simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Tume ya kuratibu maoni kuhusu Katiba … njia nyembamba

with one comment

Barabara ni nyembamba. Lori limekwama hapo katikati. Ni kwenye mteremko. Umakini ukikosekana, lori hilo linaweza kurudi nyuma. Ni jambo linaloweza kusababisha matatizo mengi.

Mchakato unaohusu kile kinachoaminika kuja kuwa Katiba mpya umeanza. Matukio ya wiki hii yanaonesha kwamba UANZAJI huu umekuwa na mushkeri … si kidogo … sana. Mabomu yamerindima. Mizengwe imetokea kwa watoto kujimwaga ukumbini na kushika nafasi zote … huku wakiwa hawachangii michango yoyote kwa Kamati ya kuratibu maoni ya muswada wa katiba. Mchakato mzima umeanza kwa kulalamikiwa na kunung’unikiwa na wasomi, wanaharakati, wananchi wa kawaida, wanasiasa na watu wengine wengi wenye weledi mkubwa wa kuchambua hoja na kutoa hoja.

Tunaweza kulinganisha hali hiyo na hilo lori hapo juu. Kwa ufupi, unahitajika umakini wa hali ya juu ili kukamilisha jambo hili kwa ufanisi na kuleta tija ambayo ndiyo matarajio ya wengi katika Taifa hili. Kama tutalishughulikia vibaya, litaporomoka na maangamizi litakayosababisha … si haba.

Nawakilisha.

Advertisements

Written by simbadeo

April 10, 2011 at 12:52 pm

Posted in Siasa na jamii

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. Maoni yangu kuhusu katiba mpya ya Tanzania.Napenda kuchukua fursa hii kama mtanzania mambo yanayotakiwa kuwemo katika katiba mpya.1]Raisi awe tu mkuu wa Nchi asiwe kiongozi wa Serikali kama ilivyo sasa.Cheo hicho kiwe ni cha kiheshima zaidi kama ilivyo Ujerumani.Waziri mkuu awe mkuu wa Serikali mwenye mamlaka.Tume ya uchaguzi iwe huru na pia isiteuliwe na Raisi.Zitangazwe nafasi za kazi,kisha waomboji wasailiwe na Bunge.Baada ya kila uchaguzi zipite siku 100 kabla ya kuwaapisha rasmi washindi ama ni wabunge ama Raisi,ili kutoa muda kwa tume kupitia malalamiko mbalimbali yatakayojitokeza baada ya uchaguzi.Mbunge achaguliwe mara mbili tu,kama ilivyo kwa Raisi.

    Like

    Ambrose Fratern Polle

    July 14, 2012 at 11:56 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: