simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Jumuiya ya Ulaya na Matokeo ya Uchaguzi Tanzania 2010 …

leave a comment »

Jumuiya Ya Ulaya Yawasilisha Taarifa Ya Mwisho Kuhusu Uchaguzi Mkuu 2010

Bw. David Martin akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Katikati ni Mchambuzi wa maswala ya Sheria na Uchaguzi Bi. Tania Marques pamoja na Afisa Habari wa Kaimisheni ya Uangalizi wa uchaguzi ya Umoja wa Ulaya Bi. Francesca Boggeri

Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi Mkuu Nchini Tanzania, Bwana David Martin, amewasilisha taarifa ya mwisho leo kuhusu uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 31 Oktoba 2010.

Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Juimuiya ya Ulaya (EU EOM) ulikuwepo nchini Tanzania kuanzia tarehe 29 Septemba hadi tarehe 28 Novemba 2010, kufuatia mwaliko wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania.

Ujumbe wa EU EOM ulisambaza waangalizi wa uchaguzi 103 katika mikoa yote 26 nchini Tanzania kutoka nchi zote 27 wanachama wa Jumuiya ya Ulaya pamoja na nchi za Canada, Norway na Switzerland ili kufuatilia kwa umakini jinsi gani mchakato mzima wa uchaguzi ulikuwa ukiendeshwa kulingana na kanuni na mapatano ya kimataifa na kikanda pamoja na sheria za Tanzania.

“Lengo la taarifa hii ya mwisho ni kutoa mapendekezo na ushauri wenye nia ya kudumisha demokrasia nchini Tanzania”, alisema Mwangalizi Mkuu wa Uchaguzi Bwana David Martin, Mbunge katika Bunge la Ulaya.

“Mapendekezo na ushauri vinavyotolewa katika taarifa hii haviilazimishi wala kuiamuru asasi au taasisi yoyote kuyatendea kazi bali yanapaswa kujadiliwa kwa kuzingatia historia, jiografia na mila na desturi za nchi hii.

Kutokana na majadiliano niliyofanya na viongozi mbalimbali nchini nina imani kuwa serikali, vyama mbalimbali vya upinzani, asasi za kiraia na umma watashiriki kikamilifu katika kujadili sheria na taratibu za uchaguzi zinazotakiwa kufanyiwa marekebisho.

Kwa sababu hiyo, tunatiwa moyo sana na maoni yaliyotolewa na Rais Kikwete pamoja na Spika kuwa taarifa yetu itahakikiwa sambamba na mchakato wa marekebisho ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo, ninaomba nieleweke vema kuwa kwa kutoa taarifa hii hatuitishi mjadala kuhusu uhalali wa matokeo ya uchaguzi. Nilipokuja mara ya mwisho nchini nilisema kwamba kipimo cha mwisho cha uchaguzi ni: “Je, wananchi waliipata serikali waliyoipigia kura? Nchini Tanzania naamini wananchi waliipata.”

Ripoti inatoa matokeo ya ufuatiliaji wa uchaguzi na mapendekezo ya kina yenye lengo la kuboresha chaguzi zijazo katika maeneo yote ya mchakato wa uchaguzi. Yafuatayo ni mapendekezo muhimu ya Ujumbe wa EU EOM:

-Kipindi cha kampeni kinapaswa kisizidi mwezi mmoja. Kipindi kirefu cha uchaguzi kinaweza kuididimiza ari ya wapiga kura na kuvitwisha mzigo mkubwa kifedha vyama vidogo vya siasa.
-Tume za NEC na ZEC hazina budi kuchukua hatua makusudi kudumisha uwazi katika ngazi zake zote za utendaji.

Tume za uchaguzi zinapaswa kuchapisha na kusambaza kwa wakati mwafaka zana muhimu za kiufundi za uchaguzi kama vile: orodha ya vituo vya kupigia kura, orodha ya majimbo ya uchaguzi, orodha ya wapiga kura na taarifa kuhusiana na fedha za umma zilizotolewa kwa ajili ya kampeni.

Hata hivyo, Ujumbe wa EU EOM ulivunjwa moyo sana kutokana na ukosefu wa uwazi katika ujumuishaji wa matokeo ya uchaguzi upande wa Tanzania Bara na Zanzibar.
-Haki ya kusimama kwenye uchaguzi haipaswi kuwanufaisha wanachama wa vyama mbalimbali vya siasa tu ila inapaswa kuwanufaisha na wagombea binafsi.

-Tume za NEC na ZEC zinapaswa kuwa asasi huru mbali na serikali ili kupunguza utegemezi wake kwenye miundo ya serikali za mitaa na hasa zinapaswa kuwa huru kuteua makamishna wa kuziongoza.

-Pia ili kudumisha uwazi katika mchakato wa uchaguzi, vyombo vya habari vianapaswa viruhusiwe kuvitembelea vituo vya uchaguzi siku ya uchaguzi. Jambo hili litahitaji kuwepo na mwongozo maalumu ambao unaweza kuandaliwa na tume za uchaguzi kwa ushirikiano na Baraza la Vyombo vya Habari (MCT).

-Mipaka ya majimbo ya uchaguzi haina budi kufanyiwa marekebisho ili kuhakikisha kila jimbo linalandana na idadi ya watu iliyopo jimboni.

-Haki ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais inapaswa kutolewa kwa kuanzisha sheria kulingana na kanuni za kimataifa zilizoridhiwa na Tanzania.
-Idara ya mahakama inapaswa kuwa na mamlaka wazi ya kusimamia utendaji na maamuzi yanayotolewa na tume za uchaguzi.

Ujumbe wa EU EOM unatoa shukrani za dhati kwa Watanzania kwa ushirikiano ulioupata wakati wote wa mchakato wa uchaguzi.

Taarifa kamili katika lugha ya Kiingereza inapatikana katika tovuti ya Ujumbe wa EU EOM.

Nimeitoa hii kwenye blog ya Majjid Mjengwa.

Ipo haja ya kujitafakari kama Taifa … wapi tunatoka, wapi tupo, wapi tunakwenda … Mungu Ibariki Tanzania … upepo wa Tunisia, Misri, Aljeria, Yemeni, Jodani … upite kwa namna tunazoweza kuzimudu kiungwana …

Advertisements

Written by simbadeo

February 12, 2011 at 6:19 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: