simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Unawajibika … ndio … wewe!

leave a comment »

Nimependa ujumbe unaotangazwa na kampuni ya shughuli za usafi inayomiliki lori hilo. Ni ukweli usiopingika kwamba suala zima la usafi wa mazingira ni la kwetu sote. Ndio. Ni la kwako. Ni la kwangu. Kila mmoja wetu anawajibika. Bado tuna matatizo mengi sana – hasa upande wa tabia zetu – kuhusu namna tunavyoshughulika na taka tunazozizalisha kila uchao. Hivi, pale unapokula pipi, unaponunua vocha ya salio la simu, unapovuta sigara barabarani … tabia yako ikoje? Je, unapomaliza kunywa maji ya chupa uliyoyanunua … unajishughulisha vipi na kuhifadhi chupa hiyo? Ukichunguza sana katika njia hizi ndogondogo za uzalishaji taka … wengi wetu tuna hatia. Kwa hiyo, tubadilike.

Inahitajika elimu zaidi … kuanzia katika ngazi ya familia, katika mfumo rasmi wa elimu, katika sehemu za kazi na biashara, kwenye mikusanyiko ya hadhara, kwenye nyumba za ibada n.k. Inafaa kutumia pia mabango ya barabarani (fikiria kama mabango yaliyotumika wakati wa kampeni za uchaguzi yangebeba ujumbe wa usafi wa mazingira na tabia zinazotakikana katika kufanikisha uimarishaji wa tabia-rafiki wa mazingira), kupitia vyombo vya habari kama vile televisheni, redio, magazeti, vitabu, majarida, vipeperushi, blogu, kurasa za mitandao ya kijamii, ujumbe wa maneno kupitia simu za mkononi. Tunaweza kuleta mapinduzi ya kijani katika upande wa mazingira.

Hivi majuzi nilisikia tamko la Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mh Masaburi, akiahidi kuigeuza Dar es Salaam kuwa ya kijani. Hili ni tamko jema sana, lakini lisiishie kuwa maneno matupu. Tunafahamu kwamba Dar es Salaam kwa sasa ni ya kijani sana tu, na, kwa hili tunamkumbuka Mkuu wa Mkoa wa enzi zile, Mzee Yusuf Makamba. Alifanya juhudi kubwa. Kwa hiyo, Mstahiki Meya, karibu kwa tamko lako, lakini inahitajika kazi … matendo. Kauli hiyo haina budi kuenda sambamba na kuhakikisha Jiji linakuwa safi … safi kabisa. Tabia za watu kukojoa ovyo barabarani, watu kutupa taka ovyo, takataka kurundikana huku na kule, kukosekana kwa sehemu za umma za kukusanyia taka katika mitaa … vyote hivi havina budi kukoma.

Kuna suala la mifugo. Naelewa kwamba kuna wajasiriamali ambao hufuata kanuni zinazotakiwa za kuweka mifugo ya aina mbalimbali. Hawa waendelee. Lakini kuna wafugaji ambao hawazingatii kanuni za afya, hawajali kwamba mifugo nayo inahitaji sana kutunzwa kwa usafi wa hali ya juu, wengine wamejenga mabanda yao ya mifugo kwenye madirisha ya majirani zao. Kiafya, tabia hizi hazikubaliki. Ni vema kama mfugaji ana eneo kubwa, au ana shamba mahali pengine, basi ahamishie mifugo yake kule.

Tuzingatie afya ya jamii na kanuni zinazoongoza vitendo vyetu. Kuna uchafu pia wa sauti … kwa nini baa ifungulie muziki kwa sauti kubwa mpaka usiku wa manane? Zile sheria ndogondogo ziko wapi? Ni wakati sasa, Mh Meya na wenzako, kusimamia sheria hizo kwa dhati. Tunachotaka wananchi ni vitendo … Sisi tunaona, tunasikia, na tuna akili za kupima ili kubaini nini kinafanyika kwa manufaa yetu sote na kipi kinafanyika kwa manufaa ya wachache.

Nawakilisha.

Advertisements

Written by simbadeo

March 4, 2011 at 11:45 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: