simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Ujasiriamali … mbinu

leave a comment »

Tuna ya kujifunza kwa mjasiriamali huyu:

1. Kuipenda kazi yako – jamaa anaipenda kazi yake. Ukikaa karibu kwa muda wa dakika tano, nawe ni mchunguzi, utagundua mara moja jinsi kijana huyu anavyoipenda kazi yake.

2. Usiweke mayai yako yote kwenye sinia moja – bila shaka mnafahamu msemo huo – nadhani tumechukua kwa Waingereza – huyu bwana anafanya diversification ya bidhaa na huduma anazotoa. Lazima tu akupate ukikatiza katika anga zake: ana embe Tanga (anazoziandaa vizuri tu); ana nanasi (nalo analiandaa vizuri); ana matango; siku nyingine anakuwa pia na ndizi mbivu. Je, hapo kwa upande wa matunda atakukosa kweli hata kwenye tunda aina mojawapo? Sidhani. Vilevile ana karanga na ana sigara. Hii ni mbinu muhimu sana miongoni wa wajasiriamali wenye mafanikio.

3. Ana uthubutu – kwa biashara yake na nyingine nyingi za namna hii – hekaheka za askari wa jiji/manispaa ni lazima. Kumbe anathubutu kubeba risk. Anaona ni vema asikae tu nyumbani bali awe mtaani na kuwasogezea watu huduma. Katiba inamruhusu kuwa mahali popote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ana haki ya kujitafutia kipato kilicho halali – ili mradi hamkabi mtu.

Kingine kilichonifurahisha kwa huyu bwana ni kwamba bidhaa zake zote ni ‘made in hapahapa’. Hakuna bidhaa ya mchina hapo. Anatufundisha uzalendo – kupenda vya kwetu kwanza. Ni mwalimu mzuri huyu. Au siyo?

Wakati umefika tuvifanyie kazi vipaumbele vyetu. Kama tunataka watu wasihamie mijini kwa matumaini ya kujipatia maisha bora, hatuna budi kuwapelekea mifumo ya ajira rasmi huko waliko. Miundombinu bora ya kilimo, viwanda vya usindikaji vya ngazi ya kwanza na ya kati. Watu watakuja mjini kufanya utalii tu na si kuhamia na kujiingiza kwenye biashara ndogondogo.

Advertisements

Written by simbadeo

January 25, 2011 at 11:07 pm

Posted in Siasa na jamii

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: