simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Serikali ya mtaa … na barabara

with one comment

Aliyeongoza kikao cha wakazi wa Mtaa wa King’azi, Kata ya Kwembe, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, Mzee Mkodomi, pamoja na viongozi wengine katika meza kuu.

Baadhi ya wajumbe/washiriki katika mkutano huo …

Mmoja wa wajumbe akisisitiza jambo …

Nilipata fursa ya kushiriki kwenye kikao kilichoitishwa na Serikali ya Mtaa wa King’azi. Mkutano ulikuwa uanze saa 8 mchana. Lakini ulianza saa 11 jioni. Moja ya sababu kubwa za kuchelewa huko ni msiba uliokuwa jirani. Ilikuwa siku ya kuzika. Kwa hiyo wajumbe wengi walikwenda kushiriki kwenye msiba kama ilivyo ada yetu Watanzania.

Ajenda kuu ya mkutano ilikuwa kuhusu kupatikana kwa barabara za mitaa katika eneo hilo. Ilitolewa hoja kwamba barabara ni moja katika miundo mbinu muhimu ya kusaidia kusogeza huduma za jamii karibu na watu. Kwa hiyo, ni muhimu karibu kila kiwanja/shamba kufikika kwa barabara. Hata hivyo, kumekuwepo na migogoro mingi kuhusina na suala la upatikanaji wa barabara, hasa kwa viwanja/mashamba yaliyo ndanindani. Kwa hiyo, kumekuwepo na haja ya kuhakikisha kwamba zinapatikana barabara za mitaa kwa lengo la kusaidia kupunguza migogoro na vilevile kuweka matayarisho ya kusogeza huduma muhimu za kijamii zikiwemo umeme na maji.

Wajumbe wa mkutano walijadiliana kwa kina kuhusu ajenda kuu na hatimaye kukubaliana kwamba ziainishwe barabara ‘kuu’ za mitaa. Kwa hiyo, wajumbe walishiriki kwa kutaja barabara hizo za viungo kutoka kiwanja kimoja hadi kingine. Hatimaye zilipatikana barabara zisizopungua 12.

Pamoja na mambo mengine, ilielezwa kwamba upana wa barabara hizo unapaswa kuwa kati ya mita 6 hadi 7. Na kwamba eneo la barabara litapatikana kwa kumega kiasi sawasawa cha ardhi kutoka kila upande.

Baadhi ya wajumbe walisisitiza sana kuhakikisha kwamba zoezi hilo linafanyika kwa haki na pasipo upendeleo. Ilisisitizwa kwamba utendaji wa haki ndiyo njia pekee ya kuondoa migogoro inayoweza kusababishwa na jukumu hilo.

Ili kufanikisha zoezi hilo, kila barabara iliundiwa kamati ambapo kila kamati itakuwa na majukumu ya kusimamia zoezi la upatikanaji barabara na vilevile ukusanyaji wa fedha za kununulia mafuta yatakayotumika kwenye grader. Manispaa itatoa grader pamoja na kumlipa dereva. Wananchi watatoa maeneo (pasipo fidia) pamoja na kuchangia mafuta.

Kikao kilimalizika saa 12.30 jioni. Utekelezaji utafuatia siku za hivi karibuni.

Nyongeza. Ni jambo la muhimu sana kuzipa nguvu serikali za mitaa katika kusimamia masuala yanayowagusa wananchi wa maeneo yanayohusika kwani viongozi katika ngazi hiyo ndiyo wanaofahamu vema yale yanayowasibu wananchi hao. Hata hivyo, ni muhimu kuona namna gani serikali hizi zinafanya kazi katika namna inayoendana na sheria za nchi pamoja na kanuni zinazoongoza utekelezaji wa sheria hizo. Suala la ardhi ni suala nyeti na unyeti wake unazidi kadiri siku zinavyokwenda mbele. Nawakilisha.

Advertisements

Written by simbadeo

January 24, 2011 at 10:21 am

Posted in Siasa na jamii

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. Zanzibar i Tanzania är en härlig plats även under regnperioden. Det är lugnt och ofta lite folk på stränderna. Regnperioden är som balsam för plånboken, då alla hotell på Zanzibar har superrea för att ens fylla upp några av sina rum. Regnet är ofta på natten så det är värt att chansa.

    Like


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: