simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Maua sawa … taa za barabarani je?

with one comment

Kuna kazi inaendelea katika kipande kimoja cha Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam. Hii ni ya kupanda miche ya miti ya maua. Ni mpango mzuri. Utasaidia kufanya taswira ya mtaa huo iwe ya kupendeza zaidi. Na hasa kwa vile huu ni msimu wa mvua, bila shaka maua hayo yataanza kukua vema … Na baada ya muda yatapata kimo cha kutosha. Ninachojiuliza tu ni kwamba katika barabara hiyo tayari kuna miti (ya mwarobaini) ambayo imefikia kimo kizuri. Miti hiyo ikidhibitiwa vizuri ili kuzuia isitengeneze vichaka tayari inapendezesha madhari. Nachelea kwamba miche hiyo ya maua inayopandwa sasa hivi isije kuleta vichaka kiasi cha kuwafanya madereva wanaotumia barabara hiyo kutoona vema. Na zaidi sana nyakati za usiku ambapo hata taa za barabarani huwaka kwa kusuasua.

Tukirejesha kumbukumbu zetu nyuma … kuna ajali nyingi za barabarani ambazo zimekuwa zikitokea katika barabara hiyo muhimu jijini Dar es Salaam na hasa nyakati za usiku. Pale Kipawa kuna magari yanayoingia kutoka JET. Ajali nyingi zimetokea pale, nakumbuka kuna kipindi daladala moja iliwahi kuliingia lori la mchanga na kuua karibu abiria wote waliokuwa ndani yake. Hata amri ilitolewa kwamba maua yaliyokuwa yamepandwa pale yang’olewe ili madereva waone vizuri zaidi. Jambo hilo lilifanyika.

Licha ya mpango mzuri wa kupendezesha mazingira … ni vema kutafakari pia ni mambo gani yanaweza kuletwa na mipango hiyo. Kwa mfano, ingewezekana kabisa kupendezesha madhari hayo kwa kupanda nyasi tu ambazo zenyewe hazina kimo kirefu… hizo zingependezesha mazingira na kuzuia mmomonyoko wa udongo. Yote yanawezekana. Tutafakari.

Advertisements

Written by simbadeo

April 3, 2011 at 10:56 am

Posted in Siasa na jamii

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. are you on linkedin?

    Like


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: