simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Utanzania wetu … tusiupoteze

with one comment

Jana Wakristo nchini Tanzania waliungana na wenzao duniani ili kusherehekea sikukuu ya Kufufuka kwa Yesu Kristo ikiwa ni siku ya tatu tangu asulubiwe. Kwa Wakristo hii ni moja ya siku muhimu sana katika imani yao.

Katika pitapita zangu … nilijikuta nimeibukia katika eneo la beach lililo mbele ya Hospitali ya Aga Khan. Hakukuwa na watu wengi sana kama ilivyo katika fukwe za bahari maeneo ya Koko Beach na kwingineko. Hata hivyo, watu waliokuwa pale si haba.

Nilipitapita huku na kule miongoni mwa watu na nilijisikia kufarijika sana. Nilifarijika na kujivunia U-Tanzania wangu. Miongoni mwa watu waliokuwa pale, niliweza kabisa pasipo shaka yoyote kumaizi kwamba SI wote waliokuwa pale walikuwa Wakristo. Nilimaizi hilo kwa mwonekano na mavazi ya watu mbalimbali na kwa yale waliyokuwa wakiongea. Niligundua kitu kimoja ambacho ni sifa pekee ya Watanzania. UDINI hauna nafasi katika maisha ya Watanzania wa kawaida. Inapokuwa sikukuu ya Wakristo, wapo Waislamu wengi tu ambao hujumuika nao na kusherehekea, vilevile, inapokuwa sikukuu ya Waislamu, Wakristo wengi tu hujumuika nao na kusherehekea.

Ama kwa hakika hili lilikuwa fundisho kubwa kwangu … sijui wewe unalionaje … ingawa mfukoni sikuwa na hata senti moja lakini nilirejea nyumbani nikiwa na amani tele … nikiwa najivunia U-Tanzania wangu. Jamani, tusipoteze tunu hii. Wala tusikubali watu fulani wachache watuburuze na kutuingiza kwenye udini. Tuendelee kuheshimiana na kushirikiana kama ambavyo tumekuwa tukifanya miaka yote.

Hali hii ya jana … inanikumbusha enzi za utoto wangu … mitaa ya Sharrif Shamba. Wakati huo sisi watoto hatukujua habari za Ukristo wala Uislamu … tulichojua ni kusherehekea … iwe Idd, iwe Pasaka, Iwe Krismasi … huku tukiwa na shilingi zetu mbili tatu mfukoni … tulirandaranda mitaani na kufurahia sikukuu … Tuendeleze hali hii.

Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu Ibariki Afrika.

Advertisements

Written by simbadeo

April 25, 2011 at 2:46 pm

Posted in Siasa na jamii

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. Na pia wabariki watu wake… ili uafrika hhalisi udumu milele na milele…Nimeipenda mada hii

    Like

    yasinta

    April 26, 2011 at 12:55 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: