simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Ujenzi …

with one comment

Dar es Salaam inajengwa kwa kasi kubwa sana. Kila mahali unapokwenda kuna shughuli kedekede za ujenzi zinaendelea. Sekta hii imekuwa ikiajiri vijana wengi sana. Pengine ingefaa taasisi kama NSSF kujaribu kutafuta wanachama miongoni mwao ili kukuza zaidi mfuko huo na wakati huohuo kuwawekea vijana hawa akiba ya baadaye. Maana ni kazi ambayo inaambatana na hatari nyingi, na ni kazi ambayo mtu anaweza kufanya mpaka katika umri fulani tu.

Hata hivyo, hilo silo nililotaka kutafakari kwa siku ya leo. Leo natafakari kuhusu ujenzi wa mabondeni. Kinapofika kipindi cha mvua kama hiki tulicho nacho ndipo tunakumbuka kuhusu hatari za ujenzi wa mabondeni, na wanasiasa wetu viongozi nao utawasikia ‘hameni, mtasombwa na mafuriko’. Lakini inapofika wakati wa jua kali, tunasahau. Hatusikii kelele hizo. Nadhani ipo haja kwa mamlaka zinazohusika kuchukua hatua za makusudi kabisa kuzuia ujenzi katika maeneo ya mabonde. Dar es Salaam bado ni kubwa na ikibidi mipaka yake inaweza kupanuliwa hadi Bagamoyo, Kibaha, Kisarawe na Mkuranga.

Ujenzi mabondeni una athari nyingi, siyo ya mafuriko tu, bali pia ndiyo maeneo ya mazalia ya mbu. Mara nyingi huwa tunasema kwamba mbu ndiyo wanaoeneza malaria, lakini tunasahau kwamba binadamu pia anaeneza malaria. Maana kama sote tutajitahidi kujikinga dhidi ya mbu, hakuna atakayeambukizwa malaria. Mbu wanaomwuma mtu mwenye malaria ndiyo wanaoipeleka malaria au vimelea vya malaria kwa mwingine asiye na vimelea hivyo. Kwa mantiki hiyo binadamu pia ni waenezaji wa malaria.

Tunaoishi mabondeni … tufanye hima tuhamie maeneo ya juu. Visenti vyetu tunavyotaka kuweka kwenye majengo, tuvihamishie katika maeneo yaliyo salama zaidi.

Ndiyo ujumbe wa leo.

Advertisements

Written by simbadeo

April 5, 2011 at 5:09 pm

Posted in Siasa na jamii

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. are you on linkedin?

    Like


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: