simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Siku ya Kimataifa ya Wanawake …

with 3 comments

Shughuli anayofanya mama huyu … ni shughuli ambayo kwayo watu wengi … wasomi wakiwemo … imewalea. Kazi na biashara ya pombe za kienyeji hutoa mchango mkubwa sana kwa uchumi wa jamii zinazoishi vijijini na hata baadhi ya maeneo ya mijini. Sehemu kubwa ya mchango huu hutumika katika maisha ya kila siku ya familia: kununua mahitaji muhimu, kununua dawa na mahitaji ya shule, kulipa karo n.k. Na kwa kiasi kikubwa biashara hii huendeshwa na akina mama. Kwa mantiki hiyo, tunaweza kusema kwa kujiamini kabisa kwamba akina mama ndiyo wanaobeba uchumi wa Taifa hili kwa njia mbalimbali ikiwemo upikaji na uuzaji pombe. Tunapoadhimisha sikukuu yao leo, tuwakumbuke akina mama wote, hususani wale ambao wanajitoa sadaka kupita kiasi ili familia zao ziendelee.

Kama leo hii tungepiga hesabu ili kujua ni wasomi wangapi nchini mwetu wamepata elimu yao kutokana na biashara hii ya uuzaji pombe, bila shaka takwimu hizo zingetushtua.

Tuache kunyanyasa akina mama. Tuwaheshimu na kuwajali kama binadamu kamili. Hongereni akina mama popote mlipo ulimwenguni humu.

Advertisements

Written by simbadeo

March 8, 2011 at 11:26 am

Posted in Siasa na jamii

3 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Hongera wanawake wote duniani kwa siku yetu hii maalumu. Pia hongera akina baba kwa kuwa bega kwa bega nasi!!

  Like

  yasinta

  March 8, 2011 at 4:55 pm

 2. Hi, Yasinta. Umenena kweli. Akina mama popote ulimwenguni wanastahili pongezi – sio katika siku hii tu bali siku zote. Wanaume pia … japo kuna wengine ambao … wanafanya ulimwengu wetu uende sivyo ndivyo. Tuko pamoja!

  Like

  DEOGRATIAS SIMBA

  March 8, 2011 at 5:12 pm

 3. Nakubalina nawe HAKUNA KAMA MAMA. Na amini mwanamke akisimama anaweza kila kitu kwani ni jeshi la jamii . wanawake tunaweza kabisa tukijishughulika na kusimama imara. Ndio hata kama wanaume wanafanya ulimwengu uende sivyo lakini wanawake bila wanaume ..sijui–

  Like

  yasinta

  March 8, 2011 at 6:47 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: