simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Kigilagila JET yaifuata Kipawa …

with 2 comments

Kigilagila JET … nayo yapigwa nyundo … siyo mabomu ya Gongo la Mboto, la hasha, eneo hilo linafuata nyayo za Kipawa, linapisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mwenyeji wangu, wakazi wa eneo hilo wamekwishalipwa fidia. Hivyo, walikuwa wakiendelea kubomoa nyumba zao ili kunusuru baadhi ya materials kama matofali, milango, madirisha na mabati.

Hapa kuna somo kwa serikali na Watanzania kwa ujumla – ni vema kuwa na mipango makini ya muda mfupi na muda mrefu. Wakati eneo hili lilipokuwa likijengeka, mamlaka mbalimbali zilikuwa zikiona … ilifahamika wazi kwamba kuna siku uwanja utahitaji kupanuliwa … kwa nini ‘stop’ isipigwe tangu mapema sana kabla ya kuwepo haja ya kuingia gharama ya kulipa fidia, kubomoa, kusafisha (na kujenga upya kwa upande wa wabomolewa)? Hii ni changamoto ambayo hujirudia kila uchao … mtu atavamia eneo linalopaswa kuwa la wazi … atachimba msingi … mchana kweupe … atapandisha jengo … mchana kweupe … karibu anamalizia … ndiyo mamlaka zinazohusika zinatoka usingizini … Wahenga walisema … kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa … TUJIFUNZE kutokana na makosa yetu.

Advertisements

Written by simbadeo

March 8, 2011 at 10:57 pm

Posted in Siasa na jamii

2 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Kweli kabisa inabidi tujifunze kutokana na makosa yetu.

  Lakini SHULE ngumu hasa ukizingatia hata viongozi wetu inaonyesha wanaongoza bila kujifunza!:-(

  Like

  Simon Kitururu

  March 9, 2011 at 2:59 am

  • Naam, Simon … kibaya zaidi ukianza kuwaonyesha makosa yao na mafunzo waliyotakiwa kujifunza … wanakuita mchochezi … Je, kwamtindo huu tutajenga nchi kweli? Ipo haja ya mabadiliko (kimtazamo, kiutendaji, kimiiko n.k.). Ulimwengu mzima ni kitabu – ni kitabu kilichojaa mafunzo kemkem kwetu na kwa jamii nzima – hebu basi tukifunue – tukisome – na kitusaidie katika kujiletea mabadiliko!

   Like

   simbadeo

   March 9, 2011 at 10:09 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: