simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Matokeo ya kidato cha nne …. Nini cha kufanya …

with 6 comments

Webpage ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inayoonyesha matokeo hayo: http://www.moe.go.tz/NectaResults/olevel.htm

Serikali kutoa kauli matokeo kidato cha nne

JIBU LA SWALI LA MBUNGE MBOZI MAGHARIBI

na Irene Mark na Danson Kaijage, Dodoma

KUTOKANA na matokeo mabovu ya mtihani wa Kidato cha Nne Serikali inatarajia kutoa kauli bungeni ili Watanzania na wadau wa elimu waelewe chanzo na sababu za wanafunzi kufeli sana.

Ahadi hiyo ilitolewa bungeni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe (CHADEMA) aliyetaka kujua mpango wa makusudi unaochukuliwa na serikali kuhusu matokeo hayo aliyoyaita kuwa ni janga, ambapo asilimia 51 ya watahiniwa wa mtihani huo walifeli.

Mbowe alisema matokeo ya kidato cha nne yanaashiria janga kubwa na wanafunzi wengi waliomaliza kidato cha nne kushindwa kuendelea na masomo ya juu.

Kiongozi huyo ambaye ni Mbunge wa Hai aliitaka serikali kueleza mpango wa dharura ili wanafunzi walioshindwa mitihani wasiendelee kuzagaa mitaani ikiwemo kuboresha shule za kata ambazo ziliongoza kwa matokeo mabaya ya kidato cha nne.

Kutokana na swali hilo waziri mkuu alilazimika kusimama na kulitolea ufafanuzi na kudai kuwa TAMISEMI pamoja na Wizara ya Elimu wameunda jopo la kuangalia ni jinsi gani ya kuweza kutatua janga la matokeo mabovu yaliyojitokeza na kuwashtua Watanzania wengi na wafau wa elimu.

Alisema baada ya jopo hilo kumaliza kazi yake itatoa maelezo na maelekezo amabayo yatatolewa kauli bungeni ili wananchi waweze kutambua tatizo la kutokea kwa matokeo hayo.

Mbali na hilo, Pinda aliwataka wazazi kuhakikisha wanashirikiana na bodi za shule ili kuangalia ni jinsi gani ya kuchangia chakula kwa ajili ya wanafunzi kupata mlo wa mchana badala ya watoto kushinda njaa.

Awali katika swali la msingi Mbunge wa Mbozi Magharibi David Silinde (CHADEMA) aliitaka serikali kueleza Bunge ni hatua gani zitachukuliwa kwa majengo ambayo hayajakamilika na ni kwa nini serikali isisitishe kuwapangia wananchi kiwango cha michango ujenzi wa sekondari badala yake wananchi wakubaliane kuchanga kutokana na kiwango cha kipato chao.

Pia mbunge huyo alitaka kujua ni kwanini serikali isianze kujenga mabweni ya wasichana kwenye sekondari za kata ili kupunguza ongezeko la wanafunzi wa kike kupata mimba wakiwa mashuleni.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Agrrey Mwanri, alisema serikali haina utaratibu wa kuwapangia wananchi viwango vya michango ambavyo wanatakiwa kuchangia.

Alisema michango hupitishwa na bodi ya shule husika kwa kukubaliana na kamati kwa kuwashirikisha wazazi wa maeneo husika kutoka na mahitaji ya shule hiyo kwani bodi ndiyo wenye mamlaka na wala si magizo ya serikali.

Chanzo cha habari: Tanzania Daima 10 Februari 2011.

Tafakari binafsi

Pamoja na yote yaliyoelezwa hapo. Ningependa kusisitiza jambo moja. Matokeo ya mitihani ya Taifa kwa Kidato cha Nne 2010 yamekuwa mabaya. Wakati ambapo hatuna budi kuacha kutupiana lawama na kutafutana uchawi au kunyoosheana vidole. Sote kama Taifa tuna wajibu kwa matokeo hayo.

Sote hatuna budi kutafuta namna gani tunawasaidia vijana wetu walioshindwa kwenye mitihani hiyo. Kama wazazi au walezi tushirikiane kuweka mkakati wa kutoa nasaha kwa vijana walioshindwa ili kwamba wasijione kana kwamba thamani ya utu wao imepotea. La hasha. Tuwatie matumaini. Tuwape miongozo kuhusu namna gani wanaweza kujaribu tena (kurudia kufanya mitihani), au kutafuta njia nyingine ya kuwasaidia kujenga maisha yao na wao kutoa mchango wao kwa ujenzi wa Taifa hili. Hatuna budi kama Taifa kuwa na mkakati wa pamoja katika kutekeleza jambo hili. Waheshimiwa Wabunge wetu na madiwani wawe vinara katika jambo hili. Pengine hapa waingie vilevile viongozi wa dini kupitia nyumba zao za ibada, asasi zisizo za kiserikali na hata zile za kiserikali. Sote kwa pamoja tuandae ‘uponyaji wa KiTaifa’ kwa ajili ya vijana wetu. Wamejeruhiwa vibaya. Tusizidi kuchokonoa majeraha yao hayo kwa maneno na matendo bali tuwasaidie katika kuponya majeraha hayo kwa kuwapa NASAHA inayostahiki.

Tujue kwamba tusipofanya hivyo, tena mapema, tutakuwa ni Taifa la watu ambao asilimia fulani ni watu wasiojiamini, watu wasioamini kwamba wanaweza kufanya vema hata kama walianguka mara ya kwanza na ya pili na ya tatu. Tuwatie moyo kwamba WANAWEZA kujiletea maisha bora kwa kufanya bidii zaidi na kujifunza kutokana na kushindwa kwao safari hii. Hawana budi pia kuelewa kwamba thamani ya utu wao ileile – haijapungua hata chembe kwa matokeo hayo. Wazazi na walezi … na tuanze mara moja uponyaji huu …

Mungu Ibariki Tanzania.

Advertisements

Written by simbadeo

February 10, 2011 at 10:50 am

Posted in Siasa na jamii

6 Responses

Subscribe to comments with RSS.

 1. Changamoto hii imeanza kujitokeza mwaka huu wa 2008 hata kabla ya kutimia miaka mitano tangu kuanza kwa zoezi hili…..Matokeo ya Kidato cha Nne….21. Mheshimiwa Spika naomba nitumie fursa hii kufafanua changamoto inayotokana na Matokeo ya Kidato cha Nne.

  Like

  Monex

  February 11, 2011 at 1:57 am

 2. jwpalzlwvqktnksgpput, obxuclfkon , [url=http://www.otwivfxmxi.com]yowaxqdpia[/url], http://www.nkpbcaldep.com obxuclfkon

  Like

  lppswtxsry

  February 23, 2011 at 9:50 pm

 3. linwqqeznrioviqaufzw, yaryeqlwtj , [url=http://www.qxpqktxhls.com]drqkznmxyo[/url], http://www.xadxcsvpps.com yaryeqlwtj

  Like

  prnqnpnzra

  February 24, 2011 at 2:57 am

 4. yvffnaeiqfywwkdvoboj, qmsovwqbnc , [url=http://www.oazggojchj.com]eoicvnspbx[/url], http://www.ukmcapmlac.com qmsovwqbnc

  Like

  afullwndzh

  February 24, 2011 at 8:03 am

 5. jrrlcbzagbqkzorrmshy, wepzuplvjz , [url=http://www.amjmssojfc.com]sikdrwtoel[/url], http://www.afpqbofyom.com wepzuplvjz

  Like

  dzeihxlnih

  February 24, 2011 at 1:22 pm

 6. wange shirikishwa wananchi kwa kila hali pamoja na wazazi ili kuwasaidia watoto wetu

  Like

  robert mhina

  August 12, 2011 at 4:21 am


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: