?

Aliahidi kwa kusema: “Sitakubali kuona mwananchi yeyote wa Kinyerezi akichakachuliwa”. Aliongeza: “Viongozi hawa, wataingia tu kwenye 18 zetu … Tutatetea haki zetu … Serikali itambue kukimbia tatizo si kutatua tatizo … Kesi ya shamba inaishia shambani … Hakitaeleweka mpaka waje … Viongozi wametunyima ushirikiano.’

Mmoja wa viongozi wa kamati ya wananchi ya kufuatilia mgogoro wa ardhi kati yao na Manispaa ya Ilala.

Advertisements

Written by simbadeo

May 21, 2011 at 5:53 pm

Posted in Siasa na jamii

3 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Poleni sana ndugu zangu wa Kinyerezi, Pia hongera sana Diwani wa Kata ya kinyerezi kwa kuwatetea wananchi wako waliokupa kura zao huo ndio uadilifu wa kazi unaotakiwa, Nimalizie kwa hao viongozi walioalikwa kwenye mkutano na hawakufika wanaagenda gani na wananchi wao?????????? “Cha ajabu hawakufika wote”

  Like

  Kaka Simba

  May 23, 2011 at 11:54 am

 2. Poleni sana ndugu zangu wa Kinyerezi, Pia hongera sana Diwani wa Kata ya kinyerezi kwa kuwatetea wananchi wako waliokupa kura zao huo ndio uadilifu wa kazi unaotakiwa, Nimalizie kwa hao viongozi walioalikwa kwenye mkutano na hawakufika wanaagenda gani na wananchi wao?????????? “Cha ajabu hawakufika wote”

  Like

  dorine

  May 23, 2011 at 11:57 am

 3. MIRADI YA KUPIMA VIWANJA VILIVYOKWISHA ENDELEZWA UNAWAPA “KULA” VIONGOZI WETU, YANAUNDWA MAZINGIRA YATAKAYOHALALISHA ULIPAJI WA FIDIA FEKI ILI WAKUBWA WAPATE PA KUCHOTEA FEDHA KWA KUWALIPA WAHUSIKA FIDIA ZISIZOWEZA KUNUNUA HATA BAKULI. HAIWEZEKANI HATA KWA UCHAWI IWEPO NYUMBA YA KUJENGWA KWA LAKI 8 KARNE HII YA 21. LABDA CHOO CHA SHIMO KISICHOFUNIKWA.

  Hiyo ni tisa tu, kumi ni pale ambapo Mtathmini (Valuer) wa hizo zinazoitwa “Halmashauri” anapofika eneo lililokwisha endelezwa kwa ujenzi wa nyumba bora za kisasa kulazimisha kutambua uwepo wa MITI tu bila kuitambua nyumba iliyopo na kuiingiza kwenye ORODHA YA VILIVYOKUTWA SITE. Nasema kwa uchungu kwamba kutotambua nyumba yangu niliyoijenga kwa thamani isiyopongua Mil. 35 kwa mikopo na shida nyingi ni sawa na KUHALALISHA VITA YA MSITUNI (GORILLAR WARS). KWA HUU MRADI WA KINYEREZI/KIFURU WATEGEMEE VITA KALI KULIKO YA TEGETA. Nawashauri waandae Defender nyingi na vyumba vya mahabusu maana TAYARI WANA WATEJA WA KUTOSHA TU.

  Serikali itambue kuwa Serikali za Misri, Libya, Syria, Morroco na kwingineko zilijifanya njema sana kwa wananchi huku zikiendeleza ukandamizaji na uonevu kama huu unaomgusa mtu mmoja mmoja binafsi. Siku hawa watu wakiamua kuungana, hakuna gereza litakalofaa kuwaweka. TUMESHAANZA KUONA MIFANO HAI KAMA ILE YA TEGETA LAKINI KWA KUWA SERIKALI YETU SIKU ZOTE NI “MUCHKNOW’ na “FORCES-ORIENTED” wanajifanya kichwa ngumu. Ni Halmashauri/Wizara gani isiyojua mahitaji ya sasa ya ardhi za ujenzi kwa wananchi wake. Wanakuwa wapi kuvamia mapori na kuyapima kabla wananchi hawajayanunua kwa wenyeji na kuyaendeleza? NINI MAANA YA KUWA NA SERIKALI KAMA HAIWEZI KUWA “PROACTIVE”?. ULIONA WAPI MSINGI UNAJENGWA BAADA YA NYUMBA KUEZEKWA? NDO KUSEMA SERIKALI HAINA MIPANGO AU WANAFAIDIKA NA ZOEZI LA ULIPAJI “FIDIA FEKI HIVYO KUSUBIRI KWANZA WALIPWA FIDIA WAPATIKANE MAANA NI MRADI WA KUJAZA MATUMBO YAO?

  USHAURI WA BURE: Wenye viwanja Kinyerezi/Kifuru wasiingizwe kwenye ushindani wa kugombea viwanja viliyopimwa (Maana tayari walikwisha vilipia kwa kununua toka kwa wenye mashamba). Badala yake wapewe fomu maalum (hata kama watalipia ada ya fomu) zinazowapa kipaumbele cha kupewa viwanja na nyumba zao kwanza kwa saizi zitakazopimwa NDIPO WATU WENGINE WASHINDANIE VIWANJA VILIVYOBAKI. Hilo litasaidia zoezi hili kufanyika kwa ustaarabu. VINGINEVYO…………..

  Like

  jonathan/Baba Fay

  May 24, 2011 at 7:32 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: