simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Sitakishari Veterans … Bonanza

leave a comment »

Kikosi cha Air Wing Veterans … waliovaa jezi rangi ya orange …

Kikosi cha Tabata Kimanga Veterans … waliovaa jezi rangi nyeupe na nyekundu

Wachezaji wa vikosi vyote viwili wakisalimiana kabla ya mechi ya ufunguzi wa Bonanza …

Wachezaji wakisalimiana na wasimamizi wa ndani wa mchezo: kushoto ni Ashura Ukama, anayefuatia jina lake halikupatikana mara moja, kisha Salehe Magulu na kulia kabisa ni Asha Mohamed.

Wadau … kushoto kabisa mtangazaji akiendelea na shughuli ya kuhabarisha nini kinaendelea uwanjani

Wadau ambao walikuwa wamekwishawasili uwanjani … mambo ndiyo yalikuwa yanaanza

Kushoto ni MC Elly Ngwala, mratibu wa shughuli nzima. Kulia kwake ni mmoja wa wadau muhimu kutoka Sitakishari Veterans.

Bonanza hili limeandaliwa na Sitakishari Veterans. Kabla ya mechi ya ufunguzi, wote waliokuwa uwanjani walisimama kwa dakika moja ili kuwakumbuka wale waliopoteza maisha yao, kuumia, kupoteza mali zao au kuhangaika kwa namna moja au nyingine kutokana na milipuko ya mabomu ya hivi karibuni kule Gongo la Mboto. Katika tukio hilo, mmoja wa wachezaji wa timu ya Kitunda Veterans, Peter Mwambungu, alipoteza maisha. Mungu amweke yeye pamoja na marehemu wengine mahali pema peponi, Amina.

Hadi tunakwenda mitamboni … Timu ya Tabata Kimanga Veterans ilikuwa imekwishapata goli 1 – 0 dhidi ya Air Wing Veterans katika mechi ya ufunguzi.

Kwa ujumla kuna timu 14 zinazotarajiwa kushiriki ambapo jumla ya mechi 7 zitachezwa … zote ni leo hii … na

BONANZA linaendelea, hivyo msomaji wa blogu hii hujachelewa … fika kwenye viwanja vya Sitakishari karibu kabisa na Kituo cha Polisi Sitakishari ili ushiriki katika tukio hili.

Advertisements

Written by simbadeo

February 27, 2011 at 11:50 am

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: