simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Tanzania on Gbagbo …

leave a comment »

Wikipedia image (http://en.wikipedia.org/wiki/Laurent_Gbagbo) showing ‘former’ President of Ivory Coast ….

Following the 2010 presidential election, Gbagbo has been urged to stand down in favour of Alassane Ouattara, after the election cited Ouattara the winner, by the international community, including the Economic Community of West African States of which Côte d’Ivoire is currently a suspended member. The AU also has voted in favour of Alassane Quattara amid controversial ‘statements’ being made by the Organ, particularly, in position towards political unrest in Libya. Tanzania supports AU position as regards to Ivorian political tension.

Membe: Hatumtambui Gbagbo

na Datus Boniface

SERIKALI ya Tanzania ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Afrika (AU) imetangaza rasmi kutomtambua rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo na kusema kuwa ikiwa kutatokea vita dhidi ya rais huyo basi vita hiyo itakuwa ni vita halali kwa manufaa ya kidemokrasia.

Aidha, kwa upande mwingine imebariki hatua zozote zitakazo amriwa kumtoa kiongozi huyo anayeng’ang’ania madarakani licha ya matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Novemba kuonyesha ameshindwa.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe wakati akifafanua matokeo ya mkutano wa usuluhishi uliofanyika Mjini Addis Ababa, Ethiopia.

“Tunajua uamuzi huu wa kutomtambua Gbagbo utaleta vita nchini humo, nitoe shaka kwamba ni bora iwe vita ya kutafuta demokrasia ya wananchi wa Ivory Coast…., itakuwa vita halali,” alisema Waziri Membe.

Alisema katika kikao kilichofanyika mjini humo AU ilitangaza kumtambua mpinzani wa Gbagbo Alassane Quatarra kama Rais halali na si vinginevyo.

Waziri Membe alisema jopo la viongozi watano; Rais wa Mauritania Mohammed Ould Abdel Aziz, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Idriss Deby wa Chad pamoja na Blaise Compaore wa Burkina Faso, kwa kauli moja walikubaliana kumtambua Quatarra.

Kwa uchunguzi waliofanya wamegundua kwamba Quatarra, alishinda kwa asilimia 54 lakini baraza la Katiba likachakachua matokeo hayo.

Katika kikao hicho Laurent Gbagbo alisusa kuhudhuria na badala yake alimtuma kiongozi wa chama chake Pascal Affi N’Guessan.

Mwakilishi wake huyo alipinga uamuzi uliofikiwa ndani ya kikao hicho, na kwamba hawakubaliki kwa Gbagbo kuondoka madarakani.

Wakati huohuo, serikali imetuma salamu za rambirambi kwa serikali ya Japan kufuatia kutokea kwa maafa ya tetemeko la ardhi.

Akitoa salama kwa niaba ya Rais Kikwete, Waziri Membe alisema Watanzania wako pamoja na taifa hilo katika kipindi hiki kigumu.

Kwa upande mwingine Waziri Membe alielezea kuhusiana na taarifa ya kutekwa wa Watanzania 16 na waharamia nchini Madagascar, na kusema tayari Watanzania hao wameachiwa huru na mipango inaandaliwa ya kurudishwa nchini.

Alisema maharamia hao wamekamatwa na wanatarajiwa kufunguliwa mashitaka kwa kuhusika na tukio hilo.

Source: Tanzania Daima Jumapili 13 Machi 2011

Aisee! Kumbe … kazi kwelikweli … coming behind the tail … lost glory … when gonna we find you again? (Just thinking aloud).

Advertisements

Written by simbadeo

March 13, 2011 at 6:10 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: