simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Libya: Kanali Muammar Quaddafi kuhimili mapigo hadi lini? …

leave a comment »

Libya surrounded by heavily and state-of-the-art weaponry of the allied forces operating under UN resolution 1973 imposing a no-fly zone over Libya …. (Map by BBC)

Colonel Muammar Gaddafi … in a possible contemplation of his future and that of his country? (Photo Byo24NEWS).

Libyan government vehicle wreckages seen on the road to Benghazi after they were bombarded by French air missiles … (Photo: Reuters)

Africa Union security council summit in Addis Ababa – Ethiopia … Au pledges to protect Libya’s sovereignity … (Photo: Bulawayo24NEWS).

Hali ya mambo nchini Libya inazidi kuwa tete ikiwa ni zaidi ya saa 48 tangu majeshi ya ushirika yalipoanza kuipiga makombora Libya kwa baraka za Azimio namba 1973 la Umoja wa Mataifa linalozuia ndege za Libya kuruka katika anga la nchi hiyo.

Ufaransa ndiyo iliyoanza mashambulizi hayo, kisha kufuatiwa na Uingereza na Marekani. Kwa mujibu wa ripoti za mashambulizi hayo, mipango ya majeshi ya washirika inakwenda vema. Rais Obama wa Marekani alikaririwa akisema kwamba huenda mashambulizi hayo yakadumu kwa siku kadhaa tu na wala si majuma mengi.

Taarifa kutoka Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilieleza kwamba majeshi ya nchi hiyo yakitumia teknolojia ya kisasa kabisa yalishambulia kiwanja muhimu cha kijeshi cha Rais Muammar Gaddafi.

Inaaminika kwamba hadi sasa majeshi ya nchi washirika yalikwishapiga kwa shabaha kabisa kiasi cha makombora 112 kwa pamoja.

Muammar Gaddafi alikaririwa kupitia Televisheni ya nchi hiyo akisema kwamba kushambuliwa kwa nchi yake na majeshi hayo ya nchi washirika ilikuwa ni sawa na ‘ugaidi’ dhidi ya watu wake na kwamba atampa silaha kila raia wa nchi yake ili kuipigania nchi hiyo.

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, alitarajiwa kukutana na majemadari wanaoongoza vita hivyo vilivyopachikwa jina la Operation Cobra Crisis ili kujadili maendeleo ya vita. Alisema: “Tunafanya kilicho cha lazima, kinachozingatia sheria, na cha haki.”

Nchi washirika katika mashambulizi hayo ni pamoja na Marekani, Ufaransa, Italia na Canada. Mashambulizi hayo pia yana baraka za Umoja wa Nchi za Kiarabu.

Taarifa kutoka Tripoli, mji mkuu wa Libya, zinadai kwamba mashambulizi hayo ya anga tayari yameua watu 48 na kujeruhi wengine zaidi ya 100 licha ya kufanya uharibifu mkubwa.

Wakati huohuo wafuasi wa Kanali Gaddafi wamejitokeza kwa maelfu na kwenda kwenye ngome yake ili kumpa kinga dhidi ya mashambulizi ya anga kiongozi wao huyo. Wapo waliosikika kwamba hawataki kuona nchi yao ikivamiwa na majeshi ya nje na kwamba watafanya kila wanaloweza kumtetea kiongozi na kuitetea nchi yao hata ikibidi kwenda nchi za ng’ambo, hasa za magharibi, na kujitoa muhanga kwa kujilipua mabomu katika balozi za mataifa hayo washirika.

Africa kupitia Umoja wa Africa (AU) imejiweka njia panda baada ya kutamka kwa pamoja kupitia baraza lake la Amani na Usalama hivi karibuni Jijini Addis Ababa, Ethiopia, kutaka kulinda mshikamano wa nchi ya Libya kama taifa moja na kupinga uingiliaji wowote wa kijeshi katika kutatua mzozo ulioikumba nchi hiyo. Si ajabu kwamba msimamo huu umezifanya hata nchi washirika katika mashambulizi haya kutoshirikisha hata taifa moja kutoka Afrika. Ni kama kusema kwamba nchi za Kiafrika zimewekwa kando katika suala zima la Libya na uamuzi wote unafanywa na mataifa hayo washirika. Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini alikaririwa kutaka kupeleka wajumbe wa amani nchini Libya ili kujaribu kufanya mazungumzo. Mataifa ya Afrika yalisema kupitia AU kwamba ni vema kwanza kutuma wajumbe ili kujionea hali halisi ya mambo nchini Libya kabla ya kuchukua hatua za kijeshi. Hata hivyo, mataifa ya magharibi yaliona kwamba Gaddafi alikuwa akijaribu kuuchezea ulimwengu kwa kuendelea kuua watu wake mwenyewe, hasa wale waliokuwa wakitaka mabadiliko ya kiutawala na kiuongozi nchini humo.

Habari hii ni kutoka vyanzo mbalimbali vya mtandao wa intaneti.

Advertisements

Written by simbadeo

March 21, 2011 at 12:19 am

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: