simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Wito: Msaidie Christina … tafadhali

leave a comment »

Christina – alipokuwa mwenye afya njema

Christina – hali aliyo nayo sasa

MTOTO CHRISTINA ANAHITAJI MSAADA WAKO WA HALI NA MALI … Ujumbe kutoka kwa wazazi wake

Sisi wazazi wa Christina Nasson Masimba, Bw na Bi. Mwinjilisti Masimba, tuna ujasiri mbele za MUNGU kukushirikisha/kuwashirikisha hitaji la msaada ili kukidhi gharama za matibabu ya mtoto wetu mpendwa.

Christina ni binti mwenye umri wa miaka 6, akiwa ni mtoto wetu wa mwisho kati ya watatu ambao Bwana ametubarikia. Ni mtoto mchangamfu sana, na anayempenda Mungu wake.

Tangu tarehe 9 Septemba 2009, binti yetu huyo aliugua malaria ambayo inasadikika kupanda kichwani na kumpa shida kubwa katika ubongo wake. Na hiyo imekuwa ndiyo chanzo cha kuugua kwake mpaka sasa. Kufuatia kuumwa huko, Christana alilazwa na kutibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kagera (Bukoba Government Hospital) zaidi ya mara tatu. Baadaye Januari 2010, alilazwa pia katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma (Dodoma General Hospital) wakati tukiwa likizo, na kisha akalazwa tena Bukoba Government Hospital, tuliporudi kazini Bukoba baada ya likizo.

Christina katika hali yake ya sasa, akiwa hana furaha tena yakutosha, kutokana na kuugua kwa muda mrefu! Aidha, amelazimika kusimama Shule kwa ajili ya kutibiwa.

Ukweli Christina na sisi wazazi wake tunahitaji sana watu wenye mapenzi mema,(WASAMARIA LUKA 10:25-27) ili aweze kupata huduma ya matibabu ya kumfaa, Pia uone Christina akiwa tayari kwenda shule asubuhi, kabl;a ya kuumwa, alipenda sana kusoma nakufurahia Shule.

Kati ya Aprili na Agosti, 2010 ugonjwa ulizidi kuongezeka na kuonyesha dalili za kupooza baadhi ya viungo vyake upande wa mkono wake wa kuume. Tulijitahidi kwa kila hali kwa maombi na tiba lakini bado hali yake ilizidi kuwa mbaya kadri siku zilivyopita.

Mnamo mwezi Novemba 2010, madaktari wa Bukoba Government Hospital walitutaka twende katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa uchunguzi na matibabu zaidi. Baada ya vipimo na matibabu kwa zaidi ya mwezi mmoja bila mafanikio, madaktari wa Bugando Hospital walitupa rufaa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (Muhimbili National Hospital – MNH).
Muhimbili walitupokea tarehe 18 Novemba, 2010 na kumtibu mpaka 21 Desemba, 2010. Walijitahidi kupima kila kipimo walichofikiria na, pale walipohitaji kipimo kilichokuwa hakifanyiki hospitalini hapo, walituelekeza kukipata katika hospitali nyingine nasi tulitekeleza maelekezo yao. Kwa ujumla, vilifanywa vipimo 14 kama vilivyoainishwa hapa chini. Ndipo shida iliyompata alipougua kwa mara ya kwanza ikagundulika.

Vipimo alivyopimwa ni:

CT – Scan (Kichwa).
EEG – (kipimo cha utendaji kazi wa ubongo).
FBP – (kipimo cha damu) Normal.
Sickling test –(Negative).
HB electrophoresis AA.
Echocardiogram (ECG) – normal.
CXR (normal).
Abdominal ultrasound.
LFT (normal).
RFT (normal).
TCD NCA (Middle Cerebral Artery) – both normal.
PT, PTT and INR (all normal).
HIV screening (Negative).
EEG – (consistent with focal seizure disorder).

Hata hivyo, vipimo hivyo na matibabu aliyopatiwa havikuleta ufumbuzi au unafuu katika hali ya Christina, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya. Mnamo tarehe 20 Desemba, 2010 MNH walituruhusu (discharge) ili turejee nyumbani kwa kupitia Bugando Referal Hospital kwa kujigharamia, na kututaka turudi hospitalini hapo baada ya muda wa miezi miwili (2) ili waangalie hali yake.

Kwa kuzingatia gharama kubwa za usafiri, na ukweli kuwa hali ya mtoto ilikuwa inazidi kuwa mbaya, hatukuweza kwenda Bugando wala Bukoba. Badala yake, tulipata familia moja hapa Dar es Salaam iliyokubali kutupokea wakati tunaendelea kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya afya ya binti yetu.

Ndipo tulipochukua hatua nyingine ya imani, na kuaza kutafuta jinsi ya kupata matibabu mahali popote. Tuliendelea na huduma za maombezi na matibabu madogo madogo hapa Dar es Salaam na Dodoma. Wakati huo huo, tulianza mawasiliano na hospitali za India ili kuona uwezekano wa kupata uchunguzi wa ziada na matibabu nchini huko.

Hivi sasa nafasi ya matibabu imepatikana katika Hospitali ya Indraprastha Appolo, New Delhi, INDIA.

Mchanganuo wa gharama za safari na matibabu ya Christina katika hospitali hiyo ni kama ifuatavyo:

HITAJI *****BEI**** IDADI ****JUMLA

1 Pasi za Kusafiria ****75,000 ****3 ****225,000
2 Visa**** 150,000 ****3 ****450,000
3 Tiketi ****1,488,000 ****3 ****4,464,000
4 Uchunguzi (siku 7 za mwanzo)**** 8,680,000**** 1 ****8,680,000
5 Makazi nje ya Hospitali (siku ya 8 – 14)***** 1,550,000 ****1**** 1,550,000
6 Matibabu na Makazi (wiki 7 zinazofuata)**** 12,400,000**** 1**** 12,400,000
7 Madeni ya matibabu tangu Disemba, 2010 ****800,000 ****1**** 800,000

JUMLA ZINAZOHITAJIKA 28,569,000/- (T.Shs)

Kiasi hiki ni kikubwa sana kwa uwezo wetu, na tunaomba mchango wako wa kutuwezesha kukidhi gharama hizi. Kwa kadri Mungu atakavyokugusa rohoni, tutashukuru kupokea mchango wako kupitia katika yoyote kati ya akaunti zifuatazo:-

Jina la Akaunti: Nasson Richard Masimba
Benki: CRDB
Namba ya Akaunti: 011 205 709 1300

Jina la Akaunti: Nasson Richard Masimba
Benki: NBC
Namba ya Akaunti: 02 720 108 8567

Jina la Akaunti: Nasson Richard Masimba
Benki NMB
Namba ya Akaunti: 318 160 5859

Nasson Richard Masimba
MPESA 076 777 8583

Ahsante sana kwa hatua yako. Tunaamini kuwa, tukinia pamoja, tutapata ushindi na ushuhuda kwa MUNGU wetu.

Bw Nasson R. Masimba na Bi Mariam N. Masimba

Wazazi wa Christina

0784778583, 0715778583, 0767 778583; 0658778583, 0756930810

masimbar2005@yahoo.com

Unaweza pia kuwasiliana nasi au kupata maelezo zaidi kupitia namba zifuatazo, na MUNGU akubariki sana.

Chanzo: SwahiliTime blogu ya Da Chemi Che Mponda

===========================================

Tafakari kuhusu hali ya malaria nchini na nini kifanyike

1. Ipo haja kwa upande wa Tanzania Bara kujifunza kutoka kwa ndugu zao wa Zanzibar. Kule wamefaulu kwa asilimia kubwa sana kudhibiti malaria. Waliamua kwamba kutumia njia ya vyandarua peke yake – haitoshi kumaliza/kupunguza tatizo, hivyo, waliamua pia kupiga dawa kwenye makazi ya watu na kwenye mazalia ya mbu. Kwa njia hiyo, wamefaulu karibu kutokomeza tatizo hilo. Kwa nini sisi huku Bara tusiweze? Kwa nini Serikali isielekeze fedha katika kumaliza mbu kwa kupiga dawa kwenye makazi na mazalia ya mbu?

Kwa taarifa ya mafanikio ya Zanzibar, tembelea ukurasa huu wa mtandaoni wenye taarifa ya UNICEF http://www.unicefusa.org/news/news-from-the-field/in-tanzania-the-island-of.html
Kwa uchache: ….There are many reasons for Zanzibar’s success, said Dr. Abdulai Tinorgah, UNICEF Tanzania’s Chief of Child Survival and Development. Most importantly, however, was that the region tackled malaria from many angles—using several strategies at once.

“They used insecticide-treated bed nets [and] spraying of insecticide in houses,” said Dr. Tinorgah. “They scaled up access to correct treatment together with simple tests for diagnosing malaria, and they also scaled up preventive treatment during pregnancy…

2. Ni wakati sasa tuachane na siasa kwenye tatizo hili. Christina ni mmoja tu kati ya watu makumi elfu wanaoteswa na malaria kwa njia moja au nyingine. Uchumi wa kaya nyingi unahangaika kwa sababu pesa kidogo wanazopata huzitumia kujitibu badala ya kuwekeza kwenye miradi midogomidogo ya maendeleo au katika kujipatia huduma bora zaidi za malazi, mavazi, chakula, na elimu.

Advertisements

Written by simbadeo

March 1, 2011 at 10:36 am

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: