simbadeo2000

WAZA MPAKA BASI (THINK TO NO END).com weblog NOTE: Views or opinions expressed in this blog do NOT in any way represent those of any organisation, community, association, company, circle of friends, religious or ethnic group to which I am associated with.

Mwalimu afariki akifundisha …

with one comment

Tumetoka mavumbini, tutarudi mavumbini … In honour of Mwalimu Emaculata.

Mwalimu afariki akifundisha darasani

na Berensi Alikadi, Bukoba

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida na ya kusikitisha mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Kabalimu B ameanguka na kufariki akiwa darasani.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Sintarwa Shakanyi, amemtaja mwalimu huyo aliyefariki kuwa ni Emaculata Nchumaye (53) mkazi wa mtaa wa Mapinduzi katika mamlaka ya mji mdogo wa Bunda.

Akisimulia tukio hilo mwalimu mkuu huyo alisema mwalimu huyo alifikwa na mauti juzi Januari 20 majira ya saa 6 mchana wakati akiwa darasani akifundisha somo la sayansi darasa la nne na kwamba hicho kilikuwa kipindi chake cha sita tangu asubuhi ya siku hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya mwalimu Shakani ni kwamba wakati mwalimu huyo akiendelea kufundisha wanafunzi ghafla walimuona akianguka chini na kupoteza fahamu ambapo wanafunzi hao waliokuwemo darasani walikimbia na kutoa taarifa kwa walimu wengine ambao walifika na kumchukua na kumkimbiza katika hosptali teule ya DDH.

“Baada ya kuanguka wanafunzi walikimbia na kuwaarifu walimu ambao walifika haraka na kumchukua na kumkumbiza katika hospital ya DDH na kwamba alipofikishwa na kupimwa madaktari waliwaambia kuwa tayari alikuwa ameshafariki,’’ alisema mwalimu mkuu huyo huku akibubujikwa na machozi.

Naye kijana wa mwalimu huyo (marehemu), Emanuel Mnada, alisema kuwa mama yake aliondoka siku hiyo majira ya asubuhi na kuwaaga kuwa anakwenda kazini na kwamba hakuwa na dalili zozote za kuugua na wala hakuwaeleza kuwa anaumwa hadi muda wa saa sita ambapo alipoletewa taarifa na mwanafunzi mmoja wa shule hiyo kuwa mama yake ameanguka darasani na amepelekwa hosptalini.

Kijana huyo alifafanua kuwa baada ya kupata taarifa hizo alikwenda moja kwa moja hosptalini hapo na kuonana na madaktari ambao walimueleza kuwa mama yake tayari alikuwa ameshafariki jambo ambalo alidai lilimshutua sana.

Hata hivyo taarifa toka kwa ndugu zake wa karibu zilidai kuwa siku za nyuma mwalimu huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na kwamba pengine wanahisi ndicho chanzo cha kifo chake.

Akizungumzia kifo cha mwalimu huyo mwenyekiti wa chama cha walimu wilaya ya Bunda, mwalimu Saulo Ruhumbika, alisema kuwa kifo hicho ni pigo kwa chama hicho kwa kuondokewa na mwanachama wake lakini pia mwalimu huyo alikuwa mchapakazi na aliyezingatia maadili ya kazi yake.

Kwa mujibu wa maelezo ya wanafamilia mazishi ya mwalimu huyo yanatarajiwa kufanyika leo katika kijiji cha Kungo’mbe nje kidogo na mji wa Bunda mara baada ya kutolewa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.

Chanzo: Tanzania Daima, 22 Januari 2011

Nimeguswa sana na tukio hili la mwalimu kukutwa na mauti yake wakati akiendelea kutimiza wajibu wake. Nadhani ipo haja ya kumtangaza kuwa ni mmoja wa mashujaa ambao wamepoteza uhai wao wakati wakiendelea kulitumikia Taifa hili. Habari hapo juu inasema kuwa alianguka wakati alipokuwa akifundisha kipindi chake cha sita (6) katika siku hiyo. Hii ndiyo hali halisi ya mfanyakazi wa kawaida nchini Tanzania. Ana majukumu mengi. Anajitoa mhanga kupita kiasi lakini malipo yake … chunguza utakuta kwamba pengine ni asilimia 15 tu ya kile ambacho angestahili. Tumuenzi mama huyu. Pengine Chama cha Walimu kichukue jukumu la kuona namna gani mama huyu anakumbukwa vizazi vingi vijavyo. Pumzika kwa amani Mama Mwalimu Emaculata.

Advertisements

Written by simbadeo

January 22, 2011 at 7:58 pm

Posted in Siasa na jamii

One Response

Subscribe to comments with RSS.

  1. Taaluma ya ualimu ni nzuri sn ila Serikali inatukatisha tamaa kwa bahati mbaya kn baadhi ya maeneo waalimu hawathamiwi hata na jamii but mwenzetu amekufa kishujaa hakika tutamuenzi. Maisha bora ya waalimu yapo Mwese Mpanda ktk mkoa wa Katavi waalimu karibuni sn

    Like

    Mwalimu

    January 23, 2011 at 10:43 pm


Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

%d bloggers like this: