simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Teknolojia … Maarifa ya Kienyeji

leave a comment »

Picha inaonyesha ghala la kuhifadhia nafaka. Ghala hilo limetengenezwa kwa maarifa ya kienyeji. Katika ghala hilo mtu anaweza kuhifadhi chakula/nafaka kwa muda mrefu pasipo kuharibiwa na mvua wala wadudu.

Jamii zetu zilikuwa (kwa kiasi fulani bado zinayo) na maarifa mengi sana ya kisayansi: kwenye tiba, kwenye vyakula, katika uzazi, katika viwanda vidogovidogo vya kutengeneza zana za uzalishaji, mipango ya vita na kujihami, mipango ya utawala, uendelezaji vizazi, mbinu za kupanua himaya, matunzo bora ya ardhi na mazingira (vikiwemo vyanzo vya maji, wanyama, ndege na viumbe wengine).

Ili Afrika ijikomboe, ni vema kutafiti maarifa waliyokuwa nayo wahenga wetu … tuyachukue, tuyaendeleze, tuyaongezee ubora ili yawe yenye ufanisi zaidi. Waarabu walipokuja, walitulaghai na kubeza maarifa yetu, wakatufanya tuamini kwamba ‘kila kitu chetu ni cha kishenzi’, Wanzungu nao hivyohivyo. Tukatae hali hiyo. Tujikomboe ili kujiletea maendeleo yetu. Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania.

Picha ni kwa hisani ya rafiki yangu: F. O. Kitipa aliyekuwa mikoa ya kusini hivi karibuni.

Advertisements

Written by simbadeo

February 1, 2011 at 1:02 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: