simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Wahisani kugomea kuisaidia Tanzania?

leave a comment »Kijana akijitafutia riziki kwa kuosha magari ya watu … gari dogo kama hilo hulipiwa kati ya shilingi 1,000 – 2,000 – bei ni maelewano.

Wahisani watafakari kuisadia Tanzania

Na Claud Mshana

WAKATI Serikali ikiendelea kuomba msaada wa dharura kukabiliana na upungufu wa fedha katika bajeti yake ya 2010/11 uliotokana na upungufu wa mapato, nchi wahisani zinazochangia Bajeti Kuu zimekiri kupokea ombi hilo na kwamba zinatafakari kabla ya kuamua watoe au la.

Ombi hilo la Serikali ni la pili kufuatia wafadhili kukataa kuchangia Bajeti Kuu ya Serikali mwishoni mwa mwaka jana baada kutoridhika na matumizi ya nyuma.

Mwaka jana nchi wahisani zilikataa kutoa Sh297 bilioni baada ya kutoridhika na utendaji wa Serikali katika kuharakisha maendeleo, kasi ndogo ya kutoa huduma bora za jamii na kushindwa kusimamia mfumo matumizi ya fedha za umma.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili, Ijumaa wiki hii, Mwenyekiti wa kundi la nchi zinazochangia Bajeti Kuu ya Serikali, Svein Baera, alisema hivi sasa wapo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha taarifa ya maamuzi yao.

“Tulihitaji kupitia kwanza taarifa ya uchumi ya Januari, tayari tumeshafanya hivyo na baada ya wiki chache tutaoa taarifa,” alisema Baera ambaye ni Balozi wa Norway nchini.

Baera alifahamisha kuwa taarifa yao ni ndefu na itatolewa kwa vyombo vya habari muda utakapofika.

Serikali inakabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha kwenye bajeti yake ya mwaka 2010/11 kutokana na makusanyo madogo ya mapato ya ndani na kile kilichodaiwa kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma
Katika kujikwamua na hali hiyo, Serikali iliamua kupiga panga bajeti za wizara zote ili kufidia upungufu huo wa Sh670.417 bilioni. Katika kutekeleza hilo kila wizara ilikatwa fedha zake za matumizi ya maendeleo na ya kawaida kulingana na ukubwa (wa kila wizara).

Kufuatia upungufu huo, Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Uchumi ililazimika kuomba msaada wa dharura kwa nchi wahisani. Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhani Khijja, iliandika barua ya kuomba msaada wa dharura kwa nchi mbalimbali zinazosaidia maendeleo ya Tanzania.

Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo alipotakiwa kuelezea suala hilo hivi karibuni alisema taarifa aliyoitoa Gavana wa Benki Kuu, Profesa Beno Ndulu kuhusu mwenendo wa uchumi Januari mwaka huu inatosha.
Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndulu alisema hakuna mfumuko wa bei unaoweza kuangusha uchumi wa nchi.

Ingawa alikiri kwamba kasi ya kukua kwa uchumi ni ndogo, alisisitiza kuwa kwa ujumla nchi inapiga hatua kimaendeleo.

Profesa Ndulu alisema tatizo lililopo ni watu kusahau walipotoka na kuona kama hakuna juhudi zinazofanyika, huku akitoa mifano ya kukua kwa pato la mtu mmojammoja kutoka Sh200 hadi 300, Sh500 badi 600 na sasa ni Sh1000.

Akilelezea kuhusu msaada ulioombwa na Serikali ya Tanzania, Balozi Baera alisema: “Nitazungumzia nchi yangu (Norway) kuhusinana na ombilo hilo. Hata hivyo, sisi nchi wahisani, kwa umjoa wetu tuliishatoa kiasi chote tulichopaswa kuchangia katika bajeti hadi kufikia Desemba 2010,” alisema.

Taarifa ya Uchumi Januari 2011

Hata hivyo, taarifa za Benki Kuu (BoT), kuhusu mapitio ya ukuaji wa uchumi ya Januari bado zinaonyesha kuwa kuna upungufu wa makusanyo ya mapato ya kodi.

Taarifa hiyo ya Benki Kuu inaonyesha kuwa kwa Desemba 2010, makusanyo ya mapato (mbali na vyanzo vya mapato vya mamlaka za serikali za mitaa) yalikuwa ni Sh 594 bilioni sawa na asilimia 91.1 ya makadirio yaliyowekwa.

Vile vile mapato yatokanayo na kodi kwa Desemba 2010 yalikuwa ni Sh 564.1 bilioni sawa na asilimia 90.5 ya makadirio yaliyowekwa, huku mapato yasiyotokana na kodi yakizidi kwa asilimia 3.7 ya Sh28.9 bilioni zilizokadiriwa.

Taarifa hiyo pia inaonyesha kuwa katika nusu ya kwanza ya mwaka wa bajeti 2010/11, makusanyo ya kodi yalifikia Sh2.55 trilioni sawa na asilimia 91.3 ya makadirio yaliyowekwa na makusanyo yasiyotokana na kodi yamefikia Sh157.2 bilioni sawa na asilimia 78.8.

Matumizi ya Serikali

Matumizi ya Serikali wakati wa mapitio hayo Januari, zinaonyesha kuwa kulikuwa na matumizi makubwa zaidi kwa asilimia 12.2 ya Sh898.8 bilioni zilizokadiriwa.

Katika matumizi hayo, fedha zilizokwenda kwenye matumizi ya kawaida ya Serikali ni Sh745.2 bilioni na fedha zilizoenda kwenye miradi ya maendeleo ni Sh 263.1 bn pekee.

Matumizi hayo yanazidi kuiweka Serikali katika wakati mgumu, kwani hivi karibuni Benki ya Dunia (WB) ilitoa masharti kumi kwa serikali ili iweze kunufaika na misaada ya WB kusaidia ya kupambana na umasikini.
Baadhi ya masharti hayo ynaitaka Serikali kuhakikisha kwamba inakuwa na miundombinu bora, kuboresha mazingira ya uwekezaji.

Taarifa WB ilisisitiza kuwa Serikali ya Tanzania inapaswa kuboresha mazingira ya kibiashara na huduma za umma.

Katika mkutano wa pamoja kati ya WB na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), uliofanyika mjini Washington, DC, Marekani, Serikali iliagiza kuwepo kwa matumizi mazuri ya rasilimali, kuongeza mapato ya ndani na kupunguza misamaha ya kodi kwa wawekezaji.


Chanzo: Mwananchi Jumapili, 27 Februari, 2011

Tafakari fupi

Utegemezi ni jambo baya sana. Bila shaka ni kutokana na kung’amua ubaya wa utegemezi kwamba Azimio la Arusha(1967) lilikuja na falsafa ya Ujamaa na Kujitegemea. Hata hivyo, Azimio hilo lilifikia ukomo baada ya Azimio la Zanzibar la 1992. Tanzania imekuwa tegemezi kwa wastani wa asilimia 40 ya bajeti yake kila mwaka. Kiwango hiki ni kikubwa sana. Kwa hiyo, haishangazi kwamba wahisani wanapoamua kubana misaada yao, hali ya uchumi wa nchi (ambayo kwa viwango vya ulimwengu ni mbaya) huwa inakuwa mbaya zaidi.

Binafsi nafikiri ipo haja ya kuchukua jitihada za makusudi kabisa na za waziwazi za kurekebisha hali hii … hatuna budi ‘kufunga mikanda’ katika namna tunavyotumia kile kidogo kinachoingia kwenye mifuko ya serikali. Ni kwa njia ya kubana matumizi, kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika matumizi ya serikali kwamba tutaweza kurekebisha sifa hii tuliyo nayo ya utegemezi. Nidhamu hiyo haina budi pia kuingia hata katika namna tunavyotumia rasilimali za nchi ili kuliiingizia Taifa kipato.

Kwa rasilimali tulizo nazo hatuna sababu hata moja kwa nini tuendelee kutegemea misaada na uhisani. Marekebisho yatawezekana na kwa kuweka uwazi, kufuata sheria na kanuni, kuhimiza uadilifu, na kuongoza watu kwa vitendo – hasa uwajibikaji.

Tuliombee Taifa letu ili liondokane na utegemezi. Pengine kukataa kwa wahisani kuchangia kwenye bajeti ya Taifa ni ‘wake up call’. Hivi kwa nini tusitumie fursa hii kujaribu kujitegemea … naelewa kwamba wananchi tupo tayari kufunga mikanda … lakini viongozi wa Serikali kuanzia ngazi ya juu kabisa hawana budi kuonyesha njia.

Vilevile kuna suala zima la aina ya ajira tunazotengeneza hapa nchini … hivi sasa tunazidi kupoteza mwelekeo … vijana wengi wanaoingia kwenye ajira hivi sasa … hawaingii kwenye ajira zenye kuzalisha moja kwa moja … bali ni zile ambazo hazina tija ya moja kwa moja kwa Taifa … Kuna tofauti kubwa kati ya kijana anaejipatia kipato kwa kuosha magari na yule anayejipatia kipato kwa kulima maharage … kati ya mchuuzi wa bidhaa rahisi zilizotengenezwa Uchina na yule anayechuuza matunda kutoka Matombo na kwingineko nchini … Tujitafakari kama Taifa kwa faida ya vizazi vya sasa na vile vijavyo …

Tusenti twangu tuwili!

Advertisements

Written by simbadeo

February 27, 2011 at 2:34 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: