simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Jaffar Sabodo … moyo wa kizalendo

with 4 comments

Akina dada kama hawa huenda watanufaika sana na mradi uliobuniwa na kufadhiliwa na Mh. Jaffar Sabodo.

Sabodo atoa bil. 1.8/- za visima nchi nzima

na Mwandishi wetu

MFANYABIASHARA, Jaffar Sabodo, ametoa sh bilioni 1.8 kwa ajili ya kuchimba visima 600 nchi nzima, ambavyo vitawasaidia wananchi kupata maji ya uhakika maeneo ya vijijini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Sabodo alisema anajua wananchi wanapata shida ya maji, hivyo amehamasika kusaidia kwa kuamua kuwachimbia visima ambavyo vitawezesha kupata maji.

Sabodo alisema kutokana na wananchi kugubikwa na ukosefu wa maji hasa vijijini, ni vema wakajengewa visima ambavyo vitasaidia kupata maji ya uhakika na kuondokana na utekaji wa maji katika umbali mrefu .

Alisema kwa uzalendo wake ameona kuna haja ya kusaidia kuchimba visima kwa gharama hiyo kama sehemu ya mchango wake katika taifa lake.

“Maji yanayopatikana kwa mfumo wa bomba hayakidhi haja, hivyo kuwa na visima ni sehemu ya kutatua matatizo ya maji kwa wananchi,” alisema.

Mfadhili huyo alisema ameunda kamati ambayo itafuatilia maombi ya visima nchi nzima kwa kutoa fedha pamoja na wataalamu wa kuchimba visima na mitambo.

Baada ya kutoa msaada huo wa kuchimba visima kupitia tangazo katika vyombo vya habari, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Professa Mark Mwandosya alifunga safari ya kumshukuru Sabodo kwa kusaidia sekta ya maji kwa visima hivyo 600.

Mwandosya alisema mchango huo wa Sabodo unatekeleza sehemu ya sera ya sekta ya maji yenye lengo la kuhakikisha kila mwananchi anapata maji kwa uhakika.

Chanzo cha Habari: Tanzania Daima 3 Februari 2011

Tafakari binafsi:

Upatikanaji wa maji safi, salama na ya uhakika ni changamoto kubwa nchini kwetu. Kasi ya ukuaji wa idadi ya watu iko juu sana kuliko uwezo wa serikali kuwapatia wananchi huduma za msingi, hususan, maji. Blogu hii inapongeza moyo wa uzalendo ambao Mzee Sabodo amekuwa akiuonyesha kwa vitendo. Kuna mengi ambayo amekuwa akitufundisha, kubwa kabisa ni KUJALI UTU wa MWENZAKO pasipo kuangalia huyu ni wa dini, imani, itikadi, rangi au daraja gani. Ninaamini Watanzania wengi sana tutaguswa na mradi huu – kwa maana ya kutumia matunda ya mradi huo – kwa njia moja au nyingine. Mungu Ibariki Tanzania yetu.

Written by simbadeo

February 3, 2011 at 9:32 am

Posted in Siasa na jamii

4 Responses

Subscribe to comments with RSS.

  1. i love it

    Like

    facebook

    February 17, 2011 at 2:19 pm

  2. kaka nahitaji kumuona huyu muheshimiwa hata nikipata address yake ntashukuru
    gwijimimi@gmail.com

    Like

    gwiji

    November 3, 2011 at 11:23 am

  3. Nampongeza sana mr sabodo kwa moyo wake wa kujitolea mungu ambariki

    Like

    Alex fredrick

    June 1, 2012 at 8:05 pm

  4. Naitaji ku exchange ideas nae mr sabodo atupe changamoto sie vijana ambao ni wajasiliamali wadogo

    Like

    Alex fredrick

    June 1, 2012 at 8:08 pm


Leave a comment