simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Tanesco … na shida ya maji

leave a comment »

Vijana wauza maji kutoka viunga vya Tabata hadi Segerea wakiwa katika moja ya visima vichache ambamo maji yanapatikana katika maeneo hayo. Kwa siku kadhaa sasa eneo la Segerea limekuwa bila umeme. Vivyo hivyo, eneo la Tabata limekuwa bila umeme kwa siku tatu mfululizo. Kukosekana huko kwa umeme kumesababisha watu kukosa huduma ya maji, kwani maeneo hayo kwa kiasi kikubwa yanategemea maji kutoka katika visima binafsi vya watu. Si wote katika hao wenye kutoa huduma hiyo walio na jenereta, wengi hutegemea umeme wa Tanesco ili kupampu maji kutoka ardhini kabla ya kuyauza kwa wauzaji wadogowadogo. Jambo hilo limefanya dumu moja la maji lenye ujazo wa lita 20 kuuzwa kwa kati ya shilingi 400 hadi 600. Pengine ni vema tatizo hilo linalowakabili wakazi wa eneo hilo lishughulikiwe … maana baada ya kitambo kifupi tutaanza kusikia habari za milipuko ya magonjwa kwa sababu ya uhaba wa maji. Ni wito.

Advertisements

Written by simbadeo

January 31, 2011 at 12:52 am

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: